箴言 30 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

箴言 30:1-33

亚古珥的箴言

1以下是雅基的儿子亚古珥的箴言。

这人说:上帝啊,我很疲倦;

上帝啊,我很疲倦,精疲力尽。30:1 希伯来文或译“这人对以铁说,对以铁和乌甲说:”

2我比众人都愚蠢,

不具备人的悟性。

3我从未学到智慧,

也不认识至圣者。

4谁升上高天又降下来?

谁将风聚在掌中?

谁将众水裹在衣服里?

谁定了地的边界?

祂叫什么名字?

祂儿子叫什么名字?

你知道吗?

5上帝的话句句千真万确,

祂作投靠祂之人的盾牌。

6你不可对祂的话有所添加,

免得祂责备你,

揭穿你的虚谎。

7上帝啊,我向你求两件事,

求你在我未死以前赐给我。

8求你使虚伪和谎言远离我,

求你让我不贫穷也不富足,

赐给我需用的饮食,

9免得我因为饱足就不认你,

说:“耶和华是谁呢?”

又恐怕我因穷困而偷窃,

以致辱没我上帝的名。

10别向主人毁谤他的仆人,

免得你受咒诅、担当罪责。

11有一种30:11 ”希伯来文是“世代”,11-14节也相同。人咒诅父亲,

不为母亲祝福。

12有一种人自以为纯洁,

却没有洗掉自己的污秽。

13有一种人趾高气扬,

目空一切。

14有一种人牙如剑,

齿如刀,

要吞吃世间的困苦人和贫穷人。

15水蛭有两个女儿,

她们不停地叫:“给我!给我!”

三样东西从不知足,

永不言“够”的共有四样:

16阴间、不孕的妇人、

干旱的土地和火焰。

17嘲笑父亲、藐视母亲教诲的,

眼睛必被谷中的乌鸦啄出,

被秃鹰吃掉。

18我测不透的妙事有三样,

我不明白的事共有四样:

19鹰在空中飞翔之道,

蛇在石上爬行之道,

船在海中航行之道,

男女相爱之道。

20淫妇的道是这样:

她吃完就擦擦嘴,

说,“我没有做坏事。”

21使大地震动的事有三样,

大地无法承受的事共有四样:

22奴仆做王,

愚人吃饱,

23丑恶女子出嫁,

婢女取代主母。

24地上有四种动物,

身体虽小却极其聪明:

25蚂蚁力量虽小,

却在夏天储备粮食;

26石獾虽不强壮,

却在岩石中筑巢穴;

27蝗虫虽无君王,

却整齐地列队前进;

28壁虎虽易捕捉,

却居住在王宫大内。

29步履威武的有三样,

走路雄壮的共有四样:

30威震百兽、从不畏缩的狮子,

31昂首阔步的雄鸡,

公山羊和率领军队的君王。

32你若行事愚昧、

妄自尊大或图谋不轨,

就当用手掩口。

33激起愤怒会引起争端,

正如搅牛奶会搅出奶油,

拧鼻子会拧出血。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Mithali 30:1-33

Misemo Ya Aguri

130:1 Mit 22:17Misemo ya Aguri mwana wa Yake, usia:

Huyu mtu alimwambia Ithieli,

naam, kwa Ithieli na kwa Ukali:

230:2 Za 73:22“Mimi ni mjinga kuliko wanadamu wote;

sina ufahamu wa kibinadamu.

330:3 Mit 9:10Sijajifunza hekima,

wala sina maarifa ya kumjua yeye Aliye Mtakatifu.

430:4 Kum 30:12; Ufu 19:12; Yn 3:13; Ay 26:8; Efe 4:7-10Ni nani ameshapanda mbinguni na kushuka?

Ni nani ameshakusanya upepo

kwenye vitanga vya mikono yake?

Ni nani ameshafungia maji kwenye nguo yake?

Ni nani ameimarisha miisho yote ya dunia?

Jina lake ni nani, na mwanawe anaitwa nani?

Niambie kama unajua!

530:5 Za 18:30; 12:6; 84:11“Kila neno la Mungu ni kamilifu;

yeye ni ngao kwa wale wanaomkimbilia.

630:6 Kum 12:32; Ufu 22:18Usiongeze kwenye maneno yake,

ama atakukemea na kukuthibitisha kuwa mwongo.

7“Ninakuomba vitu viwili, Ee Bwana;

usininyime kabla sijafa:

830:8 Mt 6:18Uutenge mbali nami udanganyifu na uongo;

usinipe umaskini wala utajiri,

bali unipe chakula cha kunitosha kila siku.

930:9 Neh 9:25; Kum 6:12; 8:12; Yos 24:27; Hos 13:6Nisije nikawa na vingi vya kuzidi nikakukana

na kusema, ‘Bwana ni nani?’

Au nisije nikawa maskini nikaiba,

nami nikaliaibisha jina la Mungu wangu.

10“Usimchongee mtumishi kwa bwana wake,

asije akakulaani, ukapatilizwa kwalo.

1130:11 Mit 20:20“Wako watu wale ambao huwalaani baba zao

na wala hawawabariki mama zao;

1230:12 Lk 18:11; Mit 16:2; Yer 2:23-35wale ambao ni safi machoni pao wenyewe

kumbe hawakuoshwa uchafu wao;

1330:13 Ay 41:34wale ambao daima macho yao ni ya kiburi,

ambao kutazama kwao ni kwa dharau;

1430:14 Ay 24:9; 29:17; Za 14:4; 57:4; Amo 8:4; Mik 2:2wale ambao meno yao ni panga

na ambao mataya yao yamewekwa visu

kuwaangamiza maskini katika nchi,

na wahitaji kutoka miongoni mwa wanadamu.

1530:15 Mit 27:20“Mruba anao binti wawili waliao,

‘Nipe! Nipe!’

“Kuna vitu vitatu visivyotosheka kamwe,

naam, viko vinne visivyosema, ‘Yatosha!’:

1630:16 Isa 5:14; Hab 2:5Ni kaburi, tumbo lisilozaa,

nchi isiyoshiba maji kamwe,

na moto, usiosema kamwe, ‘Yatosha!’

1730:17 Kum 21:18-21; Mit 20:20; Law 20:9; Ay 15:23“Jicho lile limdhihakilo baba,

lile linalodharau kumtii mama,

litangʼolewa na kunguru wa bondeni,

litaliwa na tai.

18“Kuna vitu vitatu vinavyonishangaza sana,

naam, vinne nisivyovielewa:

19Ni mwendo wa tai katika anga,

mwendo wa nyoka juu ya mwamba,

mwendo wa meli katika maji makuu ya bahari,

nao mwendo wa mtu pamoja na msichana.

2030:20 Mit 5:6“Huu ndio mwendo wa mwanamke mzinzi,

hula akapangusa kinywa chake na kusema,

‘Sikufanya chochote kibaya.’

21“Kwa mambo matatu nchi hutetemeka,

naam, kwa mambo manne haiwezi kuvumilia:

2230:22 Mit 19:10; 29:2; Mhu 10:7Mtumwa awapo mfalme,

mpumbavu ashibapo chakula,

23mwanamke asiyependwa aolewapo,

naye mtumishi wa kike achukuapo nafasi ya bibi yake.

24“Vitu vinne duniani vilivyo vidogo,

lakini vina akili nyingi sana:

2530:25 Mit 6:6-8Mchwa ni viumbe wenye nguvu ndogo,

hata hivyo hujiwekea akiba ya chakula chao wakati wa kiangazi.

2630:26 Za 104:18Pelele ni viumbe vyenye uwezo mdogo

hata hivyo hujitengenezea nyumba zao kwenye miamba.

2730:27 Kut 10:4Nzige hawana mfalme,

hata hivyo huenda pamoja vikosi vikosi.

28Mjusi anaweza kushikwa kwa mkono,

hata hivyo huonekana katika majumba ya kifalme.

29“Viko vitu vitatu ambavyo vinapendeza katika mwendo wao,

naam, vinne ambavyo hutembea kwa mwendo wa madaha:

30simba, mwenye nguvu miongoni mwa wanyama,

asiyerudi nyuma kwa chochote;

31jogoo atembeaye kwa maringo, pia beberu,

naye mfalme pamoja na jeshi lake lililomzunguka.

3230:32 Ay 21:5; 29:9; Mhu 8:3; Mik 7:16“Ikiwa umefanya upumbavu na ukajitukuza mwenyewe,

au kama umepanga mabaya,

basi funika mdomo wako na mkono wako.

33Kwa maana kama vile kusukasuka maziwa hutoa siagi,

na pia kule kufinya pua hutoa damu,

kadhalika kuchochea hasira hutokeza ugomvi.”