尼希米记 4 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

尼希米记 4:1-23

尼希米战胜阻力

1参巴拉听说我们正在重建城墙,非常愤怒,就嘲笑犹太人, 2当着他的同僚和撒玛利亚军兵的面说:“这群弱小的犹太人在做什么呢?要重建城墙吗?要献祭吗?要在一日之间建好吗?要用废墟中烧过的石头来建造吗?”

3他身旁的多比雅说:“他们建的石墙,一只狐狸上去就能踩倒!”

4我祷告说:“我们的上帝啊,求你垂听,因为我们正在被人耻笑。求你使他们对我们的凌辱归到他们自己头上,使他们被掳到外邦。 5不要遮掩他们的恶行,也不要从你面前涂抹他们的罪恶,因为他们在这些建造的人面前惹你发怒。”

6众人全心做工,把整个城墙连接起来,高达原来的一半。

7参巴拉多比雅阿拉伯人、亚扪人和亚实突人听说耶路撒冷的城墙正在重建、缺口正在填补,非常愤怒, 8便一起图谋袭击耶路撒冷,使城内混乱。 9但我们向我们的上帝祷告,并设立守卫昼夜防备他们。

10犹大人说:“工人已经筋疲力尽,还有太多瓦砾有待清理,我们自己无法重建城墙。” 11我们的敌人说:“我们要趁他们不知不觉,进入他们中间杀死他们,阻止他们的工作。” 12靠近敌人居住的犹太人十次来告诉我们,说敌人会从各方来袭击我们4:12 本节希伯来文意义不明。13于是,我按宗族派人手持刀剑、长矛和弓箭守卫在城墙后面低洼的空地上。 14我察看形势后,起来对贵族、官员和其他民众说:“不要怕他们!要记住,主伟大而可畏。要为你们的兄弟、儿女、妻子和家园而战。”

15敌人听说我们知道了他们的阴谋,上帝已破坏他们的诡计,就没有来。我们回到城墙那里,继续各人的工作。 16从那时起,我的仆人一半继续修筑城墙,一半身穿盔甲,手持长矛、盾牌和弓箭负责守卫。官长都站在修筑城墙的所有犹大人后面。 17搬运工人一手工作,一手拿兵器。 18修筑城墙的人工作的时候都腰间配剑。吹号的人在我旁边, 19我对贵族、官员和其余的民众说:“这工程浩大,范围广阔,我们在城墙上相隔很远, 20因此你们一听见号角声,就要聚到我那里。我们的上帝必为我们争战!”

21这样,从黎明直到星星出现,我们的人一半工作,一半手持兵器守卫。 22那时,我又吩咐众人各带仆人在耶路撒冷住宿。他们夜间可以帮我们守卫,白天帮我们工作。 23我和我的兄弟、仆人及跟从我的守卫都衣不解带,刀不离身4:23 刀不离身”或译“出去打水时也带着刀”。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Nehemia 4:1-23

Upinzani Wakati Wa Ujenzi

14:1 Ezr 4:1-5; Neh 2:10Sanbalati aliposikia kwamba tulikuwa tunajenga ukuta upya, alikasirika na akawa na uchungu sana. Aliwadhihaki Wayahudi 24:2 Ezr 4:9-10; Yer 26:18mbele ya rafiki zake na jeshi la Samaria, akisema, “Hawa Wayahudi wanyonge wanafanya nini? Je, wataweza kuurudishia ukuta wao? Je, watatoa dhabihu? Je, wataweza kumaliza kuujenga kwa siku moja? Je, wataweza kufufua mawe kutoka malundo ya vifusi yaliyoungua hivyo?”

34:3 Neh 2:10; Ay 13:12; 15:3Tobia Mwamoni aliyekuwa upande wake akasema, “Wanachokijenga, hata kama mbweha angepanda juu yake, huo ukuta wao wa mawe angeliubomoa!”

44:4 Za 79:12; 123:3-4; Yer 33:24; Hos 12:14Ee Mungu wetu, utusikie, kwa kuwa tumedharauliwa. Warudishie matukano yao kwenye vichwa vyao wenyewe. Uwatoe ili wawe nyara katika nchi ya waliowateka. 54:5 Za 59:5-13; 2Fal 14:21; Mao 1:22; Isa 2:9; Yer 18:23Usiusitiri uovu wao, wala usifute dhambi zao mbele zako, kwa kuwa wamewatukana wajenzi mbele.

6Basi tuliujenga upya ukuta mpaka wote ukafikia nusu ya kimo chake, kwa kuwa watu walifanya kazi kwa moyo wote.

74:7 Neh 2:10Lakini wakati Sanbalati, Tobia, Waarabu, Waamoni na watu wa Ashdodi waliposikia kuwa ukarabati wa kuta za Yerusalemu ulikuwa umeendelea na mianya ilikuwa inazibwa, walikasirika sana. 84:8 Mdo 23:12-13; Za 2:1-3; 83:1-18Wote walifanya shauri pamoja kuja kupigana dhidi ya Yerusalemu, na kuchochea machafuko dhidi yake. 94:9 Ay 22:27; Za 50:15; Mt 26:41Lakini tulimwomba Mungu wetu, na tukaweka ulinzi usiku na mchana kupambana na tishio hili.

104:10 1Nya 23:4Wakati ule ule, watu wa Yuda wakasema, “Nguvu za wafanyakazi zinapungua, nacho kifusi ni kingi mno, kiasi kwamba hatuwezi kuujenga upya ukuta.”

11Pia adui zetu walisema, “Kabla hawajajua au kutuona, tutakuwa palepale katikati yao, na tutawaua na kuikomesha hiyo kazi.”

12Kisha Wayahudi ambao waliishi karibu nao walikuja zaidi ya mara kumi na kutuambia, “Popote mtakapoelekea, watatushambulia.”

13Kwa hiyo nikaweka baadhi ya watu nyuma ya sehemu za chini za ukuta kwenye sehemu zilizo wazi, nikawaweka kufuatana na jamaa zao, wakiwa na panga, mikuki na pinde zao. 144:14 Mwa 28:15; Hes 14:9; Neh 1:5-8; Ay 37:22; 2Sam 10:12Baada ya kuona hali ilivyo, nikasimama na kuwaambia wakuu, maafisa na wengine wote, “Msiwaogope. Mkumbukeni Bwana, ambaye ni mkuu mwenye kuogofya. Piganeni kwa ajili ya ndugu zenu, wana wenu na binti zenu, wake zenu na nyumba zenu.”

154:15 2Sam 17:14; Ay 5:12Adui zetu waliposikia kwamba tumetambua hila yao, na kwamba Mungu amevuruga shauri lao, sote tulirudi kwenye ukuta, kila mmoja kwenye kazi yake.

16Kuanzia siku ile na kuendelea, nusu ya watu wangu walifanya kazi ya ujenzi, na nusu nyingine wakashika mikuki, ngao, pinde na dirii. Maafisa walijipanga nyuma ya watu wote wa Yuda 174:17 1Kor 16:13; Za 149:6waliokuwa wakijenga ukuta. Wale waliobeba vifaa vya ujenzi walifanya kazi yao kwa mkono mmoja, na kushika silaha kwa mkono mwingine, 184:18 Hes 10:2na kila mjenzi alijifunga upanga wake upande mmoja akiwa anafanya kazi. Lakini mtu wa kupiga baragumu alikaa pamoja nami.

19Kisha nikawaambia wakuu, maafisa na watu wengine wote, “Kazi hii ni kubwa na imeenea sehemu kubwa, nasi tumetawanyika kila mmoja akiwa mbali na mwenzake juu ya ukuta. 204:20 Eze 33:3; Kut 14:14; Kum 1:30; Yos 10:14Popote mtakaposikia sauti ya baragumu, jiungeni nasi huko. Mungu wetu atatupigania!”

21Basi tuliendelea na kazi, nusu ya watu wakishikilia mikuki, kuanzia mawio ya jua hadi nyota zilipoonekana. 22Wakati huo pia niliwaambia watu, “Kila mtu na msaidizi wake wakae ndani ya Yerusalemu wakati wa usiku, ili waweze kutumika kama walinzi wakati wa usiku, na kufanya kazi wakati wa mchana.” 23Mimi, wala ndugu zangu, wala watu wangu, wala walinzi waliokuwa pamoja nami hatukuvua nguo zetu. Kila mmoja alikuwa na silaha yake, hata alipokwenda kuchota maji.