Neno: Bibilia Takatifu

Matayo 7

Usihukumu Wengine

1 Usihukumu ili na wewe usihukumiwe. Kwa maana hukumu uta kayotamka juu ya wenzako ndio itakayotumiwa kukuhukumu, na kipimo utakachotoa ndicho utakachopokea. Kwa nini unaangalia kijiti kidogo kilichomo katika jicho la ndugu yako na wala huoni pande la mti lililoko jichoni mwako? Au unawezaje kumwambia ndugu yako, ‘Hebu nikutoe uchafu jichoni mwako,’ wakati jichoni mwako mna pande kubwa? Mnafiki wewe! Toa kwanza pande lililoko jichoni mwako, ndipo utaweza kuona vema, upate kukitoa kipande kilichoko ndani ya jicho la ndugu yako.

“Msiwape mbwa vitu vitakatifu; na msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe wasije wakazikanyaga kanyaga na halafu wawageukie na kuwashambulia.”

Omba, Tafuta, Bisha Hodi

“Ombeni nanyi mtapewa. Tafuteni nanyi mtapata; bisheni hodi nanyi mtafunguliwa mlango. Kwa sababu kila aombaye hupewa; naye atafutaye hupata; na abishaye hodi atafunguliwa mlango.

“Au ni nani kati yenu ambaye kama mwanae akimwomba mkate atampa jiwe? 10 Au akimwomba samaki atampa nyoka? 11 Ikiwa ninyi mlio waovu mnafahamu jinsi ya kuwapa watoto wenu zawadi nzuri, ni mara ngapi zaidi Baba yenu wa mbinguni atawapa vitu vizuri wale wamwombao? 12 Kwa hiyo cho chote ambacho ungependa watu wakutendee, na wewe watendee vivyo hivyo. Hii ndio maana ya sheria ya Musa na Maandiko ya manabii.”

Njia Nyembamba Na Njia Pana

13 “Ingieni kwa kupitia mlango mwembamba; kwa maana mlango mpana na njia rahisi huelekea kwenye maangamizo, na watu wanaopitia huko ni wengi. 14 Lakini mlango mwembamba na njia ngumu huelekea kwenye uzima, na ni wachache tu wanaoiona.”

Manabii Wa Uongo

15 “Jihadharini na manabii wa uongo wanaowajia wakiwa wamevaa ngozi ya kondoo, kumbe ndani ni mbwa mwitu wakali. 16 Mtawatambua kwa matunda yao. Je, unaweza kuchuma zabibu kwenye miiba au tini kwenye michongoma? 17 Vivyo hivyo mti mzuri huzaa matunda mazuri na mti mbaya huzaa matunda mabaya. 18 Mti mzuri hauwezi kuzaa matunda mabaya na mti mbaya hauwezi kuzaa matunda mazuri. 19 Kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa katwa na kutupwa motoni. 20 Hivyo, mtawatambua kwa matunda yao.”

Mfuasi Wa Kweli

21 “Si kila mtu anayesema, ‘Bwana, Bwana,’ ambaye ataingia katika Ufalme wa mbinguni ila ni wale wanaofanya mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. 22 Siku ile itakapofika wengi wata niambia, ‘Bwana, Bwana, hatukutoa unabii na kufukuza pepo kwa jina lako; na kufanya miujiza mingi ya ajabu kwa jina lako?’ 23 Ndipo nitawaambia wazi, ‘Sikuwafahamu kamwe. Ondokeni kwangu ninyi watenda maovu!’

Nyumba Iliyojengwa Kwenye Mwamba

24 “Basi, kila anayesikiliza haya maneno yangu na kuyate keleza, atafanana na mtu mwenye busara aliyejenga nyumba yake kwenye mwamba. 25 Mvua ikanyesha, mafuriko yakaja na upepo uka vuma ukaipiga nyumba hiyo, lakini haikuanguka kwa sababu ili jengwa kwenye msingi imara juu ya mwamba. 26 Na kila anayesikia haya maneno yangu asiyafuate, atafanana na mtu mjinga aliyejenga nyumba yake kwenye mchanga. 27 Mvua ikanyesha, yakatokea mafu riko, na upepo ukavuma ukaipiga hiyo nyumba, nayo ikaanguka kwa kishindo kikubwa.” 28 Na Yesu alipomaliza kusema maneno haya, umati wa watu waliomsikiliza walishangaa sana, 29 kwa sababu alifundisha kama mtu mwenye mamlaka, na si kama walimu wao wa sheria.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

马太福音 7

责人先责己

1“不要论断别人,免得你们被论断。 因为你们怎样论断别人,也必照样被论断;你们用什么尺度衡量别人,也要用什么尺度衡量你们。 为什么你只看见你弟兄眼中的小刺,却看不见自己眼中的大梁呢? 既然你自己眼中有大梁,又怎么能对弟兄说‘让我除去你眼中的小刺’呢? 你这伪君子啊!要先除掉自己眼中的大梁,才能看得清楚,好清除弟兄眼中的小刺。

“不要把圣物给狗,免得狗转过头来咬你们,也不要把珍珠丢在猪前,免得猪践踏了珍珠。

祈求、寻找、叩门

“祈求,就会给你们;寻找,就会寻见;叩门,就会给你们开门。 因为凡祈求的,就得到;寻找的,就寻见;叩门的,就给他开门。

“你们做父亲的,谁会在儿子要饼时给他石头, 10 要鱼时给他毒蛇呢? 11 你们虽然邪恶,尚且知道把好东西给儿女,你们的天父岂不更要把好东西赐给求祂的人吗?

12 “所以,你们希望人怎样待你们,就要怎样待人,这是律法和先知的教导。

辨别与抉择

13 “你们要进窄门,因为通向灭亡的门大,路宽,进去的人也多; 14 但通向永生的门小,路窄,找到的人也少。

15 “你们要提防假先知,他们披着羊皮到你们当中,骨子里却是凶残的狼。 16 你们可以凭他们结的果子认出他们。荆棘怎能结出葡萄呢?蒺藜怎能长出无花果呢? 17 同样,好树结好果子,坏树结坏果子; 18 好树结不出坏果子,坏树也结不出好果子。 19 凡不结好果子的树,都要被砍下来丢在火里。 20 因此,你们可以凭他们结的果子认出他们。 21 并不是所有称呼我‘主啊,主啊’的人都能进天国,只有遵行我天父旨意的人才能进去。 22 在审判那天,很多人会对我说,‘主啊,主啊,我们不是奉你的名传道,奉你的名赶鬼,奉你的名行了许多神迹吗?’ 23 我会清楚地告诉他们,‘我从来不认识你们,你们这些作恶的人走开!’

两种盖房子的人

24 “所以,凡听了我的这些话就去行的人,就像聪明人把房子建在磐石上。 25 任由风吹雨打、洪水冲击,房子仍屹立不倒,因为它建基在磐石上。 26 凡听了我这些话不去行的,就像愚昧人把房子建在沙土上。 27 遇到风吹雨打、洪水冲击,房子就倒塌了,而且倒塌得很厉害。”

28 大家听完耶稣这番教导,都很惊奇, 29 因为祂教导他们时像位有权柄的人,不像他们的律法教师。