那鸿书 1 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

那鸿书 1:1-15

1以下是关于尼尼微的预言,是伊勒歌斯那鸿的启示书。

耶和华向尼尼微发怒

2耶和华是痛恨不贞、施行报应的上帝。

耶和华施行报应,充满烈怒。

耶和华报应祂的仇敌,向他们发烈怒。

3耶和华不轻易发怒,有伟大的能力。

耶和华断不以有罪的为无罪。

祂行走在旋风和暴风中,

云彩是祂脚下的尘土。

4祂斥责大海,使大海干涸;

祂使一切河流枯竭。

巴珊迦密的草木凋零,

黎巴嫩的鲜花衰残。

5在祂面前,群山震动,丘陵消融。

在祂面前,大地隆起,

世界和世上的一切都战栗。

6祂发怒,谁能站立?

祂发烈怒,谁能承受?

祂的愤怒如火焰喷涌而出,

磐石在祂面前崩裂。

7耶和华是良善的,

是人患难时的避难所;

祂看顾那些信靠祂的人。

8祂必用滔滔洪水灭绝祂的敌人,

把他们驱逐到黑暗中。

9尼尼微人啊,

你们为何图谋抵挡耶和华?

祂要彻底毁灭你们,

无需击打两次。

10你们像纠结的荆棘,

又像酩酊大醉的人,

要如干秸被火烧尽。

11你们当中有一个人,

一个邪恶的阴谋者,

图谋抵挡耶和华。

12耶和华说:

“尽管尼尼微势力强大、人口众多,

但必被铲除,化为乌有。

我的子民啊,我使你们受了苦,

但必不再使你们受苦。

13现在我要打碎他们套在你们颈项上的轭,

松开你们身上的锁链。”

14尼尼微啊,

耶和华已发出有关你的命令:

“你的名不会传于后世。

我要摧毁你神庙中雕刻和铸造的偶像。

我要为你掘好坟墓,

因为你毫无用处。”

15看啊,

传喜讯、报平安的人穿山越岭而来。

犹大啊,

庆祝你的节期,

还你许的愿吧!

邪恶之人将不再侵扰你,

他们都将被彻底毁灭。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Nahumu 1:1-15

11:1 Isa 13:1; 19:1; Yer 23:33-34; 50:18; Mwa 10:11; Nah 2:8; 3:7Neno alilosema Mungu kuhusu Ninawi. Kitabu cha maono cha Nahumu, Mwelkoshi.

Hasira Ya Mungu Dhidi Ya Ninawi

21:2 Kut 20:5; Mwa 4:24; Kum 32:41; 7:10; Za 94:1Bwana ni mwenye wivu na Mungu mlipiza kisasi;

Bwana hulipiza kisasi na amejaa ghadhabu.

Bwana hulipiza kisasi juu ya watesi wake,

naye anadumisha ghadhabu yake dhidi ya adui zake.

31:3 Neh 9:17; Kut 34:7; 19:16; Za 103:8; Mik 7:18; 2Sam 22:10; Za 50:3; 104:3Bwana si mwepesi wa hasira naye ni mwenye nguvu,

Bwana hataacha kuadhibu wenye hatia.

Njia yake ipo katika kisulisuli na tufani,

na mawingu ni vumbi la miguu yake.

41:4 2Sam 22:16; Kut 14:22; Isa 33:9; Yos 3:15, 16Anakemea bahari na kuikausha,

anafanya mito yote kukauka.

Bashani na Karmeli zinanyauka

na maua ya Lebanoni hukauka.

51:5 Kut 19:18; Ay 9:6; 2Sam 22:8; Yoe 2:10; Eze 38:20; Mik 1:4Milima hutikisika mbele yake

na vilima huyeyuka.

Nchi hutetemeka mbele yake,

dunia na wote waishio ndani yake.

61:6 Za 130:3; Eze 22:14; Isa 5:24-25; 42:25; Yer 10:10; 1Fal 19:11Ni nani awezaye kuzuia hasira yake yenye uchungu?

Nani awezaye kuvumilia hasira yake kali?

Ghadhabu yake imemiminwa kama moto,

na miamba inapasuka mbele zake.

71:7 Yer 33:11; 17:17; Za 22:9; 1:6; 2Tim 2:19Bwana ni Mwema,

kimbilio wakati wa taabu.

Huwatunza wale wanaomtegemea,

81:8 Isa 8:7; Amo 8:8; Dan 9:26lakini kwa mafuriko makubwa,

ataangamiza Ninawi;

atafuatilia adui zake hadi gizani.

91:9 Hos 7:15Shauri baya lolote wapangalo dhidi ya Bwana

yeye atalikomesha;

taabu haitatokea mara ya pili.

101:10 2Sam 23:6; Isa 49:26; 5:24; Mal 4:1Watasongwa katikati ya miiba

na kulewa kwa mvinyo wao.

Watateketezwa kama mabua makavu.

11Ee Ninawi, kutoka kwako amejitokeza mmoja,

ambaye anapanga shauri baya

dhidi ya Bwana

na kushauri uovu.

121:12 Isa 10:34; 54:6-8; Mao 3:31-32Hili ndilo asemalo Bwana:

“Ingawa wana muungano nao ni wengi sana,

watakatiliwa mbali na kuangamia.

Ingawa nimekutesa wewe, ee Yuda,

sitakutesa tena.

131:13 Isa 9:4; Ay 12:18; Za 107:14Sasa nitavunja nira zao kutoka shingo yako,

nami nitazivunjilia mbali pingu zako.”

141:14 Isa 14:22; Mik 5:13; Yer 28:8; Eze 32:22-23Hii ndiyo amri Bwana aliyoitoa kukuhusu wewe, Ninawi:

“Hutakuwa na wazao

watakaoendeleza jina lako.

Nitaharibu sanamu za kuchonga na sanamu za kuyeyusha

ambazo zipo katika hekalu la miungu yenu.

Nitaandaa kaburi lako,

kwa maana wewe ni mwovu kabisa.”

151:15 Isa 40:9; Rum 10:15; Isa 52:7; Mdo 10:36; Law 23:2-4Tazama, huko juu milimani,

miguu ya huyo mmoja aletaye habari njema,

ambaye anatangaza amani!

Ee Yuda, sherehekea sikukuu zako,

nawe utimize nadhiri zako.

Waovu hawatakuvamia tena;

wataangamizwa kabisa.