路加福音 10 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

路加福音 10:1-42

差遣门徒

1事后,主拣选了七十个门徒10:1 七十个门徒”有古卷为“七十二个门徒”。,差遣他们两个两个地出去,先到祂将要去的城镇村庄, 2并对他们说:“要收割的庄稼很多,工人却很少,因此你们要祈求庄稼的主人派更多的工人去收割祂的庄稼。

3“你们去吧!我差你们出去,就像把羊羔送入狼群。 4钱袋、背包和鞋都不要带,在路上也不要与人寒暄。 5无论到哪一户人家,要先说,‘愿祝福临到这家!’ 6如果那里有配得祝福的人,祝福自然会临到那人,否则祝福仍归给你们。 7不要搬来搬去,要固定住在一家,接受那家的款待,因为工人理应得到工钱。

8“你们无论到哪一个城镇,如果人们接待你们,就吃他们摆上的饮食。 9要医治那城里的病人,告诉他们,‘上帝的国临近你们了。’ 10但如果哪一个城镇的人不欢迎你们,你们就到街上宣告, 11‘就连你们城里的尘土粘在我们脚上,我们都要跺掉,但是要知道,上帝的国临近了。’ 12我告诉你们,在审判之日,那城所受的刑罚将比所多玛所受的还重!

13哥拉汛啊,你大祸临头了!伯赛大啊,你大祸临头了!我在你们当中所行的神迹,如果行在泰尔西顿,那里的人早就身披麻衣,头蒙灰尘,坐在地上悔改了。 14在审判之日,你们将比泰尔西顿受更重的刑罚!

15迦百农啊,你将被提升到天上吗?不!你将被打落到阴间。”

16耶稣继续对门徒说:“谁听从你们,就是听从我;谁拒绝你们,就是拒绝我;拒绝我的,就是拒绝差我来的那位。”

17七十个门徒兴高采烈地回来说:“主啊,我们奉你的名行事,甚至降服了鬼魔。”

18耶稣回答说:“我看见撒旦像闪电一样从天上坠下。 19我已经给你们权柄,使你们能践踏蛇和蝎子,胜过仇敌的权势,没有什么能伤害你们。 20然而,不要为了邪灵向你们降服而高兴,要因你们的名字记录在天上而高兴。”

21就在这时候,耶稣受圣灵感动,充满喜乐地说:“父啊,天地的主,我颂赞你!因为你把这些事向聪明、有学问的人隐藏起来,却启示给像孩童一般的人。父啊!是的,这正是你的美意。 22我父将一切交给了我。除了父,没有人认识子;除了子和受子启示的人,没有人认识父。”

23随后,耶稣转身悄悄地对门徒说:“谁看到你们今日所看到的,谁就有福了。 24我告诉你们,以前有许多先知和君王渴望看见你们所看见的,听见你们所听见的,却未能如愿。”

好撒玛利亚人的比喻

25有一次,一名律法教师站起来试探耶稣,说:“老师,我应该怎样做才能得永生呢?”

26耶稣反问他:“律法怎么说?你怎么理解?”

27律法教师答道:“‘你要全心、全情、全力、全意爱主——你的上帝’,又要‘爱邻如己’。” 28耶稣说:“你答得对,照着去做就有永生了。”

29律法教师想证明自己有理,就问:“那么,谁是我的邻居呢?”

30耶稣回答说:“有个人从耶路撒冷耶利哥,途中被劫。强盗剥了他的衣服,把他打个半死,丢在那里,然后扬长而去。

31“刚好有位祭司经过,看见那人躺在地上,连忙从旁边绕过,继续赶路。 32又有个利未人经过,也跟先前那个祭司一样从旁边绕过去了。

33“后来,有位撒玛利亚10:33 犹太人向来轻视撒玛利亚人,认为他们血统不纯正,因此互不往来。经过,看见这个人,就动了慈心, 34连忙上前用油和酒替他敷伤口,包扎妥当,然后把他扶上自己骑的牲口,带到附近的客店照料。 35次日还交给店主两个银币,说,‘请替我好好照顾这个人。如果钱不够的话,等我回来再补给你。’ 36那么,你认为这三个人中谁是被劫者的邻居呢?”

37律法教师说:“是那个同情他的人。”

耶稣说:“你去照样做吧。”

上好的福分

38耶稣和门徒去耶路撒冷的途中路过一个村庄,遇到一位名叫玛大的女子接待他们到家里作客。 39玛大的妹妹玛丽亚坐在耶稣脚前听道, 40玛大为了招待客人忙乱不已,于是上前对耶稣说:

“主啊,我妹妹让我一个人伺候大家,你都不管吗?请你叫她来帮帮我吧。”

41耶稣对她说:“玛大玛大,你为太多事情忧虑烦恼。 42其实最要紧的事只有一件,玛丽亚选择了上好的,是夺不走的。”

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Luka 10:1-42

Yesu Awatuma Wale Sabini Na Wawili

110:1 Lk 7:13; 9:1-2, 51-52; Mk 6:7; Mt 10:1Baada ya hayo, Bwana akawachagua wengine sabini na wawili, akawatuma wawili wawili katika kila mji na kila sehemu aliyokusudia kwenda baadaye. 210:2 Mt 9:37-38; Yn 4:35Akawaambia, “Mavuno ni mengi, lakini watendakazi ni wachache. Kwa hiyo mwombeni Bwana wa mavuno, ili apeleke watendakazi katika shamba lake la mavuno. 310:3 Mt 10:16Haya! nendeni. Ninawatuma kama wana-kondoo katikati ya mbwa mwitu. 410:4 Lk 9:3-5; 2Fal 4:29Msichukue mkoba, wala mfuko, wala viatu, na msimsalimu mtu yeyote njiani.

510:5 Mt 4:12“Mkiingia katika nyumba yoyote, kwanza semeni, ‘Amani iwe kwenu.’ 6Kama kuna mtu wa amani humo, basi amani yenu itakuwa juu yake. La sivyo, itawarudia. 710:7 Mt 10:10; 1Kor 9:14Kaeni katika nyumba hiyo, mkila na kunywa kile watakachowapa, kwa sababu kila mtendakazi anastahili malipo yake. Msihamehame kutoka nyumba hadi nyumba.

810:8 1Kor 10:27“Mkienda katika mji na watu wake wakawakaribisha, kuleni chochote kiwekwacho mbele yenu, 910:9 Mt 3:2; 10:7waponyeni wagonjwa waliomo na waambieni: ‘Ufalme wa Mungu umekaribia.’ 10Lakini mkiingia katika mji, nao hawakuwakaribisha, tokeni mwende katika barabara zake mkaseme: 1110:11 Mt 10:14; Mk 6:11‘Hata mavumbi ya mji wenu yaliyoshikamana na miguu yetu, tunayakungʼuta dhidi yenu. Lakini mjue kwamba Ufalme wa Mungu umekaribia.’ 1210:12 Mt 10:15; 11:24Ninawaambia, itakuwa rahisi zaidi kwa Sodoma kustahimili katika siku ile kuliko mji ule.

Onyo Kwa Miji Isiyotubu

(Mathayo 11:20-24)

1310:13 Lk 6:24-26; Ufu 11:3“Ole wako Korazini! Ole wako Bethsaida! Kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwenu ingefanyika Tiro na Sidoni, miji hiyo ingekuwa imetubu zamani, kwa kuvaa magunia na kujipaka majivu. 14Lakini itakuwa rahisi zaidi kwa Tiro na Sidoni kustahimili katika siku ya hukumu, kuliko ninyi. 1510:15 Mt 4:13; Mwa 11:4; Kum 1:28; Isa 14:13; Yer 51:53Nawe, Kapernaumu, je, utainuliwa hadi mbinguni? La hasha, utashushwa mpaka kuzimu.”

1610:16 Mt 10:40; Yn 13:20“Yeye awasikilizaye ninyi anisikiliza mimi; naye awakataaye ninyi amenikataa mimi. Lakini yeye anikataaye mimi amkataa yeye aliyenituma.”

1710:17 Mk 16:17Wale sabini na wawili wakarudi kwa furaha, na kusema, “Bwana, hata pepo wachafu wanatutii kwa jina lako.”

1810:18 Mt 4:10; Isa 14:12; Ufu 9:1Yesu akawaambia, “Nilimwona Shetani akianguka kutoka mbinguni kama umeme wa radi. 1910:19 Mk 16:18; Mdo 28:3-5Tazama nimewapa mamlaka ya kukanyaga nyoka na nge na juu ya nguvu zote za adui; wala hakuna kitu chochote kitakachowadhuru. 2010:20 Dan 12:1; Flp 4:3Basi, msifurahi kwa kuwa pepo wachafu wanawatii, bali furahini kwa kuwa majina yenu yameandikwa mbinguni.”

Yesu Anashangilia

(Mathayo 11:25-27; 13:16-17)

2110:21 1Kor 1:26-29Wakati huo Yesu akashangilia katika Roho Mtakatifu, akasema, “Nakuhimidi Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa umewaficha mambo haya wenye hekima na wenye elimu, nawe ukawafunulia watoto wadogo. Naam, Baba, kwa kuwa hivyo ndivyo ilivyokupendeza.

2210:22 Mt 28:18; Yn 1:18“Nimekabidhiwa vitu vyote na Baba yangu. Hakuna mtu amjuaye Mwana ni nani ila Baba, wala hakuna amjuaye Baba ni nani ila Mwana na yeyote ambaye Mwana anapenda kumfunulia.”

2310:23 Mt 13:16, 17 Basi Yesu akawageukia wanafunzi wake akanena nao faraghani, akawaambia, “Heri macho yanayoona yale mambo mnayoyaona. 2410:24 1Pet 1:10-12Kwa maana nawaambia, manabii wengi na wafalme walitamani kuona yale mnayoyaona lakini hawakuyaona, na walitamani kusikia yale mnayoyasikia lakini hawakuyasikia.”

Mfano Wa Msamaria Mwema

2510:25 Mt 19:16; Lk 18:18Wakati huo mtaalamu mmoja wa sheria alisimama ili kumjaribu Yesu, akamuuliza, “Mwalimu, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?”

26Yesu akamjibu, “Imeandikwaje katika Sheria? Kwani unasoma nini humo?”

2710:27 Kum 6:5; Law 19:18; Mt 5:43Akajibu, “ ‘Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote’; tena, ‘Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.’ ”

2810:28 Law 18; 5; Rum 7:10Yesu akamwambia, “Umejibu vyema. Fanya hivyo nawe utaishi.”

2910:29 Lk 16:15Lakini yule mtaalamu wa sheria, akitaka kujionyesha kuwa mwenye haki, akamuuliza Yesu, “Jirani yangu ni nani?”

30Yesu akamjibu akasema, “Mtu mmoja alikuwa akiteremka kutoka Yerusalemu kwenda Yeriko, naye akaangukia mikononi mwa wanyangʼanyi. Wakampiga, wakaondoka, wakamwacha akiwa karibu kufa. 3110:31 Law 21:1-3Kuhani mmoja alikuwa akipitia njia ile, alipomwona huyo mtu, akapita upande mwingine, akamwacha hapo barabarani. 32Vivyo hivyo, Mlawi mmoja naye alipofika mahali pale, alimwona, akapita upande mwingine, akamwacha hapo barabarani 3310:33 Mt 10:5Lakini Msamaria mmoja aliyekuwa akisafiri alipomwona, alimhurumia. 34Akaenda alipokuwa na akasafisha majeraha yake kwa divai na mafuta, kisha akayafunga. Ndipo akampandisha kwenye punda wake, akampeleka mpaka kwenye nyumba ya wageni na kumtunza. 35Kesho yake, yule Msamaria akachukua dinari mbili10:35 Dinari mbili ni sawa na mshahara wa kibarua wa siku mbili. akampa yule mwenye nyumba ya wageni na kusema, ‘Mtunze, nami nirudipo nitakulipa gharama yoyote ya ziada uliyotumia kwa ajili yake.’

36“Ni yupi basi miongoni mwa hawa watatu wewe unadhani ni jirani yake yule mtu aliyeangukia mikononi mwa wanyangʼanyi?”

37Yule mtaalamu wa sheria akajibu, “Ni yule aliyemhurumia.”

Ndipo Yesu akamwambia, “Nenda, ukafanye vivyo hivyo.”

Yesu Awatembelea Martha Na Maria

3810:38 Yn 11:1; 12:2-3Ikawa Yesu na wanafunzi wake walipokuwa wakienda Yerusalemu, akaingia kwenye kijiji kimoja ambapo mwanamke mmoja aliyeitwa Martha alimkaribisha nyumbani kwake. 3910:39 Lk 8:35Martha alikuwa na mdogo wake aliyeitwa Maria, ambaye aliketi chini miguuni mwa Bwana akisikiliza yale aliyokuwa akisema. 4010:40 Mk 4:38Lakini Martha alikuwa akihangaika na maandalizi yote yaliyokuwa yafanyike. Martha akaja kwa Yesu na kumuuliza, “Bwana, hujali kwamba ndugu yangu ameniachia kazi zote mwenyewe? Basi mwambie anisaidie.”

4110:41 Mt 6:25-34; Lk 12:11, 22Lakini Bwana akamjibu, “Martha, Martha, mbona unasumbuka na kuhangaika na mengi? 4210:42 Za 27:4Lakini kunahitajika kitu kimoja tu. Maria amechagua kile kilicho bora, wala hakuna mtu atakayemwondolea.”