耶利米书 38 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

耶利米书 38:1-28

耶利米陷在枯井里

1玛坦的儿子示法提雅巴施户珥的儿子基大利示利米雅的儿子犹甲玛基雅的儿子巴施户珥听见了耶利米对众人说: 2“耶和华说,‘凡留在这城的,必死于刀剑、饥荒和瘟疫;凡出去向迦勒底人投降的,必保全性命。’ 3耶和华说,‘这城必落在巴比伦王的军队手中,他们必攻占这城。’” 4这几位官长就对西底迦王说:“求你处死这人!因为他的话令这城的军民士气低落。这人不为人民着想,反要害他们。” 5西底迦王说:“你们可以随意处置他,我不会阻止你们。” 6于是,他们拿住耶利米,用绳子把他缒到王子玛基雅的蓄水池里。那池子在护卫兵的院子里,池中没有水,只有淤泥。耶利米就陷在淤泥中。

7那时,王正坐在便雅悯门口。宫廷侍臣古实以伯·米勒听说他们把耶利米囚在蓄水池里, 8便从王宫跑去对王说: 9“我主我王啊!这些人对耶利米先知太狠毒了。他们把他丢在蓄水池里,他必饿死在那里,因为城中绝粮了。” 10于是,王吩咐古实以伯·米勒率领三十人,在耶利米先知未死之前把他从池中救出来。 11以伯·米勒带着他的手下进入王宫,从库房下面的房间拿了些碎布和破衣,用绳索缒到池底给耶利米12让他把这些碎布和破衣垫在腋下,以免被绳索勒伤。耶利米就照做了。 13他们便把耶利米从池中拉上来拘留在护卫兵的院子里。

西底迦王密会耶利米

14西底迦王派人把耶利米先知带到耶和华殿的第三道门那里与他会面。他对耶利米说:“我要问你一件事,你不可隐瞒。” 15耶利米说:“我若从实禀告,你一定会杀我。我就是给你建议,你也不会听。” 16于是,他私下向耶利米发誓说:“我凭那赐给我们生命的永活的耶和华起誓,我决不杀你,也不把你交在想杀你的人手中。”

17耶利米说:“以色列的上帝——万军之上帝耶和华说,‘如果你出去向巴比伦王的将领投降,就可以保住你和你全家的性命,这城也不会被烧毁。 18但如果你不出去向巴比伦王的将领投降,这城必落在迦勒底人手里,被付之一炬,你也逃不掉。’” 19西底迦王说:“我害怕那些已经向迦勒底人投降的犹大人,恐怕迦勒底人会把我交给他们,任由他们羞辱。” 20耶利米说:“不会的。只要你听从耶和华吩咐我对你说的话,你就可以平安无事,保全性命。 21耶和华已指示我,如果你不肯投降, 22所有留在犹大王宫的妇女都必被巴比伦王的将领俘虏,她们会讽刺你说,‘你被好友欺骗、误导,当你陷入泥潭时,他们就离弃了你。’

23“你的嫔妃和儿女必被交给迦勒底人,你也逃不掉,必被巴比伦王所擒。这城也要被付之一炬。”

24西底迦说:“不可让人知道我们的谈话,否则你会丧命。 25如果有官长知道我曾与你会面,前来以死亡相威胁,逼你说出我们谈话的内容。 26你可以告诉他们,你是在求我不要把你押回约拿单的房子,以免死在那里。” 27果然,官长前来查问耶利米,他就照王的吩咐回复他们,他们便不再追问,因为他跟王的谈话无人知道。 28耶利米被囚在护卫兵的院子里,一直到耶路撒冷沦陷。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Yeremia 38:1-28

Yeremia Atupwa Kwenye Kisima

138:1 Yer 37:3; Mdo 4:2; 1Nya 9:12Shefatia mwana wa Matani, na Gedalia mwana wa Pashuri, na Yehukali mwana wa Shelemia, na Pashuri mwana wa Malkiya wakasikia kile Yeremia alichokuwa akiwaambia watu wote wakati aliposema, 238:2 Yer 34:17; 11:21; 45:5; 21:9; 38:19; Mt 24:7-8“Hili ndilo asemalo Bwana: ‘Yeyote akaaye ndani ya mji huu atakufa kwa upanga, njaa au tauni, lakini yeyote atakayejisalimisha kwa Wakaldayo ataishi. Atakayeyatoa maisha yake kama nyara, ataishi.’ 338:3 Yer 21:10; 32:3Tena hili ndilo asemalo Bwana: ‘Mji huu kwa hakika utatiwa mikononi mwa jeshi la mfalme wa Babeli, ambaye atauteka.’ ”

438:4 Yer 36:12; 11:21; 26:11; Za 37:12-40; Amo 7:10; 1Sam 17:32Ndipo maafisa wakamwambia mfalme, “Mtu huyu imempasa kuuawa. Anawakatisha tamaa askari waliobaki katika mji huu, vivyo hivyo na watu wote pia, kwa ajili ya mambo anayowaambia. Mtu huyu hawatakii mema watu hawa, bali maangamizi yao.”

538:5 Yer 26:14; 1Sam 15:24Mfalme Sedekia akajibu, “Yeye yuko mikononi mwenu! Mfalme hawezi kufanya lolote kuwapinga ninyi.”

638:6 Yer 37:21; Mao 3:53; Mk 9:42; Yos 2:15; Mwa 37:24; Ay 30:9Basi wakamchukua Yeremia na kumtia kwenye kisima cha Malkiya, mwana wa mfalme, kilichokuwa katika ua wa walinzi. Wakamteremsha Yeremia kwa kamba ndani ya kisima. Hakikuwa na maji ndani yake, ila tope tu, naye Yeremia akazama ndani ya matope.

738:7 Yer 39:16; Isa 56:3-5; Mdo 8:27; Ay 29:7Lakini Ebed-Meleki Mkushi, aliyekuwa afisa katika jumba la kifalme, akasikia kuwa walikuwa wamemtia Yeremia ndani ya kisima. Wakati mfalme alipokuwa ameketi katika Lango la Benyamini, 8Ebed-Meleki akatoka nje ya jumba la kifalme na kumwambia, 938:9 Yer 37:21; Mwa 37:20“Mfalme bwana wangu, watu hawa wamefanya uovu kwa yote waliomtendea nabii Yeremia. Wamemtupa ndani ya kisima, mahali ambapo atakufa kwa njaa wakati ambapo hakuna chakula popote katika mji.”

10Basi mfalme akamwamuru Ebed-Meleki Mkushi, akisema, “Chukua watu thelathini kutoka hapa pamoja nawe, mkamtoe nabii Yeremia huko kwenye kisima kabla hajafa.”

11Basi Ebed-Meleki akawachukua watu pamoja naye, wakaenda mpaka kwenye chumba kilichoko chini ya hazina ndani ya jumba la kifalme. Akachukua matambaa makuukuu pamoja na nguo zilizochakaa kutoka huko, na kumshushia Yeremia kwa kamba ndani ya kisima. 12Ebed-Meleki Mkushi akamwambia Yeremia, “Weka haya matambaa makuukuu na hizo nguo zilizochakaa makwapani ili kuzuia kamba.” Yeremia akafanya hivyo, 1338:13 Yer 37:21; 2Kor 6:4-5nao wakamvuta juu kwa kamba na kumtoa katika kisima. Yeremia akakaa katika ua wa walinzi.

Sedekia Amhoji Yeremia Tena

1438:14 1Sam 3:17; Za 82:4; Yer 37:3Ndipo Mfalme Sedekia akatuma watu wamwitie nabii Yeremia wamlete kwake kwenye ingilio la tatu la Hekalu la Bwana. Mfalme akamwambia Yeremia, “Ninataka kukuuliza jambo fulani, usinifiche kitu chochote.”

15Yeremia akamwambia Sedekia, “Nikikupa jibu, je, hutaniua? Hata kama nikikupa shauri, wewe hutanisikiliza.”

1638:16 Yer 37:17; Hes 16:22; Isa 42:5; 57:16; Ebr 12:9Lakini Mfalme Sedekia akamwapia Yeremia kiapo hiki kwa siri, akisema, “Hakika kama aishivyo Bwana, ambaye ametupa pumzi, sitakuua wala sitakutia mikononi mwa wale wanaotafuta uhai wako.”

1738:17 2Fal 24:12; Yer 21:8-10; 27:8Kisha Yeremia akamwambia Sedekia, “Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli: ‘Ikiwa utajisalimisha kwa maafisa wa mfalme wa Babeli, maisha yako yatasalimika, na mji huu hautateketezwa kwa moto. Pia wewe na jamaa yako mtaishi. 1838:18 Yer 34:3; 37:8; 24:8; 32:4Lakini ikiwa hutajisalimisha kwa maafisa wa mfalme wa Babeli, mji huu utatiwa mikononi mwa Wakaldayo na watauteketeza kwa moto, nawe mwenyewe hutaweza kujiokoa mikononi mwao.’ ”

1938:19 Isa 51:12; Yn 12:42; Yer 52:15; 1Sam 31:4; Yer 39:9Mfalme Sedekia akamwambia Yeremia, “Ninawaogopa Wayahudi ambao wamekimbilia kwa Wakaldayo, kwa kuwa Wakaldayo wanaweza kunitia mikononi mwao, nao wakanitenda vibaya.”

2038:20 Yer 11:4; Isa 55:3; 2Kor 5:20; Kum 5:33; Yer 40:9Yeremia akajibu, “Hawatakutia mikononi mwao. Mtii Bwana kwa kufanya kile ninachokuambia. Kisha utafanikiwa na maisha yako yatakuwa salama. 21Lakini ukikataa kujisalimisha, hili ndilo Bwana alilonifunulia: 2238:22 Yer 6:12; Ay 19:14; Yer 13:21; Ay 30:19; Za 69:14Wanawake wote walioachwa katika jumba la kifalme la mfalme wa Yuda wataletwa mbele ya maafisa wa mfalme wa Babeli. Wanawake hao watakuambia:

“ ‘Walikupotosha na kukushinda,

wale rafiki zako uliowaamini.

Miguu yako imezama matopeni;

rafiki zako wamekuacha.’

2338:23 2Fal 25:6; Yer 24:8; 41:10; 32:4; Eze 17:15; Yer 21:10; 37:8“Wake zako wote na watoto wataletwa na kutiwa mikononi mwa Wakaldayo. Wewe mwenyewe hutaweza kujiokoa mikononi mwao. Lakini utatekwa na mfalme wa Babeli, na mji huu utateketezwa kwa moto.”

2438:24 Yer 37:17-21Kisha Sedekia akamwambia Yeremia, “Usiruhusu mtu yeyote ajue kuhusu haya mazungumzo, la sivyo utakufa. 25Maafisa wakisikia kwamba nimezungumza nawe, nao wakakujia na kusema, ‘Tuambie kile ulichozungumza na mfalme na kile mfalme alichokuambia, usitufiche au sivyo tutakuua,’ 2638:26 Yer 37:15, 20; 39:14; 1Sam 16:2basi waambie, ‘Nilikuwa ninamsihi mfalme asinirudishe kwenye nyumba ya Yonathani nisije nikafia humo.’ ”

27Maafisa wote wakamjia Yeremia na kumuuliza, naye Yeremia akawaambia kila kitu mfalme alichomwagiza kusema. Kisha hawakusema lolote zaidi na Yeremia kwa sababu hakuna yeyote aliyesikia mazungumzo yake na mfalme.

28Naye Yeremia akabaki katika ua wa walinzi hadi siku Yerusalemu ilipotekwa.