约书亚记 4 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

约书亚记 4:1-24

堆石为证

1民众都过河之后,耶和华对约书亚说: 2“你去从民众中选出十二个人,每支派选一人, 3吩咐他们从约旦河床祭司站立的地方取十二块石头,放在你们今天晚上住宿的地方。” 4约书亚便召来他从以色列人中选的十二个人,对他们说: 5“你们到约旦河床你们的上帝耶和华的约柜前面,每人扛一块石头回来,每个支派一块,一共十二块。 6这些石头要在你们中间作记号。以后,倘若你们的子孙问你们,‘这些石头是什么意思?’ 7你们就告诉他们,‘约旦河水在耶和华的约柜前曾经被截断,当约柜过河的时候,河水被截断了。这些石头要在以色列人当中作为永久的纪念。’”

8以色列人就照约书亚的吩咐,也就是照耶和华对约书亚的吩咐,按以色列人支派的数目,从约旦河中取了十二块石头,搬来放在住宿的地方。 9约书亚又在约旦河床抬约柜的祭司站立的地方立了十二块石头。石头至今还在那里。 10抬约柜的祭司站在约旦河中间,一直站到耶和华吩咐约书亚交待民众做的每一件事都完成了,正如摩西约书亚的吩咐。民众迅速过了河。 11所有人都过河以后,祭司才抬着耶和华的约柜在民众注视之下过了河。 12吕便支派、迦得支派和玛拿西半个支派的人照摩西从前的嘱咐,带着兵器走在以色列人的前面。 13大约有四万全副武装的以色列人在耶和华面前过了河,前往耶利哥平原,准备作战。 14那一天,耶和华使约书亚以色列众人面前受尊重,他像摩西一样终生受民众敬畏。

15耶和华对约书亚说: 16“你去吩咐抬约柜的祭司从约旦河里上来。” 17约书亚便吩咐他们上来。 18抬耶和华约柜的祭司从河床上来,脚刚一踏上岸,约旦河的水立刻恢复了原状,像以往一样涨过两岸。

19那天是一月十日。以色列人从约旦河上来之后,就在耶利哥东边的吉甲扎营。 20约书亚把从约旦河取来的十二块石头立在吉甲21并对以色列人说:“以后,你们的子孙问你们这堆石头是什么意思, 22你们就告诉他们,‘这是代表以色列人曾在干地上走过约旦河。’ 23因为你们的上帝耶和华为了让你们过河而使约旦河成为干地,就像祂从前为了让我们过红海而使海成为干地一样。 24这是要让天下万民都知道耶和华有无比的能力,要让你们永远敬畏你们的上帝耶和华。”

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Yoshua 4:1-24

Ukumbusho Wa Kuvuka Mto Yordani

14:1 Kum 27:2; Yos 2:17Wakati taifa lote lilipokwisha kuvuka Mto Yordani, Bwana akamwambia Yoshua, 24:2 Yos 3:17; Hes 13:1; 34:18; Yos 1:4-15; 1Fal 18:31“Chagua watu kumi na wawili miongoni mwa watu, kila kabila mtu mmoja, 3nawe uwaambie wachukue mawe kumi na mawili katikati ya Mto Yordani, palepale makuhani waliposimama, wayachukue na kuyaweka mahali mtakapokaa usiku huu wa leo.”

44:4 Yos 3:12Basi Yoshua akawaita watu kumi na wawili ambao alikuwa amewachagua kutoka miongoni mwa Waisraeli, mtu mmoja kutoka kila kabila, 54:5 Yos 3:17naye akawaambia, “Mtangulie mbele ya Sanduku la Bwana Mungu wenu, mwende katikati ya Mto Yordani. Kila mmoja wenu atainua jiwe begani mwake, kufuatana na hesabu ya makabila ya Waisraeli, 64:6 Yos 2:12; Kut 10:2; 12:26; 13:14; Kum 6:20; Za 78:3-6; Isa 38:16kuwa kama ishara katikati yenu. Siku zijazo, wakati watoto wenu watakapowauliza, ‘Ni nini maana ya mawe haya?’ 74:7 Yos 3:13; Kut 28:12; 12:14waambieni kwamba maji ya Mto Yordani yaliyokuwa yakitiririka yalitindika mbele ya Sanduku la Agano la Bwana. Wakati lilipovuka Yordani, maji ya Yordani yalitindika. Mawe haya yatakuwa kumbukumbu kwa watu wa Israeli milele.”

84:8 Kut 28:21; Yos 3:17Hivyo Waisraeli wakafanya kama Yoshua alivyowaagiza. Wakachukua mawe kumi na mawili kutoka katikati ya Mto Yordani, kulingana na hesabu ya kabila za Waisraeli kama Bwana alivyomwambia Yoshua, nao wakayabeba hadi kambini mwao, mahali walipoyatua chini. 94:9 Mwa 28:18; Yos 24:26; 1Sam 7:12; Mwa 35:20Yoshua akayasimamisha yale mawe kumi na mawili ambayo yalikuwa katikati ya Mto Yordani, mahali pale ambapo miguu ya makuhani waliobeba Sanduku la Agano iliposimama. Nayo yako huko mpaka leo.

10Makuhani waliobeba lile Sanduku walibakia wakiwa wamesimama katikati ya Mto Yordani mpaka kila kitu Bwana alichomwamuru Yoshua kilipokuwa kimefanywa na watu, sawasawa na vile Mose alivyokuwa amemwamuru Yoshua. Watu wakafanya haraka kuvuka, 11na mara tu watu wote walipokwisha kuvuka, Sanduku la Bwana na makuhani wakavuka watu wakiwa wanatazama. 124:12 Mwa 29:32; 30:11; 41:51; Hes 32:27-29Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase wakavuka mbele ya Waisraeli, wakiwa wamevaa silaha, kama Mose alivyowaamuru. 134:13 Kut 13:18; Hes 32:17Kiasi cha watu 40,000 waliojiandaa kwa vita walivuka mbele za Bwana hadi nchi tambarare za Yeriko kwa ajili ya vita.

144:14 Yos 3:7; 1Sam 2:30; 2Nya 32:23; 1Nya 29:12Siku ile Bwana akamtukuza Yoshua mbele ya Israeli yote, nao wakamheshimu siku zote za maisha yake, kama vile walivyomheshimu Mose.

15Basi Bwana akamwambia Yoshua, 164:16 Kut 25:22; Ufu 11:19; Yos 3:15“Waamuru hao makuhani wanaolibeba Sanduku la Ushuhuda, wapande kutoka ndani ya Mto Yordani.”

17Kwa hiyo Yoshua akawaamuru hao makuhani akisema, “Pandeni kutoka ndani ya Mto Yordani.”

184:18 Kut 14:27; Yos 3:15Nao makuhani wakapanda kutoka ndani ya Mto Yordani wakilibeba hilo Sanduku la Agano la Bwana. Mara tu walipoiweka miguu yao penye kingo, nje ya mto, maji ya Yordani yakarudi kufurika kama ilivyokuwa kabla.

194:19 Kum 11:30; Yos 5:9; 15:17; 1Sam 11:14-15; Amo 4:4; 5:5; Mik 6:5Siku ya kumi ya mwezi wa kwanza watu walipanda kutoka Yordani na kupiga kambi huko Gilgali, kwenye mpaka wa mashariki ya Yeriko. 20Naye Yoshua akayasimamisha huko Gilgali yale mawe kumi na mawili ambayo walikuwa wameyachukua katikati ya Mto Yordani. 21Akawaambia Waisraeli, “Wazao wenu watakapowauliza baba zao siku zijazo wakisema, ‘Mawe haya maana yake ni nini?’ 224:22 Kut 14:22; Yos 3:17Basi waambieni, ‘Israeli ilivukia mahali pakavu katika Mto Yordani.’ 234:23 Kut 14:19-22; Neh 9:11; Za 77:16-19; Isa 43:16; 63:12Kwa maana Bwana Mungu wenu alikausha maji ya Yordani mbele yenu, hadi mlipomaliza kuvuka. Bwana Mungu wenu alifanya haya kwa Mto Yordani sawasawa na kile alichoifanyia Bahari ya Shamu wakati alipoikausha mbele yetu hadi tulipomaliza kuvuka. 244:24 1Fal 8:60; 18:36; 2Fal 5:15; Za 67:2; 83:18; 106:8; Isa 37:20; 52:10; Kut 15:16; 1Nya 29:12; Za 44:3; 89:13; 98:1; 118:15-16; Kut 14:31Alifanya hivi ili kwamba mataifa yote ya dunia yapate kujua kuwa mkono wa Bwana ni wenye nguvu, na ili kwamba kila wakati mpate kumcha Bwana Mungu wenu.”