历代志上 10 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

历代志上 10:1-14

扫罗之死

1非利士人与以色列人交战,以色列人败逃,许多人在基利波山被杀。 2非利士人穷追扫罗及其众子,杀了扫罗的儿子约拿单亚比拿达麦基舒亚3扫罗周围的战斗非常猛烈,他被弓箭手发现、射成重伤, 4就对为他拿兵器的人说:“拔出你的刀来刺死我吧!免得那些未受割礼的人来凌辱我。”但拿兵器的人非常害怕,不敢动手,扫罗就自己伏刀自尽。 5拿兵器的人看见扫罗已死,也伏刀自尽了。 6这样,扫罗和他的三个儿子及全家都死了。 7住在山谷中的以色列人看见以色列军败逃、扫罗及其众子已死,都弃城而逃。于是,非利士人占领了那些城邑。 8次日,非利士人来剥阵亡者的衣物,发现扫罗及其众子横尸基利波山, 9就剥下扫罗的盔甲,割下他的头颅,并派人到非利士四境向他们的偶像和民众通告消息。 10他们将扫罗的盔甲放在他们的神庙里,把他的头颅挂在大衮神庙中。 11基列·雅比人听见非利士人对扫罗的所作所为, 12他们所有的勇士就去把扫罗和他儿子们的尸体运到雅比,葬在雅比的橡树下,并禁食七天。 13扫罗死了,因为他对耶和华不忠,不听从祂的教诲,甚至去求问灵媒, 14而不求问耶和华。因此,耶和华使他被杀,把王位交给了耶西的儿子大卫

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

1 Nyakati 10:1-14

Sauli Ajiua

(1 Samweli 31:1-13)

110:1 1Sam 7:7; 13:5; 31:1Basi Wafilisti wakapigana na Israeli. Waisraeli wakawakimbia, na wengi wakauawa katika mlima Gilboa. 2Wafilisti wakawafuatia kwa bidii Sauli na wanawe, wakawaua Yonathani, Abinadabu na Malki-Shua. 3Mapigano yakawa makali kumzunguka Sauli na wakati wapiga mishale walipompata, wakamjeruhi.

410:4 Amu 16:21Sauli akamwambia mbeba silaha wake, “Futa upanga wako unichome nao, la sivyo hawa watu wasiotahiriwa watakuja na kunidhalilisha.”

Lakini mbeba silaha wake akaogopa sana wala hakuweza kufanya hivyo. Kwa hiyo Sauli akachukua upanga wake mwenyewe na kuuangukia. 5Mbeba silaha wake alipoona kwamba Sauli amekufa, naye pia akauangukia upanga wake akafa. 6Kwa hiyo Sauli na wanawe watatu wakafa, pamoja na nyumba yake yote.

7Waisraeli wote waliokuwa bondeni walipoona kwamba jeshi limekimbia na kwamba Sauli na wanawe wamekufa, waliacha miji yao wakakimbia. Nao Wafilisti wakaja na kukaa humo.

8Kesho yake Wafilisti walipokuja kuwavua maiti silaha, walimkuta Sauli na wanawe wameanguka katika Mlima Gilboa. 9Wakamvua mavazi, wakachukua kichwa chake pamoja na silaha zake, wakawatuma wajumbe katika nchi yote ya Wafilisti kutangaza habari hizi miongoni mwa sanamu zao na watu wao. 1010:10 Amu 16:23; 1Sam 31:10; Isa 48:5Waliweka silaha zake katika hekalu la miungu yao, wakatundika kichwa chake katika hekalu la Dagoni.

1110:11 Amu 21:8Wakazi wote wa Yabeshi-Gileadi waliposikia yote Wafilisti waliyomtendea Sauli, 12mashujaa wao wote wakaondoka, wakautwaa mwili wa Sauli na miili ya wanawe, wakaileta Yabeshi. Wakaizika mifupa yao chini ya mti mkubwa huko Yabeshi, nao wakafunga kwa siku saba.

1310:13 2Sam 1; 1; 15:23; 1Nya 5:25; 1Sam 13:13; Kum 18:9-14; 1Sam 28:7; 1Fal 18:18; 2Nya 16:9; Kut 22:18; Law 19:31; 20:27; 2Fal 21:6Sauli alikufa kwa sababu hakuwa mwaminifu kwa Bwana. Hakulishika neno la Bwana, hata akataka shauri kwa mwaguzi kwa ajili ya uongozi, 1410:14 1Nya 12:23; 1Sam 13:14; 15:28hakumuuliza Bwana. Kwa hiyo Bwana alimuua, na ufalme akampa Daudi mwana wa Yese.