雅歌 8 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

雅歌 8:1-14

1如果你是我的同胞兄弟就好了。

这样,在外头遇见你,

我也可以亲吻你,

没有人会取笑我。

2我可以把你带进我母亲的家——她教养了我。

我要给你喝石榴汁酿的醇酒。

3你的左手扶着我的头,

右手紧抱着我。

4耶路撒冷的少女啊,

我恳求你们,

不要叫醒或惊动爱情,

等它自发吧。

耶路撒冷的少女:

5那从旷野上来、靠在良人身旁的是谁呢?

女子:

我在苹果树下唤醒你,

你母亲在那里怀你养你,

为你受生产之苦。

6请把我印在你的心上,

刻在你的手臂上,

因为爱情如死亡一般坚固,

嫉妒像阴间一样残酷,

它燃起的火焰是烧灭一切的烈火。

7爱情,大水不能熄灭,

江河不能淹没。

若有人想倾其家财买爱情,

必遭唾弃。

女子的兄长:

8我们有一个小妹,

她的胸脯还没有发育。

若有人来提亲,

我们该怎么办?

9她若是墙,

我们要在上面建造银塔;

她若是门,

我们要用香柏木板围护她。

女子:

10我是一面墙,

双乳像城楼,

我在他眼中像找到平安的人。

11所罗门巴力·哈们有一个葡萄园,

他把葡萄园租给农夫,

租金是每人一千块银子。

12我的葡萄园,我自己作主。

所罗门啊,你的一千块银子自己留着,

二百块银子给管果园的人。

男子:

13你这住在园中的人啊,

同伴们都在聆听你的声音,

求你让我也听见吧!

女子:

14我的良人啊,

愿你像香草山上的羚羊和小鹿,

快快来到我身边!

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Wimbo 8:1-14

18:1 Mit 9:2; Wim 3:4Laiti ungelikuwa kwangu kama ndugu wa kiume,

ambaye aliyanyonya matiti ya mama yangu!

Kisha, kama ningekukuta huko nje,

ningelikubusu,

wala hakuna mtu yeyote angelinidharau.

2Ningelikuongoza na kukuleta

katika nyumba ya mama yangu,

yeye ambaye amenifundisha.

Ningelikupa divai iliyokolezwa unywe,

asali ya maua ya mikomamanga yangu.

38:3 Wim 2:6Mkono wake wa kushoto uko chini ya kichwa changu,

na mkono wake wa kuume unanikumbatia.

48:4 Wim 2:7; 3:5Binti za Yerusalemu, ninawaagiza:

msichochee wala kuamsha mapenzi

hata yatakapotaka yenyewe.

Shairi La Sita

Marafiki

58:5 Wim 3:4-6; Yn 17:14Ni nani huyu anayekuja kutoka nyikani

akimwegemea mpenzi wake?

Mpendwa

Nilikuamsha chini ya mtofaa,

huko mama yako alipotunga mimba yako,

huko yeye alipata utungu akakuzaa.

68:6 Wim 1:2; Hes 5:14; Hag 2:23; Isa 49:16Nitie kama muhuri moyoni mwako,

kama muhuri kwenye mkono wako;

kwa maana upendo una nguvu kama mauti,

wivu wake ni mkatili kama kuzimu.

Unachoma kama mwali wa moto,

kama mwali mkubwa wa moto wa Bwana hasa.

78:7 Mit 6:35Maji mengi hayawezi kuuzimisha upendo,

mito haiwezi kuugharikisha.

Kama mtu angelitoa mali yote ya nyumbani mwake

kwa ajili ya upendo,

angelidharauliwa kabisa.

Marafiki

8Tunaye dada mdogo,

matiti yake hayajakua bado.

Tutafanya nini kwa ajili ya dada yetu

wakati atakapokuja kuposwa?

9Kama yeye ni ukuta,

tutajenga minara ya fedha juu yake.

Na kama yeye ni mlango,

tutamzungushia mbao za mierezi.

Mpendwa

108:10 Kol 2:7; Eze 16:7Mimi ni ukuta,

nayo matiti yangu ni kama minara.

Ndivyo ambavyo nimekuwa machoni pake

kama yule anayeleta utoshelevu.

118:11 Mhu 2:4; Mt 21:33; Isa 7:23Solomoni alikuwa na shamba la mizabibu huko Baal-Hamoni;

alikodisha shamba lake la mizabibu kwa wapangaji.

Kila mmoja angeleta kwa ajili ya matunda yake

shekeli 1,0008:11 Shekeli 1,000 ni kama kilo 11.5. za fedha.

12Lakini shamba langu la mizabibu

ambalo ni langu mwenyewe

ni langu kutoa;

hizo shekeli 1,000 ni kwa ajili yako, ee Solomoni,

na shekeli mia mbili8:12 Shekeli 200 ni kama kilo 2.3. ni kwa ajili

ya wale wanaotunza matunda yake.

Mpenzi

138:13 Wim 2:14Wewe ukaaye bustanini

pamoja na marafiki mliohudhuria,

hebu nisikie sauti yako!

Mpendwa

148:14 Mit 5:19; Wim 2:8-17Njoo, mpenzi wangu,

uwe kama swala

au kama ayala kijana

juu ya milima iliyojaa vikolezo.