Daily Manna for Thursday, June 10, 2021

Daily Manna is a daily Bible devotional service provided by Biblica. The Scripture is provided in many forms and is new every day. It is a great way to receive the encouragement and hope found in the Word of God.

Verse of the Day

Matendo 3:19-23

3:19 Za 5:11; Mdo 2:38Tubuni basi mkamgeukie Mungu, dhambi zenu zifutwe, ili zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwepo kwake Bwana, 3:20 Lk 2:11naye apate kumtuma Kristo, ambaye ameteuliwa kwa ajili yenu, yaani Yesu. 3:21 Mdo 1:11; Mt 17:11; Lk 1:70Ilimpasa mbingu zimpokee mpaka wakati wa kufanywa upya kila kitu, kama Mungu alivyoahidi zamani kupitia kwa vinywa vya manabii wake watakatifu. 3:22 Kum 18:15-18; Mdo 7:37Kwa maana Mose alisema, ‘Bwana Mungu wenu atawainulia nabii kama mimi kutoka miongoni mwa ndugu zenu. Itawapasa kumtii huyo kwa kila jambo atakalowaambia. 3:23 Kum 18:19; Law 23:29Mtu yeyote ambaye hatamsikiliza huyo nabii, atatupiliwa mbali kabisa na watu wake.’