申命记 6 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

申命记 6:1-25

最大的诫命

1“你们的上帝耶和华吩咐我教导你们以下的诫命、律例和典章,以便你们在将要占领的土地上遵行。 2这样,你们就会得享长寿,你们及子孙就会终生敬畏你们的上帝耶和华,遵守祂借我吩咐你们的一切律例和诫命。 3以色列人啊,你们要留心听,谨慎遵行,以便你们在那奶蜜之乡可以凡事顺利、子孙众多,正如你们祖先的上帝耶和华给你们的应许。 4听啊,以色列人,耶和华是我们的上帝,耶和华是独一的。 5你们要全心、全意、全力爱你们的上帝耶和华。 6要将我今天吩咐你们的话牢记在心, 7并教导你们的儿女,无论在家在外,或起或卧,都要讲论这些律例和诫命。 8要把它们系在手上、戴在额上作记号, 9要写在城门上和自家的门框上。

10“你们的上帝耶和华将带你们进入祂向你们祖先亚伯拉罕以撒雅各起誓要赐给你们的土地。那里的宏伟城邑不是你们建造的, 11满屋的美物不是你们积攒的,井不是你们挖掘的,葡萄园和橄榄树也不是你们栽种的。你们在那里吃饱喝足之后, 12要小心,不可忘记把你们从受奴役之地——埃及救出来的耶和华。 13要敬畏你们的上帝耶和华,事奉祂,凭祂的名起誓。 14不可随从周围各族的神明, 15免得你们的上帝耶和华向你们发怒,把你们从世上消灭;因为祂住在你们当中,祂痛恨不贞。

16“不可像在玛撒那样试探你们的上帝耶和华。 17要谨遵你们的上帝耶和华吩咐你们的诫命、法度和律例。 18你们要做耶和华视为正与善的事,以便你们可以凡事顺利,得到耶和华起誓赐给你们祖先的佳美之地, 19赶出所有敌人,正如耶和华所言。

20“将来你们的子孙会问,‘我们的上帝耶和华给你们颁布这些法度、律例和典章是什么意思?’ 21你们要告诉他们,‘我们曾在埃及做法老的奴隶,耶和华用大能的手领我们离开埃及22我们亲眼看见耶和华行伟大而可畏的神迹奇事,惩罚埃及和法老全家。 23祂带领我们离开埃及,为要把我们带进祂起誓赐给我们祖先的这片土地。 24我们的上帝耶和华吩咐我们遵守这一切律例、敬畏祂,以便我们可以常常受益,生命无忧,正如今日的情形。 25如果我们按照我们的上帝耶和华的吩咐,在祂面前谨遵这一切诫命,我们便被算为义人。’

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Kumbukumbu 6:1-25

Mpende Bwana Mungu Wako

1Haya ndiyo maagizo, amri na sheria ambazo Bwana Mungu wenu aliniagiza niwafundishe ninyi ili mpate kuyashika katika nchi ambayo ninyi mnavuka Yordani kuimiliki, 26:2 Kut 20:20; 1Sam 12:24; Kum 4:9; Mwa 26:5; Kut 20:12ili kwamba ninyi, watoto wenu na watoto wao baada yao wamche Bwana Mungu wenu siku zote kwa kushika amri na maagizo yake yote ninayowapa, ili mweze kuyafurahia maisha marefu. 36:3 Mwa 15:5; Kum 5:33; 32:13-14; Kut 3:8; 13:5; 19:5Sikia, ee Israeli, nawe uwe mwangalifu kutii ili upate kufanikiwa na kuongezeka sana katika nchi itiririkayo maziwa na asali, kama Bwana, Mungu wa baba zenu, alivyowaahidi ninyi.

46:4 Zek 14:9; Kum 4:35-39; Neh 9:6; Za 86:10; Isa 44:6; Mk 12:29; Yn 10:30; 1Kor 8:4; Efe 4:6; Yak 2:19Sikia, ee Israeli: Bwana Mungu wako, Bwana ni mmoja. 56:5 Kum 11:1, 22; Mt 22:37; Mk 12:30; Lk 10:27; 1Sam 12:24; Kum 4:29; 10:12; Yos 22:5Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote. 66:6 Kum 11:18; 30:14; 32:46; Za 26:2; 37:31; 40:8; 119:11; Mit 3:3; Isa 51:7; Yer 17:1; 31:33; Eze 40:4Amri hizi ninazokupa leo zitakuwa katika moyo wako. 76:7 Kum 4:9; 11:19; Mit 22:6; Efe 6:4Wafundishe watoto wako kwa bidii. Nena kuhusu amri hizi uketipo nyumbani na wakati utembeapo njiani, ulalapo na uamkapo. 86:8 Kut 13:9; Mt 23:5; Mit 3:3; 7:3; 6:21Zifunge kama alama juu ya mkono wako, na uzifunge juu ya paji la uso wako. 96:9 Kum 11:20; Isa 50:8; 57:8Ziandike kwenye miimo ya milango ya nyumba yako na juu ya malango yako.

106:10 Mwa 11:4; Kum 12:29; 19:1; Yos 24:13Wakati Bwana Mungu wako atakapokuleta katika nchi aliyowaapia baba zako, Abrahamu, Isaki na Yakobo, kukupa wewe, nchi kubwa, ina miji inayopendeza ambayo hukuijenga, 116:11 Yer 22:13; Law 26:5; Kum 8:10; 11:29; 31:20nyumba zilizojaa vitu vizuri vya aina nyingi ambavyo hukuvijaza, visima ambavyo hukuchimba, na mashamba ya mizabibu na mizeituni ambayo hukupanda wewe, basi, utakapokula na kushiba, 126:12 Kum 4:9, 23; 2Fal 17:38; Za 44:17; 78:7; 103:2jihadhari usije ukamwacha Bwana, aliyekutoa katika nchi ya Misri, kutoka nchi ya utumwa.

136:13 Za 33:8; 34:9; Kum 13:4; 1Sam 7:3; Yer 44:10; Mt 4:10; Lk 4:4, 8; 1Sam 20:3; Kut 20:7; Mt 5:33Utamcha Bwana Mungu wako, na umtumikie yeye peke yake na kuapa kwa jina lake. 14Usifuate miungu mingine, miungu ya mataifa yanayokuzunguka; 156:15 Kum 4:24kwa kuwa Bwana Mungu wako, ambaye yuko katikati yako, ni Mungu mwenye wivu na hasira yake itawaka dhidi yako, naye atakuangamiza kutoka uso wa nchi. 166:16 Kut 17:2; Mt 4:7; Lk 4:12Usimjaribu Bwana Mungu wako kama ulivyofanya huko Masa. 176:17 Law 26:3; Kum 11:22; Za 119:4-5, 56, 100, 134, 168Utayashika maagizo ya Bwana Mungu wako kwa bidii, na masharti na amri alizokupa. 186:18 2Fal 18:6; Isa 36:7; 38:3; Kum 4:40Fanya lililo haki na jema mbele za Bwana, ili upate kufanikiwa, uweze kuingia na kuimiliki nchi nzuri ambayo Bwana aliahidi kwa kiapo kwa baba zako, 196:19 Kut 23:27; Yos 21:44; Za 78:53; 107:2; 136:24kuwafukuza kwa nguvu adui zako mbele yako kama Bwana alivyosema.

206:20 Kut 10:2; 13:14Siku zijazo, mtoto wako atakapokuuliza, “Ni nini maana ya masharti haya, amri na sheria hizi ambazo Bwana Mungu wako alikuagiza wewe?” 216:21 Kum 4:34Mwambie: “Tulikuwa watumwa wa Farao huko Misri, lakini Bwana alitutoa sisi kutoka Misri kwa mkono wenye nguvu. 22Bwana akapeleka mbele yetu ishara za miujiza na maajabu makubwa na ya kutisha mno juu ya Misri na Farao pamoja na nyumba yake yote. 23Lakini Mungu akatutoa huko, akatuleta na kutupa nchi hii ambayo aliwaahidi baba zetu kwa kiapo. 246:24 Kum 10:12; 30:6; Za 86:11; Yer 32:39; Za 27:12; 41:2; Rum 10:5Bwana akatuagiza tutii amri hizi zote na kumcha Bwana Mungu wetu, ili tupate kustawi na kuendelea kuwa hai kama ilivyo leo. 256:25 Za 103:18; 119:34, 55; Kum 24:13; Rum 9:31Kama tukizitii kwa bidii amri hizi zote mbele za Bwana Mungu wetu, kama alivyotuamuru sisi, hiyo itakuwa haki yetu.”