Daily Manna for Wednesday, June 9, 2021

Daily Manna is a daily Bible devotional service provided by Biblica. The Scripture is provided in many forms and is new every day. It is a great way to receive the encouragement and hope found in the Word of God.

Verse of the Day

Mithali 1:7-19

1:7 Kut 20:20; Ay 28:28Kumcha Bwana ndicho chanzo cha maarifa,

lakini wapumbavu hudharau hekima na adabu.

1:8 Mit 6:20; 22:17; Kum 21:18Mwanangu, sikiliza mwongozo wa baba yako,

wala usiyaache mafundisho ya mama yako.

1:9 Mit 3:21-22; 4:1-9Hayo yatakuwa taji la maua la neema kichwani pako,

na mkufu wa kuipamba shingo yako.

1:10 Mwa 39:7; Ay 24:15; Kum 13:8; Rum 16:18Mwanangu, kama wenye dhambi wakikushawishi,

usikubaliane nao.

1:11 Mit 12:6; Yer 5:26; Mik 7:2Kama wakisema, “Twende tufuatane;

tukamvizie mtu na kumwaga damu,

njoo tukavizie nafsi isiyo na hatia;

1:12 Ay 33:18; Mwa 38:25; Za 40:3tuwameze wakiwa hai kama kaburi,

wakiwa wazima kama wale wanaotumbukia shimoni.

Tutapata aina zote za vitu vya thamani

na kujaza nyumba zetu kwa nyara.

1:14 Mit 1:19Njoo ushirikiane nasi,

vitu vyote tutakavyopata tutagawana.”

1:15 Za 119:101; Mwa 49:6; Mit 4:14Mwanangu, usiandamane nao.

Usiweke mguu wako katika njia zao,

1:16 Mit 6:18; Isa 59:7kwa kuwa miguu yao hukimbilia kwenye dhambi,

ni wepesi kumwaga damu.

Tazama ni jinsi gani ilivyo kazi bure kutandaza wavu

wakati ndege wote wanakuona!

1:18 Za 71:10Watu hawa huvizia kumwaga damu yao wenyewe;

hujivizia tu wenyewe!

1:19 Mit 11:19; 15:27; 2Fal 5:20-27Huu ndio mwisho wa wote ambao wanajipatia mali kwa hila;

huuondoa uhai wa wale wenye mali.