Daily Manna for Friday, October 30, 2020

Daily Manna is a daily Bible devotional service provided by Biblica. The Scripture is provided in many forms and is new every day. It is a great way to receive the encouragement and hope found in the Word of God.

Verse of the Day

Kumbukumbu 28:1-6

(Walawi 26:3-13; Kumbukumbu 7:12-24)

28:1 Kum 15:5; Law 26:3; Hes 24:7; Kum 26:19; Kut 15:26; Za 106:3; 111:10; Isa 1:19; 3:10; Yer 11:4; 12:16; 1Nya 14:2; Rum 2:10Kama ukimtii Bwana Mungu wako kwa bidii na kufuata amri zake zote ninazokupa leo kwa bidii, Bwana Mungu wako atakuweka juu ya mataifa yote katika dunia. 28:2 Yer 32:24; Zek 1:6Baraka hizi zote zitakuja juu yako na kukupata, kama ukimtii Bwana Mungu wako:

28:3 Za 144:15; Mwa 39:5; Za 128:1-4Utabarikiwa mjini na utabarikiwa mashambani.

28:4 Mwa 49:25; Kum 8:18; Mit 10:22; 1Tim 4:8Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na mazao ya nchi yako na wanyama wako wachanga wa kufugwa, yaani ndama wa makundi yako ya ngʼombe, na wana-kondoo wa makundi yako.

Kapu lako na vyombo vyako vya kukandia vitabarikiwa.

28:6 Za 121:8Utabarikiwa uingiapo na utabarikiwa utokapo.