Psalms 75 – NIV & NEN

New International Version

Psalms 75:1-10

Psalm 75In Hebrew texts 75:1-10 is numbered 75:2-11.

For the director of music. To the tune of “Do Not Destroy.” A psalm of Asaph. A song.

1We praise you, God,

we praise you, for your Name is near;

people tell of your wonderful deeds.

2You say, “I choose the appointed time;

it is I who judge with equity.

3When the earth and all its people quake,

it is I who hold its pillars firm.75:3 The Hebrew has Selah (a word of uncertain meaning) here.

4To the arrogant I say, ‘Boast no more,’

and to the wicked, ‘Do not lift up your horns.75:4 Horns here symbolize strength; also in verses 5 and 10.

5Do not lift your horns against heaven;

do not speak so defiantly.’ ”

6No one from the east or the west

or from the desert can exalt themselves.

7It is God who judges:

He brings one down, he exalts another.

8In the hand of the Lord is a cup

full of foaming wine mixed with spices;

he pours it out, and all the wicked of the earth

drink it down to its very dregs.

9As for me, I will declare this forever;

I will sing praise to the God of Jacob,

10who says, “I will cut off the horns of all the wicked,

but the horns of the righteous will be lifted up.”

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 75:1-10

Zaburi 75

Mungu Ni Mwamuzi

Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Usiharibu!” Zaburi ya Asafu. Wimbo.

175:1 Yos 3:5; Za 44:1; 71:16; 77:12; 105:2; 107:8, 15; 145:5, 12, 18Ee Mungu, tunakushukuru,

tunakushukuru wewe,

kwa kuwa jina lako li karibu;

watu husimulia matendo yako ya ajabu.

275:2 Kut 13:10; Za 7:11Unasema, “Ninachagua wakati maalum;

ni mimi nihukumuye kwa haki.

375:3 Ebr 1:3; Isa 24:19; 1Sam 2:8; 2Sam 22:8Wakati dunia na watu wake wote inapotetemeka,

ni mimi ninayezishikilia nguzo zake imara.

475:4 Za 5:5; Zek 1:21; 1Sam 2:3Kwa wale wenye majivuno ninasema,

‘Msijisifu tena,’

kwa wale waovu, ‘Msiinue pembe zenu.

575:5 Ay 15:25Msiinue pembe zenu dhidi ya mbingu;

msiseme kwa shingo zilizonyooshwa.’ ”

6Hakuna yeyote atokaye mashariki wala magharibi

au kutoka jangwani awezaye kumkweza mwanadamu.

775:7 Mwa 16:5; Ufu 18:8; 1Sam 2:7; Ay 5:11; Za 50:6; 58:11; 147:6; Eze 21:26; Dan 2:21; Lk 1:52Bali Mungu ndiye ahukumuye:

Humshusha huyu na kumkweza mwingine.

875:8 Mit 23:30; Isa 51:17; Yer 25:15; Zek 12:2; Ufu 14:10; Ay 21:20Mkononi mwa Bwana kuna kikombe

kilichojaa mvinyo unaotoka povu

uliochanganywa na vikolezo;

huumimina, nao waovu wote wa dunia

hunywa mpaka tone la mwisho.

975:9 Za 40:10; 76:6; 108:1; Mwa 24:12Bali mimi, nitatangaza hili milele;

nitaimba sifa kwa Mungu wa Yakobo.

1075:10 Za 89:17; 92:10; 112:9; 148:14Nitazikatilia mbali pembe za waovu wote,

bali pembe za wenye haki zitainuliwa juu.