New Living Translation

Revelation 9

The Fifth Trumpet Brings the First Terror

1Then the fifth angel blew his trumpet, and I saw a star that had fallen to earth from the sky, and he was given the key to the shaft of the bottomless pit.[a] When he opened it, smoke poured out as though from a huge furnace, and the sunlight and air turned dark from the smoke.

Then locusts came from the smoke and descended on the earth, and they were given power to sting like scorpions. They were told not to harm the grass or plants or trees, but only the people who did not have the seal of God on their foreheads. They were told not to kill them but to torture them for five months with pain like the pain of a scorpion sting. In those days people will seek death but will not find it. They will long to die, but death will flee from them!

The locusts looked like horses prepared for battle. They had what looked like gold crowns on their heads, and their faces looked like human faces. They had hair like women’s hair and teeth like the teeth of a lion. They wore armor made of iron, and their wings roared like an army of chariots rushing into battle. 10 They had tails that stung like scorpions, and for five months they had the power to torment people. 11 Their king is the angel from the bottomless pit; his name in Hebrew is Abaddon, and in Greek, Apollyon—the Destroyer.

12 The first terror is past, but look, two more terrors are coming!

The Sixth Trumpet Brings the Second Terror

13 Then the sixth angel blew his trumpet, and I heard a voice speaking from the four horns of the gold altar that stands in the presence of God. 14 And the voice said to the sixth angel who held the trumpet, “Release the four angels who are bound at the great Euphrates River.” 15 Then the four angels who had been prepared for this hour and day and month and year were turned loose to kill one-third of all the people on earth. 16 I heard the size of their army, which was 200 million mounted troops.

17 And in my vision, I saw the horses and the riders sitting on them. The riders wore armor that was fiery red and dark blue and yellow. The horses had heads like lions, and fire and smoke and burning sulfur billowed from their mouths. 18 One-third of all the people on earth were killed by these three plagues—by the fire and smoke and burning sulfur that came from the mouths of the horses. 19 Their power was in their mouths and in their tails. For their tails had heads like snakes, with the power to injure people.

20 But the people who did not die in these plagues still refused to repent of their evil deeds and turn to God. They continued to worship demons and idols made of gold, silver, bronze, stone, and wood—idols that can neither see nor hear nor walk! 21 And they did not repent of their murders or their witchcraft or their sexual immorality or their thefts.

Footnotes

  1. 9:1 Or the abyss, or the underworld; also in 9:11.

Neno: Bibilia Takatifu

Ufunua wa Yohana 9

Tarumbeta Ya Tano

1Kisha malaika wa tano akapiga tarumbeta yake, nikaona nyota iliyokuwa imeanguka kutoka angani hadi ardhini. Nyota hiyo ili pewa ufunguo wa shimo la kuzimu. Alipolifungua hilo shimo, moshi ulitoka ndani yake kama moshi wa tanuru kubwa sana. Jua na anga vilitiwa giza kwa ajili ya ule moshi uliotoka katika shimo hilo. Kisha, katika ule moshi wakatoka nzige wakatua ardhini. Nao wakapewa nguvu kama nguvu ya nge wa duniani. Waliambiwa wasidhuru nyasi za nchi, wala majani, wala mmea au mti wo wote. Bali wawadhuru wale watu wasiokuwa na muhuri wa Mungu kwenye vipaji vya nyuso zao. Waliruhusiwa kuwatesa kwa muda wa miezi mitano lakini wasiwaue. Na uchungu wa kuuma kwao ulikuwa kama uchungu wa mtu anapoumwa na nge. Katika siku hizo watu watata futa kifo lakini hawatakiona; watatamani kufa, lakini kifo kita wakimbia.

Wale nzige walionekana kama farasi waliotayarishwa kwa vita; vichwani mwao kulikuwa na kitu kama taji za dhahabu; na nyuso zao zilikuwa kama za binadamu. Manyoya yao yalifanana kama nywele za wanawake; na meno yao yalikuwa kama meno ya simba. Walikuwa na magamba yaliyofanana na ngao za chuma; na kelele za mabawa yao zilikuwa kama kelele za magari ya farasi yenye farasi wanaokimbia kwenda vitani. 10 Walikuwa na mikia ya kuuma kama nge; nguvu yao ya kutesa watu kwa muda wa miezi mitano ilikuwa katika mikia yao. 11 Walikuwa na mfalme wa kuwatawala, naye ni malaika wa shimo la kuzimu ambaye jina lake kwa Kiebrania ni Aba doni na kwa Kigiriki ni Apolioni.

12 Maafa ya kwanza yamepita; bado mengine mawili yanakuja.

Tarumbeta Ya Sita

13 Malaika wa sita akapiga tarumbeta yake, nami nikasikia sauti ikitoka katika zile pembe nne za madhabahu iliyoko mbele ya Mungu. 14 Sauti hiyo ikamwambia yule malaika wa sita mwenye tar umbeta, “Wafungulie wale malaika wanne waliofungwa kwenye mto mkubwa wa Efrati.” 15 Basi wakafunguliwa wale malaika wanne waliokuwa wamewekwa tayari kwa ajili ya saa hiyo, na siku hiyo na mwezi huo na mwaka huo, wawaue theluthi moja ya wanadamu. 16 Idadi ya majeshi wapandao farasi ilikuwa milioni mia mbili. 17 Na hivi ndivyo nilivyowaona hao farasi na wapanda farasi katika maono yangu: wapanda farasi walivaa ngao vifuani zenye rangi ya moto na samawati na kiberiti. Na vichwa vya farasi hao vilikuwa kama vichwa vya simba; na moto, moshi na kiberiti vili kuwa vinatoka vinywani mwao. 18 Theluthi moja ya wanadamu waliu awa kwa maafa hayo matatu, yaani, moto, moshi na kiberiti, yaliy otoka vinywani mwa hao farasi. 19 Nguvu ya hao farasi ilikuwa vinywani mwao na mikiani mwao; kwa sababu mikia yao ilikuwa kama nyoka wenye vichwa ambavyo vilitumika kuwadhuru watu.

20 Wanadamu waliosalia, ambao hawakuuawa katika maafa hayo, bado walikataa kutubu na kuacha kuabudu vitu walivyotengeneza kwa mikono yao wenyewe. Waliendelea kuabudu pepo, sanamu za dhahabu na za fedha na za shaba na za mawe na za miti, sanamu zisizoweza kuona, kusikia wala kutembea. 21 Wala hawakutubu na kuacha matendo yao ya uuaji, uchawi, uasherati na wizi.