Neno: Bibilia Takatifu

1 Timotheo 2

Maagizo Kuhusu Ibada

1Basi, kwanza kabisa, naagiza kwamba dua, sala, maombezi na shukrani zitolewe kwa ajili ya watu wote: kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, ili tupate kuishi maisha ya utulivu na amani, tukimcha Mungu na kuwa wenye heshima kwa kila njia. Jambo hili ni jema na linampendeza Mungu Mwokozi wetu ambaye anapenda watu wote waokolewe na wapate kuijua kweli. Maana kuna Mungu mmoja na mpatanishi mmoja kati ya Mungu na wanadamu, yaani mwanadamu Kristo Yesu, aliyejitoa mwenyewe kuwa fidia kwa ajili ya wote. Yeye ni uthibitisho wa mambo haya, uliotolewa kwa wakati wake. Na hii ndio sababu nilichaguliwa niwe mhubiri na mtume, nasema kweli sisemi uwongo; nilichaguliwa niwe mwalimu wa watu wa mataifa katika imani na kweli.

Kwa hiyo, nataka kila mahali wanaume wasali wakiinua mikono iliyotakaswa pasipo hasira wala mabishano. Kadhalika, nataka wanawake wajipambe kwa heshima na kwa busara. Mavazi yao yawe nadhifu, si kwa kusuka nywele, kujipamba kwa dhahabu, lulu na mavazi ya gharama kubwa, 10 bali kwa matendo mema kama iwapa savyo wanawake wanaokiri kuwa wanamcha Mungu. 11 Mwanamke na ajifunze katika utulivu na unyenyekevu.

12 Simruhusu mwanamke ye yote kufundisha au kuwa na mamlaka juu ya wanaume. Mwanamke anapaswa kukaa kimya. 13 Kwa maana Adamu aliumbwa kwanza kisha Hawa; 14 na Adamu hakudanganywa bali mwanamke alidanganywa akawa mkosaji. 15 Lakini mwanamke ataoko lewa kwa kuzaa, kama ataendelea kudumu katika imani, upendo na utakatifu, pamoja na kujiheshimu.

New International Version - UK

1 Timothy 2

Instructions on worship

1I urge, then, first of all, that petitions, prayers, intercession and thanksgiving be made for all people – for kings and all those in authority, that we may live peaceful and quiet lives in all godliness and holiness. This is good, and pleases God our Saviour, who wants all people to be saved and to come to a knowledge of the truth. For there is one God and one mediator between God and mankind, the man Christ Jesus, who gave himself as a ransom for all people. This has now been witnessed to at the proper time. And for this purpose I was appointed a herald and an apostle – I am telling the truth, I am not lying – and a true and faithful teacher of the Gentiles.

Therefore I want the men everywhere to pray, lifting up holy hands without anger or disputing. I also want the women to dress modestly, with decency and propriety, adorning themselves, not with elaborate hairstyles or gold or pearls or expensive clothes, 10 but with good deeds, appropriate for women who profess to worship God.

11 A woman[a] should learn in quietness and full submission. 12 I do not permit a woman to teach or to assume authority over a man;[b] she must be quiet. 13 For Adam was formed first, then Eve. 14 And Adam was not the one deceived; it was the woman who was deceived and became a sinner. 15 But women[c] will be saved through childbearing – if they continue in faith, love and holiness with propriety.

Footnotes

  1. 1 Timothy 2:11 Or wife; also in verse 12
  2. 1 Timothy 2:12 Or over her husband
  3. 1 Timothy 2:15 Greek she