创世记 2 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

创世记 2:1-25

1天地万物都造好了。 2第七天,上帝完成了祂的创造之工,就在第七天歇了一切的工。 3上帝赐福给第七天,将其定为圣日,因为祂在这一天歇了祂一切的创造之工。 4这是有关创造天地的记载。

上帝造亚当和夏娃

耶和华上帝创造天地的时候, 5地上还没有草木菜蔬,因为耶和华上帝还没有降雨在地上,土地也没有人耕作, 6但有水从地里涌出,浇灌大地。 7耶和华上帝用地上的尘土造了人,把生命的气息吹进他的鼻孔里,他就成了有生命的人。 8耶和华上帝在东方的伊甸开辟了一个园子,把祂所造的人安置在里面。 9耶和华上帝使地面长出各种树木,它们既好看又能结出可吃的果子。在园子的中间有生命树和分别善恶的树。

10有一条河从伊甸流出来灌溉那园子,又从那里分出四条支流。 11第一条支流叫比逊河,它环绕着哈腓拉全境。那里有金子, 12且是上好的金子,还有珍珠和红玛瑙。 13第二条支流是基训河,它环绕着古实全境。 14第三条支流名叫底格里斯河,它流经亚述的东边。第四条支流是幼发拉底河。

15耶和华上帝把那人安置在伊甸的园子里,让他在那里耕种、看管园子。 16耶和华上帝吩咐那人说:“你可以随意吃园中所有树上的果子, 17只是不可吃那棵分别善恶树的果子,因为你若吃了,当天必死。”

18耶和华上帝说:“那人独自一人不好,我要为他造一个相配的帮手。” 19耶和华上帝用尘土造了各种田野的走兽和空中的飞鸟,把它们带到那人跟前,看他怎么称呼这些动物。他叫这些动物什么,它们的名字就是什么。 20那人给所有的牲畜及田野的走兽和空中的飞鸟都起了名字。可是他找不到一个跟自己相配的帮手。 21耶和华上帝使那人沉睡,然后从他身上取出一根肋骨,再把肉合起来。 22耶和华上帝用那根肋骨造成一个女人,带到那人跟前。 23那人说:

“这才是我的同类,

我骨中的骨,肉中的肉,

要称她为女人,

因为她是从男人身上取出来的。”

24因此,人要离开父母,与妻子结合,二人成为一体。 25当时,他们夫妇二人都赤身露体,并不觉得羞耻。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Mwanzo 2:1-25

12:1 Kum 4:19; 17:3; 2Fal 17:16; 21:3; Za 104:2; Isa 44:24; 45:12; 48:13; 51:13Kwa hiyo mbingu na dunia zikakamilika, pamoja na vyote vilivyomo.

22:2 Kum 5:14; Ebr 4:4; Kut 20:11; 31:17; 34:21; Yn 5:17Katika siku ya saba Mungu alikuwa amekamilisha kazi aliyokuwa akiifanya, hivyo siku ya saba akapumzika kutoka kazi zake zote. 32:3 Kut 16:23; 20:10; 23:12; 31:15; 35:2; Law 23:3; Ebr 4:11; Neh 9:14; Mwa 1:1; Za 95:11; Isa 58:13; Yer 17:22Mungu akaibariki siku ya saba akaifanya takatifu, kwa sababu katika siku hiyo alipumzika kutoka kazi zote za kuumba alizokuwa amefanya.

Adamu Na Eva

42:4 Mwa 5:1; 6:9; 1:1; 10:1; 11:10; 27:25; Ay 38:8-11Haya ndiyo maelezo ya mbingu na dunia wakati zilipoumbwa.

Bwana Mungu alipoziumba mbingu na dunia, 52:5 Mwa 1:11; Ay 38:28; Za 65:9-10; Yer 10:13hapakuwepo na mche wa shambani uliokuwa umejitokeza ardhini, wala hapakuwepo na mmea wa shamba uliokuwa umeota, kwa kuwa Bwana Mungu alikuwa hajanyeshea mvua juu ya nchi, na hapakuwepo mtu wa kuilima ardhi, 6lakini umande ulitokeza kutoka ardhini na kunyesha uso wote wa nchi: 72:7 Isa 29:16; 43:1, 21; 44:2; Mwa 1:27; 3:19; 18:27; 5:23; 4:2; Ay 4:19; 10:9; 17:16; 34:15; Za 103:14; 90:3; Mhu 3:20; 12:7Bwana Mungu alimuumba mtu kutoka mavumbi2:7 Neno la Kiebrania la mavumbi ya ardhi ndilo kiini cha jina Adamu. ya ardhi, akampulizia pumzi ya uhai puani mwake, naye mtu akawa kiumbe hai.

82:8 Mwa 3:23-24; 4:16; 13:10; Isa 51:3; Eze 28:13; 36:35; 31:9, 16; Yoe 2:3Basi Bwana Mungu alikuwa ameotesha bustani upande wa mashariki, katika Edeni, huko akamweka huyo mtu aliyemuumba. 92:9 Eze 31:8; 47:12; Mit 3:18; 11:30; Ufu 2:7; Mwa 3:22, 24Bwana Mungu akafanya aina zote za miti ziote kutoka ardhini, miti yenye kupendeza macho na mizuri kwa chakula. Katikati ya bustani ulikuwepo mti wa uzima na mti wa kujua mema na mabaya.

102:10 Hes 24:6; Eze 47:5; Za 46:4Mto wa kunyeshea bustani ulitiririka toka Edeni, kuanzia hapa ukagawanyika kuwa mito minne. 112:11 Mwa 10:7; 25:18Mto wa kwanza uliitwa Pishoni, nao huzunguka nchi yote ya Havila ambako kuna dhahabu. 122:12 Hes 11:7(Dhahabu ya nchi hiyo ni nzuri, bedola na vito shohamu pia hupatikana huko.) 13Jina la mto wa pili ni Gihoni, ambao huzunguka nchi yote ya Kushi. 142:14 Mwa 15:18; 41:1; 31:21; Dan 10:4; Kut 23:31; Hes 22:5; Ufu 9:14; 1Fal 4:21; 2Sam 8:3; Kum 11:24; 2Fal 23:29; 24:7; 1Nya 5:9; 18:3; 2Nya 35:20; Yer 13:4; 42:6; 51:63Jina la mto wa tatu ni Tigrisi, unaopita mashariki ya Ashuru. Mto wa nne ni Frati.

15Bwana Mungu akamchukua huyo mtu, akamweka kwenye Bustani ya Edeni ailime na kuitunza. 162:16 Mwa 3:1-2Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu, akamwambia, “Uko huru kula matunda ya mti wowote katika bustani, 172:17 Mwa 3:11, 17; 9:29; Yer 42:16; Kum 30:15, 19; Eze 3:18; Rum 5:13; 6:23lakini kamwe usile matunda ya mti wa kujua mema na mabaya, kwa maana siku utakapokula matunda yake, hakika utakufa.”

182:18 Mit 11:31; 1Kor 11:9; 1Tim 2:13Bwana Mungu akasema, “Si vyema huyu mtu awe peke yake. Nitamfanyia msaidizi wa kumfaa.”

192:19 Za 8:7; Mwa 1:5, 20, 24Basi Bwana Mungu alikuwa amefanyiza kutoka ardhi wanyama wote wa porini na ndege wote wa angani. Akawaleta kwa huyu mtu aone atawaitaje, nalo jina lolote alilokiita kila kiumbe hai, likawa ndilo jina lake. 202:20 Mwa 3:20; 4:1Hivyo Adamu akawapa majina wanyama wote wa kufugwa, ndege wa angani, na wanyama wote wa porini.

Lakini kwa Adamu hakupatikana msaidizi wa kumfaa. 212:21 Mwa 15:12; 1Sam 26:12; Ay 33:15Hivyo Bwana Mungu akamfanya Adamu kulala usingizi mzito, naye alipokuwa amelala akachukua moja ya mbavu zake, akapafunika mahali pale kwa nyama. 222:22 1Kor 11:8-9, 12; 1Tim 2:12Kisha Bwana Mungu akamfanya mwanamke kutoka kwenye ule ubavu aliouchukua kutoka kwa huyo mwanaume, akamleta huyo mwanamke kwa huyo mwanaume.

232:23 Mwa 29:14; Efe 5:28-30; 1Kor 11:8Huyo mwanaume akasema,

“Huyu sasa ni mfupa wa mifupa yangu

na nyama ya nyama yangu,

ataitwa ‘mwanamke,’2:23 Jina la Kiebrania la mwanamke linafanana na lile la mwanaume.

kwa kuwa alitolewa katika mwanaume.”

242:24 Mal 2:15; Mt 19:5; Mk 10:7-8; Efe 5:31; 1Kor 6:16Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake na kuambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.

252:25 Mwa 3:7, 10-11; Isa 47:3; Mao 1:8Adamu na mkewe wote wawili walikuwa uchi, wala hawakuona aibu.