历代志下 35 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

历代志下 35:1-27

约西亚守逾越节

1约西亚耶路撒冷为耶和华守逾越节。一月十四日,众人宰杀逾越节的祭牲。 2他指派祭司各尽其职,鼓励他们在耶和华的殿里事奉, 3又对将自己献给耶和华、负责教导以色列人的利未人说:“你们把圣约柜放在以色列大卫的儿子所罗门建的殿里,不用再扛在肩上。现在你们去事奉你们的上帝耶和华和祂的以色列子民吧。 4你们要按宗族和班次,依照以色列大卫和他儿子所罗门所写的指示,预备自己。 5你们要按你们弟兄所在宗族的班次,侍立在圣所,每个班次中要有几个利未宗族的人。 6你们要宰杀逾越节的羊羔,洁净自己,为你们的弟兄做好准备,依照耶和华借摩西所吩咐的去行。”

7约西亚从自己的产业中,捐出三万只绵羊羔和山羊羔,以及三千头公牛,赐给所有在场的人做逾越节的祭牲。 8他的众官员也自愿为民众、祭司和利未人捐献。管理上帝殿的希勒迦撒迦利亚耶歇献出两千六百只羊羔和三百头牛,给祭司做逾越节的祭牲。 9利未人的首领歌楠雅和他的两个兄弟示玛雅拿坦业,及哈沙比雅耶利约撒拔献出五千只羊羔和五百头牛,给利未人做逾越节的祭牲。

10一切都准备好后,依照王的吩咐,祭司站在自己的地方,利未人按照班次侍立。 11利未人宰杀逾越节的羊羔,祭司从他们手中接过血,洒在坛上,又剥去祭牲的皮。 12他们按照宗族把燔祭分给众人,好使他们按照摩西书上所写的,把祭物献给耶和华。献牛也是这样。 13他们按规定用火烤逾越节的羊羔,在锅里、罐里和盆里煮圣物,然后迅速分给民众。 14之后,利未人为自己和祭司预备祭物,因为做祭司的亚伦子孙要继续献燔祭和脂肪一直到晚上。 15负责歌乐的亚萨子孙依照大卫亚萨希幔和王的先见耶杜顿的吩咐,站在自己的岗位上;殿门守卫都看守各门,不必离开工作岗位,因为他们的弟兄利未人为他们预备了祭物。

16当天,一切事奉的事都办好了,他们就按约西亚王的命令守逾越节,又在耶和华的坛上献燔祭。 17所有在场的以色列人都在那时守逾越节,又守除酵节七天。 18撒母耳先知以来,在以色列从来没有守过这样的逾越节,以色列从没有君王像约西亚、祭司、利未人、所有在场的犹大人和以色列人,以及耶路撒冷的居民这样守过逾越节。 19这次逾越节是在约西亚执政第十八年庆祝的。

约西亚逝世

20约西亚办理完殿里的事后,埃及尼哥上来,要攻打幼发拉底河附近的迦基米施约西亚出兵拦阻。 21尼哥派使者对约西亚说:“犹大王啊,我与你没有恩怨。我今天来不是要攻击你,乃是要攻击与我作战的那一家。上帝吩咐我要速速完成,你不要与上帝作对,免得祂毁灭你,因为上帝与我同在。” 22约西亚却不听上帝借尼哥说的话。他没有退兵,反而乔装上阵,与尼哥会战于米吉多平原。 23约西亚王在战场上中箭受伤,就对仆人说:“我受了重伤,带我离开吧。” 24他的仆人就扶他下战车,上另一辆战车,送到耶路撒冷约西亚死在那里,葬在他祖先的坟墓里。所有犹大耶路撒冷的人都为他哀悼。 25耶利米约西亚作了哀歌,所有的男女歌乐手至今仍用这些哀歌纪念约西亚,成了以色列的传统。这些哀歌都记在《哀歌书》上。

26约西亚其他的事迹和他怎样忠心地遵行耶和华的律法, 27自始至终都记在《以色列和犹大的列王史》上。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

2 Nyakati 35:1-27

Mfalme Yosia Anaadhimisha Pasaka

(2 Wafalme 23:21-23)

135:1 Kut 12:1-30; Hes 9:3; Eze 45:21; Ezr 6:17; 2Fal 23:21Yosia akaadhimisha Pasaka kwa Bwana katika Yerusalemu, mwana-kondoo wa Pasaka akachinjwa siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza. 235:2 Ezr 6:18-19; 2Nya 23:18; 29:11Akawaweka makuhani kwenye wajibu wao na kuwatia moyo katika utumishi wa Hekalu la Bwana. 335:3 Kum 33:10; 1Nya 23:26; 2Nya 34:14; 30:22; 5:7Akawaambia Walawi, waliowafundisha Waisraeli wote na waliokuwa wamejiweka wakfu kwa ajili ya kazi ya Bwana, “Liwekeni hilo Sanduku takatifu katika Hekalu lile alilojenga Solomoni mwana wa Daudi mfalme wa Israeli. Halipaswi kubebwa huku na huko mabegani mwenu. Sasa mtumikieni Bwana Mungu wenu na watu wake Israeli. 435:4 1Nya 9:10-13; Ezr 6:15; 2Nya 8:14Jiandaeni kwa kufuata jamaa zenu katika migawanyo yenu, kufuatana na maelezo yaliyoandikwa na Daudi mfalme wa Israeli na mwanawe Solomoni.

5“Simameni mahali patakatifu kwa kufuata migawanyo ya jamaa za baba zenu kulingana na koo zenu na pawepo Walawi kwa ajili ya kila mgawanyo wa nyumba ya baba zenu. 635:6 Law 11:44; 2Nya 29:5-15; Kut 19:10; Ebr 9:13-14; Kut 19:10; Ezr 6:20; Za 51:7; Yoe 2:16; 2Nya 30:3, 15Chinjeni mwana-kondoo wa Pasaka, jitakaseni, nanyi kwa niaba ya koo zenu fanyeni maandalizi, mkitenda sawasawa na neno la Bwana kwa mkono wa Mose.”

735:7 2Nya 30:24; Mik 6:7; 2Nya 31:3Ndipo Yosia akawapa watu wote wana-mbuzi waliokuwepo jumla ya kondoo wapatao 30,000 kwa ajili ya sadaka ya Pasaka, pia na ngʼombe 10,000, vyote hivi kutoka mali binafsi ya mfalme.

835:8 1Nya 29:3; 6:13; 2Kor 9:7Pia maafisa wake, wakatoa kwa hiari yao wakawapa watu, makuhani na Walawi. Hilkia, Zekaria na Yehieli, waliokuwa maafisa wakuu wa Hekalu la Mungu, wakawapa makuhani sadaka za Pasaka wana-kondoo na wana-mbuzi 2,600 na mafahali 300. 935:9 2Nya 31:12-13Konania na nduguze wawili, Shemaya na Nethaneli, pamoja na Hashabia, Yeieli na Yozabadi waliokuwa viongozi wa Walawi, nao pia wakawapa Walawi wana-kondoo na wana-mbuzi 5,000 na mafahali 500, kwa ajili ya sadaka za Pasaka.

1035:10 Ezr 6:18; 2Nya 30:16Huduma ilipomalizika kuandaliwa makuhani wakasimama mahali pao na Walawi katika migawanyo yao kama mfalme alivyokuwa ameamuru. 1135:11 2Nya 29:22; 30:17Wana-kondoo wa Pasaka wakachinjwa, nao makuhani wakanyunyiza ile damu waliyokabidhiwa, wakati Walawi wakiwa wanawachuna wale wanyama ngozi. 1235:12 Law 3:3Wakatenga sadaka za kuteketezwa ili waweze kugawia ili migawanyo kwa kufuata jamaa za baba zao ili watoe sadaka kwa Bwana kama ilivyoandikwa katika Kitabu cha Mose. Wakafanya vivyo hivyo kwa wale mafahali. 1335:13 Law 6:25; 1Sam 2:13-15; Kut 12:8; 13:6; Law 23:5-6; 2Nya 30:21; 1Kor 5:7-8Wakawaoka wale wanyama wa Pasaka kwenye moto kama ilivyoamriwa, wakachemsha zile sadaka takatifu kwenye vyungu, masufuria makubwa na vikaango na kuwagawia watu wote upesi. 1435:14 Kut 29:13Hatimaye wakafanya maandalizi kwa ajili yao wenyewe na kwa ajili ya makuhani, kwa sababu wale makuhani, yaani, wazao wa Aroni, walikuwa wanatoa sadaka za kuteketezwa pamoja na zile sehemu zilizonona mpaka usiku. Hivyo Walawi wakafanya maandalizi kwa ajili yao wenyewe na kwa ajili ya makuhani wa uzao wa Aroni.

1535:15 Neh 12:46; Za 68:25Waimbaji, wazao wa Asafu, walikuwa katika nafasi zao, kama ilivyoagizwa na Mfalme Daudi, Asafu, Hemani na Yeduthuni mwonaji wa Mfalme. Mabawabu katika kila lango hawakuhitaji kuacha nafasi zao kwa sababu Walawi wenzao walifanya maandalizi kwa ajili yao.

1635:16 2Nya 3:10; Za 35:16; Yer 5:12; 32:3Kwa hiyo wakati ule huduma yote ya Bwana ilifanyika katika kuadhimisha Pasaka, kutoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu ya Bwana kama alivyoamuru Mfalme Yosia. 1735:17 Kut 12:15; Hes 28:16-17; Kum 16:3-8Waisraeli waliokuwepo wakaadhimisha Pasaka wakati huo na Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu kwa siku saba. 1835:18 2Fal 23:22-23Kulikuwa hakujafanyika Pasaka kama hii katika Israeli tangu siku za nabii Samweli wala hakukuwa na mfalme yeyote wa Israeli ambaye kamwe alishaadhimisha Pasaka kama ile aliyofanya Mfalme Yosia, akiwa na makuhani, Walawi na watu wote wa Yuda na watu wa Israeli waliokuwepo huko, pamoja na watu wa Yerusalemu. 19Pasaka iliadhimishwa katika mwaka wa kumi na nane wa utawala wa Mfalme Yosia.

Kifo Cha Yosia

(2 Wafalme 23:28-30)

2035:20 Isa 10:9; Yer 46:2; Mwa 2:14; 2Fal 23:29; 25:11Baada ya haya yote, Yosia alipomaliza kulitengeneza vizuri Hekalu, Neko mfalme wa Misri, akapanda ili kupigana huko Karkemishi katika Mto Frati, naye Yosia akatoka kwenda kupigana naye. 2135:21 2Fal 18:25; Dan 4:35; 1Fal 13:18; Isa 36:10; Yer 25:9Lakini Neko akamtumia wajumbe kusema, “Kuna ugomvi gani kati yangu mimi na wewe, Ee Mfalme wa Yuda? Si wewe ninayekushambulia wakati huu, bali ile nyumba ambayo nina vita nayo, Mungu ameniambia niharakishe, kwa hivyo acha kumpinga Mungu, ambaye yuko pamoja nami, la sivyo atakuangamiza.”

2235:22 Amu 5:19; 1Sam 28:8; 1Fal 22:30; 14:2; 2Nya 18:29Lakini hata hivyo, Yosia hakukubali kumwacha, bali alijibadilisha ili kupigana naye vita. Hakusikiliza yale Neko aliyokuwa amemwambia kwa agizo la Mungu bali alikwenda kupigana naye katika tambarare ya Megido.

2335:23 1Fal 22:34; Dan 2:21Wapiga upinde wakampiga Mfalme Yosia, naye akawaambia maafisa wake, “Niondoeni, nimejeruhiwa vibaya sana.” 2435:24 2Fal 23:30; Zek 12:11Kwa hiyo wakamshusha kutoka kwenye gari lake la farasi, wakamweka kwenye gari lingine alilokuwa nalo na kumleta Yerusalemu, ambako alifia. Akazikwa katika makaburi ya baba zake, nayo Yuda yote na Yerusalemu wakamwombolezea Yosia.

2535:25 Mwa 50:10; Yer 22:10-16; Mao 4:20; Mt 9:23; Amo 5:16; Mhu 12:5; Yer 9:17Nabii Yeremia akatunga maombolezo kwa ajili ya kifo chake, nao waimbaji wote, wanaume kwa wanawake, hufanya ukumbusho wa Yosia katika maombolezo hadi leo. Haya yakafanywa desturi katika Israeli, nayo yameandikwa katika Maombolezo.

2635:26 Za 112:6; Mit 10:7; 22:1Matukio mengine ya utawala wa Yosia na matendo yake mema, kulingana na yale yaliyoandikwa katika sheria ya Bwana: 27matukio yote, kuanzia mwanzo hadi mwisho, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli na Yuda.