Daily Manna for Wednesday, April 7, 2021

Daily Manna is a daily Bible devotional service provided by Biblica. The Scripture is provided in many forms and is new every day. It is a great way to receive the encouragement and hope found in the Word of God.

Verse of the Day

2 Samweli 22:1-7

(Zaburi 18)

22:1 Kut 15:1; Amu 5:1; Za 18:2-50Daudi alimwimbia Bwana maneno ya wimbo huu wakati Bwana alipomwokoa mikononi mwa adui zake wote, na pia mkononi mwa Sauli. 22:2 1Sam 2:2; Za 31:3; 91:2; 71:3; 144:2; Kum 32:4; Za 18:2; Mit 18:10; Mt 18:10Akasema:

Bwana ni mwamba wangu,

ngome yangu na mwokozi wangu,

22:3 Mit 10:29; Yoe 3:16; Kum 23:15; 32:37; Za 14:6; 31:2; 59:16; 71:7; 91:2; 94:22; Isa 25:4; Yer 16:19; Mwa 15:1; Kum 33:17; Lk 1:69; Za 9:9; 52:7Mungu wangu ni mwamba wangu,

ambaye kwake ninakimbilia,

ngao yangu na pembe ya wokovu wangu.

Yeye ni ngome yangu, kimbilio langu

na mwokozi wangu,

huniokoa kutoka kwa watu wenye jeuri.

22:4 Za 48:1; 96:4; 145:3Ninamwita Bwana, anayestahili kusifiwa,

nami ninaokolewa kutoka kwa adui zangu.

22:5 Za 69:14-15; Yon 2:3“Mawimbi ya mauti yalinizunguka,

mafuriko ya maangamizi yalinilemea.

22:6 Za 116:3; Mdo 2:24Kamba za kuzimu zilinizunguka,

mitego ya mauti ilinikabili.

22:7 Mwa 35:3; Amu 2:15; 2Nya 15:4; Za 4:1; 77:2; 120:1; Isa 26:16; Za 34:15; 116:4; 116:4; Kut 3:7Katika shida yangu nalimwita Bwana,

nilimlilia Mungu wangu.

Kutoka Hekaluni mwake alisikia sauti yangu,

kilio changu kikafika masikioni mwake.