以西結書 32 – CCBT & NEN

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

以西結書 32:1-32

為法老唱哀歌

1第十二年十二月一日,耶和華對我說: 2「人子啊,你要為埃及王法老唱哀歌,對他說,

『你自認為是列邦中的雄獅,

其實你像激蕩江河、

用腳把江河攪渾的海怪。

3主耶和華說,

我要差遣多國組成的大軍,

用我的網把你拉上來,

4拋在地上,丟在田野,

給天上的飛鳥吃,

讓地上的走獸飽餐。

5我要把你的肉丟在山間,

把你的屍首填滿山谷,

6用你的血澆灌大地,

漫過群山,溢滿溝壑。

7當我消滅你的時候,

我要用雲遮蔽天空,

使日月無光,星辰昏暗。

8我要遮蔽天上所有的光,

使黑暗籠罩你的四境。

這是主耶和華說的。

9「『我把你滅亡的消息帶到你不認識的列邦時,必使許多人惶恐不安。 10我在他們面前揮刀攻擊你的時候,各國的人都必因你而驚駭,他們的君王必膽戰心驚。在你傾覆那天,他們都必時刻為自己的性命戰戰兢兢。』

11「主耶和華這樣說,『巴比倫王的刀必來攻擊你。 12我要使你的人民喪身在各國中最殘暴的勇士刀下。

『他們必摧毀埃及的驕傲,

消滅她的人民。

13我要殺盡她河邊的牲畜,

使人足獸蹄不再攪渾河水。

14我要使埃及的河流清澈見底,

像油一樣緩緩流淌。

這是主耶和華說的。

15我要使埃及的土地荒涼,

毀滅其中的居民,

那時他們就知道我是耶和華。

16「『這是列國為埃及唱的哀歌,各國的婦女要為埃及和她的人民唱這哀歌。這是主耶和華說的。』」

17第十二年十二月十五日,耶和華對我說: 18「人子啊,為埃及的百姓哀哭吧!我要把她與各強國的人民一同送入陰間。

19埃及啊,你比誰更美呢?

你下去跟未受割禮的人躺在一起吧!

20埃及人要倒斃在喪身刀下的人當中。刀已出鞘,她和她的國民要被拖走。 21英勇的統領要在陰間談論埃及王和他的盟友說,『這些喪身刀下、未受割禮的人下來長眠了。』

22亞述和她的大軍都在那裡,她周圍是她大軍的墳墓。他們都是喪身刀下的人。 23他們的墳墓在陰間的最深處,她的大軍躺臥在她墳墓的周圍。他們生前曾使人恐懼,如今卻喪身刀下。 24以攔在那裡,她的百姓在她墳墓的周圍。他們都未受割禮,喪身刀下,下到了陰間。他們生前曾使人恐懼,如今卻和下墳墓的人一同抱愧蒙羞。 25以攔躺臥在被殺的人當中,周圍是她百姓的墳墓。他們都未受割禮、喪身刀下。他們生前曾使人恐懼,如今卻和喪身刀下的人在一起,與下墳墓的人一同抱愧蒙羞。

26米設土巴都在那裡,周圍是她們百姓的墳墓。他們都未受割禮,生前曾使人恐懼,如今卻喪身刀下。 27他們沒有古代32·27 古代」有古卷作「未受割禮的」。勇士的榮耀葬禮,那些勇士帶著兵器下到陰間,頭枕著刀,屍骨上蓋著盾,生前曾使人恐懼。

28「法老啊,你要被毀滅,跟那些未受割禮、喪身刀下的人躺在一起。

29以東也在那裡,她的王侯儘管力量強大,卻和喪身刀下的人在一起,與那些未受割禮、下墳墓的人躺在一起。

30「北方的諸王和所有的西頓人也在那裡,雖然他們力量強大,令人恐懼,卻羞辱地與被殺的人下到了陰間。他們未受割禮,與喪身刀下的人躺在一起,與下墳墓的人一同蒙羞。

31「法老看見這些人,便得到了安慰,因為並非只有他的軍隊被殺。這是主耶和華說的。 32我使法老生前給人帶來恐懼,但他和他的百姓最後還是要躺臥在未受割禮、喪身刀下的人當中。這是主耶和華說的。」

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Ezekieli 32:1-32

Maombolezo Kwa Ajili Ya Farao

132:1 Eze 31:1; 33:21Katika mwaka wa kumi na mbili, mwezi wa kumi na mbili, siku ya kwanza ya mwezi, neno la Bwana likanijia, kusema: 232:2 2Sam 1:17; 2Nya 35:25; 2Fal 24:1; Nah 2:11-13; Ay 41:31; Eze 29:3; Ay 3:8; Eze 34:18; 2Sam 3:33“Mwanadamu, fanya maombolezo kwa ajili ya Farao mfalme wa Misri na umwambie:

“ ‘Wewe ni kama simba miongoni mwa mataifa,

wewe ni kama joka kubwa baharini,

unayevuruga maji kwa miguu yako

na kuchafua vijito.

332:3 Eze 12:13; Hab 1:15“ ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:

“ ‘Nikiwa pamoja na wingi mkubwa wa watu

nitautupa wavu wangu juu yako,

nao watakukokota katika wavu wangu.

432:4 Isa 18:6; 1Sam 17:44-46; Eze 39:4-5; 31:12-13Nitakutupa nchi kavu

na kukuvurumisha uwanjani.

Nitawafanya ndege wote wa angani watue juu yako

na wanyama wote wa nchi

watajishibisha nyama yako.

532:5 Eze 31:12Nitatawanya nyama yako juu ya milima

na kujaza mabonde kwa mabaki yako.

632:6 Isa 34:3; Eze 29:5Nitailowanisha nchi kwa damu yako inayotiririka

njia yote hadi milimani,

nayo mabonde yatajazwa na nyama yako.

732:7 Yoe 3:15; Mt 24:29; Ufu 6:12; Isa 34:4; Eze 30:3; Yoe 2:2Nitakapokuzimisha, nitafunika mbingu

na kuzitia nyota zake giza;

nitalifunika jua kwa wingu,

nao mwezi hautatoa nuru yake.

832:8 Za 102:26; Ay 9:7; Yer 4:23; Yoe 2:10Mianga yote itoayo nuru angani

nitaitia giza juu yako;

nitaleta giza juu ya nchi yako,

asema Bwana Mwenyezi.

9Nitaifadhaisha mioyo ya mataifa mengi

nitakapokuangamiza miongoni mwa mataifa,

nikikuleta uhamishoni miongoni mwa nchi

ambazo haujapata kuzijua.

1032:10 Yer 46:10; Eze 26:16; Ufu 18:9-10; Isa 30:32; Eze 27:35; 30:9Nitayafanya mataifa mengi wakustaajabie,

wafalme wao watatetemeka

kwa hofu kwa ajili yako

nitakapotikisa upanga wangu mbele yao.

Siku ya anguko lako

kila mmoja wao atatetemeka

kila dakika kwa ajili ya maisha yake.

1132:11 Isa 19:4; Yer 46:26; Eze 21:19; 46:13; 29:19“ ‘Kwa kuwa hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:

“ ‘Upanga wa mfalme wa Babeli

utakuja dhidi yako.

1232:12 Eze 28:7; 31:11-12Nitafanya makundi yako ya wajeuri kuanguka

kwa panga za watu mashujaa,

taifa katili kuliko mataifa yote.

Watakivunjavunja kiburi cha Misri,

nayo makundi yake yote

ya wajeuri yatashindwa.

1332:13 Eze 29:8-11Nitaangamiza mifugo yake yote

wanaojilisha kando ya maji mengi,

hayatavurugwa tena kwa mguu wa mwanadamu

wala kwato za mnyama

hazitayachafua tena.

14Kisha nitafanya maji yake yatulie

na kufanya vijito vyake

vitiririke kama mafuta,

asema Bwana Mwenyezi.

1532:15 Kut 7:5; Za 107:33-34; Kut 14:4; 18Nitakapoifanya Misri kuwa ukiwa

na kuiondolea nchi kila kitu

kilichomo ndani yake,

nitakapowapiga wote waishio humo,

ndipo watakapojua kuwa

Mimi ndimi Bwana.’

1632:16 Mwa 50:10; 2Sam 1:17; Eze 26:17; 19:1“Hili ndilo ombolezo watakalomwimbia. Binti za mataifa wataliimba, kwa kuwa Misri na makundi yake yote ya wajeuri wataliimba, asema Bwana Mwenyezi.”

17Katika mwaka wa kumi na mbili, mwezi wa kwanza, siku ya kumi na tano ya mwezi, neno la Bwana likanijia kusema: 1832:18 Yer 1:10; Mik 1:8; Eze 26:20; 31:14-16; 32:1“Mwanadamu, omboleza kwa ajili ya makundi ya wajeuri wa Misri na uwatupe kuzimu yeye na binti za mataifa yenye nguvu, waende huko pamoja nao washukao shimoni. 1932:19 Eze 28:10; 31:18Je, ninyi mnamzidi nani kwa uzuri? Shukeni chini! Nanyi mkalazwe pamoja na hao wasiotahiriwa! 2032:20 Za 28:3; Eze 31:17-18Wataanguka miongoni mwa wale waliouawa kwa upanga. Upanga umefutwa, mwache aburutwe mbali pamoja na hao wajeuri wake wote. 2132:21 Isa 14:9; Eze 28:10Kutoka kuzimu viongozi hodari watanena kuhusu Misri pamoja na wale walioungana nao, ‘Wameshuka chini, nao wamelala kimya pamoja na hao wasiotahiriwa, pamoja na wale waliouawa kwa upanga.’

2232:22 Eze 32:24, 26, 29, 30“Ashuru yuko huko pamoja na jeshi lake lote, amezungukwa na makaburi ya watu wake wote waliouawa, wale wote walioanguka kwa upanga. 2332:23 Isa 14:15; Nah 1:14Makaburi yao yako kwenye kina cha chini cha shimo na jeshi lake limelala kulizunguka kaburi lake. Wote waliokuwa wameeneza hofu kuu katika nchi ya walio hai wameuawa, wameanguka kwa upanga.

2432:24 Mwa 10:22; Yer 49:37; Ay 28:13; Eze 26:20“Elamu yuko huko, pamoja na makundi yake yote ya wajeuri wakiwa wamelizunguka kaburi lake. Wote wameuawa, wameanguka kwa upanga. Wote waliokuwa wameeneza hofu katika nchi ya walio hai walishuka kuzimu bila kutahiriwa. Wanaichukua aibu yao pamoja na wale washukao shimoni. 2532:25 Eze 28:10; 28:10Kitanda kimetandikwa kwa ajili yake miongoni mwa waliouawa, pamoja na makundi yake yote ya wajeuri wakiwa wamelizunguka kaburi lake. Wote ni watu wasiotahiriwa, wameuawa kwa upanga. Kwa sababu vitisho vyao vilienea katika nchi ya walio hai, wameichukua aibu yao pamoja na wale washukao shimoni, nao wamewekwa miongoni mwa waliouawa.

2632:26 Mwa 10:2; Eze 27:13“Mesheki na Tubali wako humo, pamoja na makundi yao ya wajeuri wakiwa wameyazunguka makaburi yao. Wote hawakutahiriwa, wameuawa kwa upanga kwa sababu walieneza vitisho vyao katika nchi ya walio hai. 27Je, hawakulala na mashujaa wengine wasiotahiriwa waliouawa, ambao wameshuka kaburini wakiwa na silaha zao za vita, ambao panga zao ziliwekwa chini ya vichwa vyao na uovu wao juu ya mifupa yao? Adhabu kwa ajili ya dhambi zao ilikuwa juu ya mifupa yao, ingawa vitisho vya mashujaa hawa vilikuwa vimeenea hadi kwenye nchi ya walio hai.

28“Wewe pia, ee Farao, utavunjwa nawe utalala miongoni mwa wasiotahiriwa, pamoja na wale waliouawa kwa upanga.

2932:29 Za 137:7; Eze 25:12-14; 35:15; Yer 49:7; Isa 34:5-15“Edomu yuko humo, wafalme wake wote na wakuu wake wote, ambao ijapokuwa wana nguvu, wamelazwa pamoja na wale waliouawa kwa upanga. Wamelala pamoja na wasiotahiriwa, pamoja na wale washukao shimoni.

3032:30 Isa 14:31; Yer 25:26; Mwa 10:15; Eze 38:6; Yer 25:22; Eze 28:10; 28:8“Wakuu wote wa kaskazini na Wasidoni wote wako huko, wameshuka chini pamoja na waliouawa kwa aibu ijapokuwa kuna vitisho vilivyosababishwa na nguvu zao. Wamelala bila kutahiriwa pamoja na wale waliouawa kwa upanga na kuchukua aibu yao pamoja na wale washukao chini shimoni.

3132:31 Eze 14:22; 31:16“Farao, yeye pamoja na jeshi lake lote, atakapowaona atafarijiwa kwa ajili ya makundi yake yote ya wajeuri, wale waliouawa kwa upanga, asema Bwana Mwenyezi. 3232:32 Yer 44:30; Ay 3:14Ingawa nilimfanya Farao aeneze vitisho vyake katika nchi ya walio hai, Farao pamoja na makundi yake yote ya wajeuri watalazwa miongoni mwa wasiotahiriwa, pamoja na wale waliouawa kwa upanga, asema Bwana Mwenyezi.”