马太福音 12 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

马太福音 12:1-50

安息日的问题

1那时,耶稣在安息日经过一片麦田。祂的门徒饿了,便随手搓麦穗吃。 2法利赛人看见后,对耶稣说:“你看,你的门徒做了在安息日不准做的事!”

3耶稣回答说:“你们没有读过大卫的事迹吗?当时他和部下饿了, 4进入上帝的殿,吃了献给上帝的供饼。这饼只有祭司才可以吃,大卫和部下是不准吃的。 5此外律法书又记载,安息日,祭司在圣殿里触犯了守安息日的规条也不算有罪。你们没有读过吗? 6我告诉你们,这里有一人比圣殿更伟大, 7如果你们明白‘我喜爱怜悯之心,而非祭物’这句经文的意义,就不会冤枉无辜了。 8因为人子是安息日的主。”

9耶稣离开那里,走进会堂, 10里面有个人,一只手是萎缩的。法利赛人企图找借口控告耶稣,就问祂:“安息日可不可以医病呢?”

11耶稣回答说:“如果你们有一只羊在安息日掉进坑里,难道你们不把它拉上来吗? 12人比羊要贵重多了!所以在安息日行善合情合理。”

13于是,耶稣转过身来对那人说:“把手伸出来!”那人一伸手,手就复原了,跟另一只手一样健康。 14法利赛人却走了出去,策划怎样除掉耶稣。

上帝的仆人

15耶稣知道了,就离开那个地方。很多人跟随祂,耶稣医好了其中所有患病的人, 16吩咐他们不要泄露祂的身份。 17这是要应验以赛亚先知的话:

18“看啊!我所拣选、

所眷爱、所喜悦的仆人,

我要将我的灵赐给祂,

祂要向万邦宣扬正义。

19祂不争竞,不喧嚷,

街上也听不见祂的声音。

20压伤的芦苇,祂不折断;

将残的灯火,祂不吹灭;

祂终必使正义得胜。

21普世都要仰望祂的圣名。”

22有人带一个被鬼附身、又瞎又哑的人来见耶稣,耶稣便医好他,使他能说能看。 23众人都很惊奇,就说:“这人会不会是大卫的那个后裔?” 24法利赛人听见后却说:“祂不过是靠鬼王别西卜赶鬼罢了。”

25耶稣知道他们的心思,就说:“一个国内部自相纷争,必然灭亡;一座城、一个家内部自相纷争,必然崩溃。 26若撒旦驱逐撒旦,就是自相纷争,它的国怎能维持呢? 27若我是靠别西卜赶鬼,你们的子弟又是靠谁赶鬼呢?为此,他们要审判你们。 28若我是靠上帝的灵赶鬼,就是上帝的国已降临在你们中间了。

29“人如何进入壮汉家中抢夺他的财物呢?除非先把那壮汉捆绑起来,才有可能抢劫他的家。

30“不与我为友就是与我为敌;不助我召集就是故意拆散。 31所以我告诉你们,一切的罪和亵渎的话都可以得到赦免,但亵渎圣灵的罪必得不到赦免。 32说话得罪人子的,还可以得到赦免;但那些说话冒犯圣灵的,今生永世都得不到赦免。

树与果

33“好树结好果子,坏树结坏果子,看果子就能知道树的好坏。 34你们这些毒蛇的后代!你们心里邪恶,又怎能讲出好话呢?因为心里充满的,口里自然会说出来。 35善人心存良善,就从他里面发出良善;恶人心存邪恶,就从他里面发出邪恶。 36我告诉你们,在审判之日,人将为自己所说的每一句闲话负责, 37因为将来要凭你口中的话来判断你是否有罪。”

求神迹

38当时,有几个律法教师和法利赛人对耶稣说:“老师,我们想要看你行个神迹。” 39耶稣回答说:“一个邪恶淫乱的世代想看神迹,可是除了约拿先知的神迹以外,再没有神迹给他们看。 40约拿在大鱼腹中三日三夜,人子也要在地里三日三夜。 41在审判的日子,尼尼微人和这世代的人都要起来12:41 起来”或作“复活”。尼尼微人要定这个世代的罪,因为他们听到约拿的宣告,就悔改了。看啊!这里有一人比约拿更伟大。 42在审判的日子,南方的女王和这世代的人都要起来,她要定这个世代的罪,因为她曾不远千里来听所罗门王的智言慧语。看啊!这里有一人比所罗门王更伟大。

乘虚而入

43“有一个污鬼离开了它以前所附的人,在干旱无水之地四处游荡,寻找安歇之处,却没有找到。 44于是它说,‘我要回到老地方。’它回去后,看见里面空着,打扫得又干净又整齐, 45就去带来了七个比自己更邪恶的鬼一起住在那里。那人的下场比从前更惨了。这个邪恶的世代也会这样。”

真正的亲属

46耶稣还在和众人说话的时候,祂的母亲和兄弟站在外面,想要跟祂说话。 47有人告诉祂:“你的母亲和兄弟在外面有话要跟你说。”

48耶稣说:“谁是我的母亲?谁是我的兄弟?” 49祂伸出手来指着门徒说:“你们看!这些人就是我的母亲和我的兄弟。 50凡遵行我天父旨意的人都是我的弟兄、姊妹和母亲。”

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Mathayo 12:1-50

Bwana Wa Sabato

(Marko 2:23-28; Luka 6:1-5)

112:1 Kum 23:25Wakati huo Yesu alipitia kwenye mashamba ya nafaka siku ya Sabato. Wanafunzi wake walikuwa na njaa, nao wakaanza kuvunja masuke ya nafaka na kuyala. 212:2 Kut 20:10; Yn 9:6Lakini Mafarisayo walipoona jambo hili, wakamwambia, “Tazama! Wanafunzi wako wanafanya jambo lisilo halali kufanywa siku ya Sabato.”

312:3 1Sam 21:1-6Yesu akawajibu, “Je, hamjasoma alichofanya Daudi na wenzake walipokuwa na njaa? 412:4 Law 24:5-9Aliingia katika nyumba ya Mungu, akala mikate iliyowekwa wakfu, yeye na wenzake, jambo ambalo halikuwa halali kwao kufanya, isipokuwa makuhani peke yao. 512:5 Hes 28:9-10; Yn 7:22-23Au hamjasoma katika Sheria kwamba siku ya Sabato makuhani huvunja sheria ya Sabato Hekaluni lakini hawahesabiwi kuwa na hatia? 612:6 Mt 12:41-42Nawaambia wazi kwamba, yeye aliye mkuu kuliko Hekalu yupo hapa. 712:7 Hos 6:6; Mt 9:13Kama mngekuwa mmejua maana ya maneno haya, ‘Nataka rehema, wala si dhabihu,’ msingewalaumu watu wasio na hatia, 812:8 Mt 8:20kwa maana Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa Sabato.”

Yesu Anamponya Mtu Aliyepooza Mkono

(Marko 3:1-6; Luka 6:6-11)

912:9 Mk 3:1; Lk 6:6Yesu akaondoka mahali hapo, akaingia ndani ya sinagogi lao, 1012:10 Lk 14:3; Yn 9:6na huko alikuwepo mtu aliyepooza mkono. Wakitafuta sababu ya kumshtaki Yesu, wakamuuliza, “Je, ni halali kuponya siku ya Sabato?”

1112:11 Lk 15:5Yesu akawaambia, “Ni nani miongoni mwenu, mwenye kondoo wake ambaye huyo kondoo akitumbukia shimoni siku ya Sabato hatamtoa? 1212:12 Mt 6:26; 10:31Mtu ana thamani kubwa kuliko kondoo. Kwa hiyo ni halali kutenda mema siku ya Sabato.”

13Ndipo akamwambia yule mtu, “Nyoosha mkono wako.” Akaunyoosha, nao ukaponywa ukawa mzima kama ule mwingine. 1412:14 Mwa 37:18; Yn 11:53Lakini Mafarisayo wakatoka nje, wakafanya shauri baya juu ya Yesu jinsi watakavyoweza kumuua.

Mtumishi Aliyechaguliwa Na Mungu

1512:15 Mt 4:23Lakini Yesu alipoyatambua mawazo yao, akaondoka mahali hapo. Watu wengi wakamfuata, naye akawaponya wagonjwa wao wote, 1612:16 Mt 8:4akiwakataza wasiseme yeye ni nani. 1712:17 Isa 42:1-4; 41:9Hii ilikuwa ili litimie lile neno lililonenwa kwa kinywa cha nabii Isaya kusema:

1812:18 Mt 3:7; Isa 42:1-4; 41:9“Tazama mtumishi wangu niliyemchagua,

mpendwa wangu, ninayependezwa naye.

Nitaweka Roho wangu juu yake,

naye atatangaza haki kwa mataifa.

19Hatagombana wala hatapiga kelele,

wala hakuna atakayesikia sauti yake njiani.

20Mwanzi uliopondeka hatauvunja,

na utambi unaofuka moshi hatauzima,

mpaka atakapoifanya haki ishinde.

2112:21 Isa 42:1-4Katika Jina lake mataifa

wataweka tumaini lao.”

Yesu Na Beelzebuli

(Marko 3:20-30; Luka 11:14-23)

2212:22 Mt 4:24; 9:32-33Kisha wakamletea mtu aliyekuwa amepagawa na pepo mchafu, na alikuwa kipofu na bubu. Yesu akamponya, hata akaweza kusema na kuona. 2312:23 Mt 9:27Watu wote wakashangaa na kusema, “Je, yawezekana huyu ndiye Mwana wa Daudi?”

2412:24 Mk 3:22; Mt 9:34Lakini Mafarisayo waliposikia jambo hili wakasema, “Mtu huyu anatoa pepo wachafu kwa uwezo wa Beelzebuli,12:24 Beelzebuli au Beelzebubu; pia 12:27. mkuu wa pepo wachafu.”

2512:25 Mt 9:4Yesu alijua walichokuwa wakiwaza, hivyo akawaambia, “Kila ufalme ukigawanyika dhidi yake wenyewe huangamia. Hali kadhalika kila mji au watu wa nyumba moja waliogawanyika dhidi yao wenyewe hawawezi kusimama. 2612:26 Mt 4:10Kama Shetani akimtoa Shetani, atakuwa amegawanyika yeye mwenyewe. Basi ufalme wake utawezaje kusimama? 2712:27 Mdo 19:13Nami kama natoa pepo wachafu kwa nguvu za Beelzebuli, watu wenu je, wao hutoa pepo wachafu kwa uwezo wa nani? Hivyo basi, wao ndio watakaowahukumu. 2812:28 1Yn 3:8; Mt 3:2Lakini kama mimi ninatoa pepo wachafu kwa Roho wa Mungu, basi Ufalme wa Mungu umekuja juu yenu.

2912:29 Isa 49:24-25; Lk 11:21-22“Au tena, mtu awezaje kuingia katika nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuteka nyara mali zake asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu? Akishamfunga, ndipo hakika anaweza kuteka nyara mali zake.

3012:30 Mk 9:40; Yn 11:52; Lk 11:23“Mtu asiyekuwa pamoja nami yu kinyume nami, na mtu ambaye hakusanyi pamoja nami, hutawanya. 3112:31 Mk 3:28-29; Lk 12:10Kwa hiyo nawaambia, kila dhambi na kufuru watu watasamehewa, lakini mtu atakayemkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa. 3212:32 Tit 2:12; Efe 1:21; Ebr 6:5Mtu yeyote atakayesema neno dhidi ya Mwana wa Adamu atasamehewa, lakini yeyote anenaye neno dhidi ya Roho Mtakatifu hatasamehewa, iwe katika ulimwengu huu au katika ulimwengu ujao.

Mti Na Matunda Yake

(Luka 6:43-45)

3312:33 Mt 7:16-17; Lk 6:43-44“Ufanye mti kuwa mzuri, nayo matunda yake yatakuwa mazuri. Au ufanye mti kuwa mbaya, na matunda yake yatakuwa mabaya. Kwa maana mti hutambulika kwa matunda yake. 3412:34 Mt 3:7; 23:33; 15:18; Yn 8:43Enyi uzao wa nyoka! Mnawezaje kunena mambo mema, wakati ninyi ni waovu? Kwa maana kinywa cha mtu huyanena yale yaliyoujaza moyo wake. 3512:35 Lk 6:45Mtu mwema hutoa yaliyo mema kutoka hazina ya mambo mema yaliyohifadhiwa ndani yake, naye mtu mwovu hutoa yaliyo maovu kutoka hazina ya mambo maovu yaliyohifadhiwa ndani yake. 36Lakini nawaambia, katika siku ya hukumu watu watatoa hesabu kuhusu kila neno lisilo maana walilonena. 37Kwa maana kwa maneno yako utahesabiwa haki, na kwa maneno yako utahukumiwa.”

Ishara Ya Yona

(Marko 8:11-12; Luka 11:29-32)

3812:38 Yn 6:30; 1Kor 1:22Kisha baadhi ya Mafarisayo na walimu wa sheria wakamwambia, “Mwalimu, tunataka kuona ishara kutoka kwako.”

3912:39 Yn 1:7; Mt 8:20; 16:21Lakini yeye akawajibu, “Kizazi kiovu na cha uzinzi kinaomba ishara! Lakini hakitapewa ishara yoyote isipokuwa ile ishara ya nabii Yona. 4012:40 Yn 2:1, 2; 1:17; Mt 8:20; 16:21Kwa maana kama vile Yona alivyokuwa ndani ya tumbo la nyangumi12:40 Nyangumi ni samaki mkubwa sana. kwa siku tatu, usiku na mchana, vivyo hivyo Mwana wa Adamu atakuwa katika moyo wa nchi siku tatu, usiku na mchana. 4112:41 Yn 1:2; 3:15Siku ya hukumu watu wa Ninawi watasimama pamoja na kizazi hiki na kukihukumu; kwa maana wao walitubu waliposikia mahubiri ya Yona. Na tazama, hapa yupo yeye aliye mkuu kuliko Yona. 4212:42 1Fal 10:2; 2Nya 9:1Malkia wa Kusini atasimama wakati wa hukumu na kukihukumu kizazi hiki. Kwa kuwa yeye alikuja kutoka miisho ya dunia ili kuisikiliza hekima ya Solomoni. Na hapa yupo aliye mkuu kuliko Solomoni.”

Mafundisho Kuhusu Pepo Mchafu

(Luka 11:24-26)

43“Pepo mchafu amtokapo mtu, hutangatanga katika sehemu zisizo na maji akitafuta mahali pa kupumzika, lakini hapati. 44Ndipo husema, ‘Nitarudi kwenye nyumba yangu nilikotoka.’ Naye arudipo huikuta ile nyumba ikiwa tupu, imefagiliwa na kupangwa vizuri. 4512:45 2Pet 2:20Kisha huenda na kuwaleta pepo wachafu wengine saba wabaya kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo. Nayo hali ya mwisho ya yule mtu huwa ni mbaya kuliko ile ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kiovu.”

Mama Na Ndugu Zake Yesu

(Marko 3:31-35; Luka 8:19-21)

4612:46 Lk 11:24; Ay 1:7; 1Pet 5:8Wakati alikuwa angali anazungumza na makutano, mama yake na ndugu zake wakasimama nje wakitaka kuongea naye. 47Ndipo mtu mmoja akamwambia, “Tazama, mama yako na ndugu zako wamesimama nje, wanataka kuongea na wewe.”

4812:48 Lk 2:49Lakini yeye akamjibu na kumwambia yule mtu, “Mama yangu ni nani, nao ndugu zangu ni nani?” 49Akawanyooshea mkono wanafunzi wake, akasema, “Hawa hapa ndio mama yangu na ndugu zangu! 5012:50 Mt 6:10; Yn 15:14Kwa maana yeyote afanyaye mapenzi ya Baba yangu wa mbinguni, huyo ndiye ndugu yangu, na dada yangu na mama yangu.”