Neno: Bibilia Takatifu

Warumi 13

Kutii Mamlaka

1Kila mtu hana budi kutii serikali inayotawala. Kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na serikali zote zilizopo zimewekwa na Mungu. Kwa hiyo anayepinga mamlaka inayotawala ana pinga chombo kilichowekwa na Mungu; na watu wanaoasi watajiletea hukumu. Kwa maana watawala hawatishi watu wanaotenda mema bali wale wanaotenda maovu. Kama hupendi kuishi kwa kumwogopa mwenye mamlaka, basi tenda mema naye atakusifu. Maana mwenye mamlaka ni mtumishi wa Mungu kwa manufaa yako. Lakini kama ukitenda maovu, basi ogopa kwa maana hatembei na silaha bure. Yeye ni mtumishi wa Mungu anayetekeleza adhabu ya Mungu juu ya watenda maovu. Kwa hiyo ni lazima kutii wenye mamlaka, si kwa sababu ya kuogopa adhabu tu bali pia kwa ajili ya dhamiri.

Kwa sababu hiyo hiyo mnalipa kodi, kwa maana watawala ni watumishi wa Mungu ambao hutumia muda wao wote kutawala. Wal ipeni wote haki zao; mtu wakodi mlipe kodi; na mtoza ushuru mli pe ushuru; astahilie kunyenyekewa, mnyenyekee; astahiliye hesh ima, mheshimu.

Upendo Na Sheria

Msiwe na deni la mtu ye yote; isipokuwa deni la kupendana; kwa maana ampendaye mwenzake, ameitimiza sheria. Kwa maana amri zisemazo: Usizini, Usiue, Usiibe, Usitamani na amri nyingine zote, zinajumlishwa katika amri hii moja: “Mpende jirani yako kama nafsi yako.” 10 Upendo haumfanyii jirani jambo baya, kwa hiyo upendo unakamilisha sheria zote.

11 Fanyeni hivi mkitambua kuwa sasa tumo katika wakati gani. Huu ni wakati wa kuamka kutoka usingizini, kwa maana wokovu wetu umekaribia zaidi sasa kuliko wakati tulipoamini kwa mara ya kwanza. 12 Usiku unakwisha na mchana unakaribia. Kwa hiyo tutupe kando matendo ya giza, tuvae silaha za nuru. 13 Tuishi maisha ya heshima kama inavyopasa wakati wamchana: si kwa ulafi na ulevi; si kwa ufisadi na uasherati; si kwa ugomvi na wivu. 14 Bali jivikeni Bwana Yesu Kristo, na msitoe nafasi kwa miili yenu yenye asili ya dhambi, kutimiza tamaa zake.

King James Version

Romans 13

1Let every soul be subject unto the higher powers. For there is no power but of God: the powers that be are ordained of God.

Whosoever therefore resisteth the power, resisteth the ordinance of God: and they that resist shall receive to themselves damnation.

For rulers are not a terror to good works, but to the evil. Wilt thou then not be afraid of the power? do that which is good, and thou shalt have praise of the same:

For he is the minister of God to thee for good. But if thou do that which is evil, be afraid; for he beareth not the sword in vain: for he is the minister of God, a revenger to execute wrath upon him that doeth evil.

Wherefore ye must needs be subject, not only for wrath, but also for conscience sake.

For for this cause pay ye tribute also: for they are God's ministers, attending continually upon this very thing.

Render therefore to all their dues: tribute to whom tribute is due; custom to whom custom; fear to whom fear; honour to whom honour.

Owe no man any thing, but to love one another: for he that loveth another hath fulfilled the law.

For this, Thou shalt not commit adultery, Thou shalt not kill, Thou shalt not steal, Thou shalt not bear false witness, Thou shalt not covet; and if there be any other commandment, it is briefly comprehended in this saying, namely, Thou shalt love thy neighbour as thyself.

10 Love worketh no ill to his neighbour: therefore love is the fulfilling of the law.

11 And that, knowing the time, that now it is high time to awake out of sleep: for now is our salvation nearer than when we believed.

12 The night is far spent, the day is at hand: let us therefore cast off the works of darkness, and let us put on the armour of light.

13 Let us walk honestly, as in the day; not in rioting and drunkenness, not in chambering and wantonness, not in strife and envying.

14 But put ye on the Lord Jesus Christ, and make not provision for the flesh, to fulfil the lusts thereof.