2 Chronicles 18 – NIVUK & NEN

New International Version – UK

2 Chronicles 18:1-34

Micaiah prophesies against Ahab

1Now Jehoshaphat had great wealth and honour, and he allied himself with Ahab by marriage. 2Some years later he went down to see Ahab in Samaria. Ahab slaughtered many sheep and cattle for him and the people with him and urged him to attack Ramoth Gilead. 3Ahab king of Israel asked Jehoshaphat king of Judah, ‘Will you go with me against Ramoth Gilead?’

Jehoshaphat replied, ‘I am as you are, and my people as your people; we will join you in the war.’ 4But Jehoshaphat also said to the king of Israel, ‘First seek the counsel of the Lord.’

5So the king of Israel brought together the prophets – four hundred men – and asked them, ‘Shall we go to war against Ramoth Gilead, or shall I not?’

‘Go,’ they answered, ‘for God will give it into the king’s hand.’

6But Jehoshaphat asked, ‘Is there no longer a prophet of the Lord here whom we can enquire of?’

7The king of Israel answered Jehoshaphat, ‘There is still one prophet through whom we can enquire of the Lord, but I hate him because he never prophesies anything good about me, but always bad. He is Micaiah son of Imlah.’

‘The king should not say such a thing,’ Jehoshaphat replied.

8So the king of Israel called one of his officials and said, ‘Bring Micaiah son of Imlah at once.’

9Dressed in their royal robes, the king of Israel and Jehoshaphat king of Judah were sitting on their thrones at the threshing-floor by the entrance of the gate of Samaria, with all the prophets prophesying before them. 10Now Zedekiah son of Kenaanah had made iron horns, and he declared, ‘This is what the Lord says: “With these you will gore the Arameans until they are destroyed.” ’

11All the other prophets were prophesying the same thing. ‘Attack Ramoth Gilead and be victorious,’ they said, ‘for the Lord will give it into the king’s hand.’

12The messenger who had gone to summon Micaiah said to him, ‘Look, the other prophets without exception are predicting success for the king. Let your word agree with theirs, and speak favourably.’

13But Micaiah said, ‘As surely as the Lord lives, I can tell him only what my God says.’

14When he arrived, the king asked him, ‘Micaiah, shall we go to war against Ramoth Gilead, or shall I not?’

‘Attack and be victorious,’ he answered, ‘for they will be given into your hand.’

15The king said to him, ‘How many times must I make you swear to tell me nothing but the truth in the name of the Lord?’

16Then Micaiah answered, ‘I saw all Israel scattered on the hills like sheep without a shepherd, and the Lord said, “These people have no master. Let each one go home in peace.” ’

17The king of Israel said to Jehoshaphat, ‘Didn’t I tell you that he never prophesies anything good about me, but only bad?’

18Micaiah continued, ‘Therefore hear the word of the Lord: I saw the Lord sitting on his throne with all the multitudes of heaven standing on his right and on his left. 19And the Lord said, “Who will entice Ahab king of Israel into attacking Ramoth Gilead and going to his death there?”

‘One suggested this, and another that. 20Finally, a spirit came forward, stood before the Lord and said, “I will entice him.”

‘ “By what means?” the Lord asked.

21‘ “I will go and be a deceiving spirit in the mouths of all his prophets,” he said.

‘ “You will succeed in enticing him,” said the Lord. “Go and do it.”

22‘So now the Lord has put a deceiving spirit in the mouths of these prophets of yours. The Lord has decreed disaster for you.’

23Then Zedekiah son of Kenaanah went up and slapped Micaiah in the face. ‘Which way did the spirit from18:23 Or Spirit of the Lord go when he went from me to speak to you?’ he asked.

24Micaiah replied, ‘You will find out on the day you go to hide in an inner room.’

25The king of Israel then ordered, ‘Take Micaiah and send him back to Amon the ruler of the city and to Joash the king’s son, 26and say, “This is what the king says: put this fellow in prison and give him nothing but bread and water until I return safely.” ’

27Micaiah declared, ‘If you ever return safely, the Lord has not spoken through me.’ Then he added, ‘Mark my words, all you people!’

Ahab killed at Ramoth Gilead

28So the king of Israel and Jehoshaphat king of Judah went up to Ramoth Gilead. 29The king of Israel said to Jehoshaphat, ‘I will enter the battle in disguise, but you wear your royal robes.’ So the king of Israel disguised himself and went into battle.

30Now the king of Aram had ordered his chariot commanders, ‘Do not fight with anyone, small or great, except the king of Israel.’ 31When the chariot commanders saw Jehoshaphat, they thought, ‘This is the king of Israel.’ So they turned to attack him, but Jehoshaphat cried out, and the Lord helped him. God drew them away from him, 32for when the chariot commanders saw that he was not the king of Israel, they stopped pursuing him.

33But someone drew his bow at random and hit the king of Israel between the breastplate and the scale armour. The king told the chariot driver, ‘Wheel round and get me out of the fighting. I’ve been wounded.’ 34All day long the battle raged, and the king of Israel propped himself up in his chariot facing the Arameans until evening. Then at sunset he died.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

2 Nyakati 18:1-34

Mikaya Atoa Unabii Dhidi Ya Ahabu

(1 Wafalme 22:1-28)

118:1 2Nya 17:5; 19:1-3; 21:6; Mhu 5:19; Mit 4:5-8; Za 112:2-9; Kum 8:10, 18; 1Sam 2:7, 30; 1Fal 3:13; 1Tim 4:8; 2Fal 8:18; 2Kor 6:14Basi, Yehoshafati alikuwa na mali nyingi sana na heshima. Naye akafanya urafiki na Ahabu kwa mwanawe kumwoa binti wa Ahabu. 218:2 1Fal 22:2; 2Nya 19:2Baada ya miaka kadhaa akashuka kumtembelea Ahabu huko Samaria. Ahabu akachinja ngʼombe na kondoo wengi kwa ajili yake na watu aliokuwa amefuatana nao. Kisha Ahabu akamshawishi Yehoshafati kukwea pamoja naye ili kuishambulia Ramoth-Gileadi. 3Ahabu mfalme wa Israeli akamuuliza Yehoshafati mfalme wa Yuda, “Je, utakwenda pamoja nami kupigana dhidi ya Ramoth-Gileadi?”

Yehoshafati akamjibu mfalme wa Israeli, “Mimi ni kama wewe, watu wangu ni kama watu wako, farasi wangu ni kama farasi wako. Tutakuwa pamoja nawe vitani.” 418:4 1Sam 23:2-9; Yer 21:2; Eze 20:3; 1Fal 22:5-6; 2Nya 34:26Lakini Yehoshafati pia akamwambia mfalme wa Israeli, “Kwanza tafuta shauri la Bwana.”

518:5 Yer 23:17; Eze 13:3; Mt 23:16-19Kwa hiyo mfalme wa Israeli akawaleta pamoja manabii wanaume wapatao mia nne, akawauliza, “Je, twende vitani dhidi ya Ramoth-Gileadi, au niache?”

Wakajibu, “Naam, nenda kwa kuwa Mungu ataiweka Ramoth-Gileadi mkononi mwa mfalme.”

6Lakini Yehoshafati akauliza, “Je, hayuko nabii wa Bwana hapa ambaye tunaweza kumuuliza?”

7Mfalme wa Israeli akamjibu Yehoshafati, “Bado yupo mtu mmoja ambaye kupitia yeye twaweza kumuuliza shauri la Bwana, lakini namchukia kwa sababu huwa hatabiri jambo lolote jema kunihusu mimi, lakini kila mara hunitabiria mabaya tu. Yeye ni Mikaya mwana wa Imla.”

Yehoshafati akajibu, “Mfalme hapaswi kusema hivyo.”

8Kwa hiyo mfalme wa Israeli akamwita mmoja wa maafisa wake na kusema, “Mlete Mikaya mwana wa Imla mara moja.”

9Wakiwa wamevalia majoho yao ya kifalme, mfalme wa Israeli na Yehoshafati mfalme wa Yuda walikuwa wameketi juu ya viti vyao vya kifalme katika sakafu ya kupuria, kwenye ingilio la lango la Samaria, pamoja na manabii wote wakiwa wakitabiri mbele yao. 10Wakati huu Sedekia mwana wa Kenaana alikuwa ametengeneza pembe za chuma, akatangaza, “Hivi ndivyo Bwana asemavyo, ‘Kwa hizi pembe utawapiga na kuwarudisha Waaramu nyuma mpaka wameangamizwa.’ ”

1118:11 2Nya 22:5Manabii wengine wote walikuwa wanatabiri kitu hicho hicho, wakisema, “Ishambulie Ramoth-Gileadi na uwe mshindi. Kwa kuwa Bwana ataitia mkononi mwa mfalme.”

12Mjumbe aliyekuwa amekwenda kumwita Mikaya akamwambia, “Tazama, manabii wote kama mtu mmoja wanatabiri ushindi kwa mfalme. Neno lako na likubaliane na lao, nawe unene mema kuhusu mfalme.”

1318:13 Hes 22:18-20, 35; 1Fal 22:14; Mdo 20:27; Hes 23:12, 26; 24:13; Yer 23:8; 42:4; Eze 2:7; Mik 2:6-7; 1Kor 11:23; 1The 2:4Lakini Mikaya akasema, “Hakika kama Bwana aishivyo, nitamwambia kile tu Bwana atakachoniambia.”

1418:14 1Fal 18:27; Amo 4:4Alipofika, mfalme akamuuliza, “Mikaya, je, twende vitani dhidi ya Ramoth-Gileadi au niache?”

Akamjibu, “Shambulia na ushinde, kwa kuwa watatiwa mkononi mwako.”

15Mfalme akamwambia, “Je, ni mara ngapi nitakuapisha ili usiniambie kitu chochote ila kweli tu kwa jina la Bwana?”

1618:16 Hes 27:17; Eze 34:5-8Ndipo Mikaya akajibu, “Niliona Israeli wote wametawanyika vilimani kama kondoo wasio na mchungaji, naye Bwana akasema, ‘Watu hawa hawana bwana. Mwache kila mmoja aende nyumbani kwa amani.’ ”

17Mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati, “Sikukuambia kwamba huwa hatabiri jambo lolote jema kunihusu bali mabaya tu?”

1818:18 Dan 7:9; Za 103:20Mikaya akaendelea, “Kwa hiyo lisikie neno la Bwana: Nilimwona Bwana ameketi juu ya kiti chake cha enzi pamoja na jeshi lote la mbinguni likiwa limesimama upande wa kulia na wa kushoto. 19Naye Bwana akasema, ‘Ni nani atakayemshawishi Ahabu, mfalme wa Israeli, ili aishambulie Ramoth-Gileadi na kukiendea kifo chake huko?’

“Mmoja akapendekeza hili na mwingine lile. 2018:20 Ay 1:6; 2The 2:9Mwishoni, roho akajitokeza, akasimama mbele za Bwana na kusema, ‘Nitamshawishi.’

Bwana akauliza, ‘Kwa njia gani?’

2118:21 Zek 13:2; Yn 8:44; Hos 4:12; 1Fal 22:21-22“Akasema, ‘Nitakwenda na kuwa roho ya uongo katika vinywa vya manabii wake wote.’

Bwana akasema, ‘Utafanikiwa katika kumshawishi. Nenda ukafanye hivyo.’

2218:22 Ay 12:16; Isa 19:14; Mt 24:24-25; 2The 2:9-11; Eze 14:9; Yak 1:13“Kwa hiyo sasa Bwana ameweka roho ya kudanganya ndani ya vinywa vya hawa manabii wako wote. Bwana ameamuru maafa kwa ajili yako.”

2318:23 Yer 20:2; Mk 14:65; Mdo 23:2Kisha Sedekia mwana wa Kenaana akatoka na kumpiga Mikaya kofi usoni. Akauliza, “Huyo Roho kutoka kwa Bwana alipita njia gani alipotoka kwangu ili kusema nawe?”

24Mikaya akajibu, “Utagundua siku hiyo utakapokwenda kujificha kwenye chumba cha ndani.”

25Kisha mfalme wa Israeli akaagiza, “Mchukueni na mkamrudishe kwa Amoni mtawala wa mji na kwa Yoashi mwana wa mfalme. 2618:26 1Sam 25:21; 2Nya 16:10; Ebr 11:36; Lk 23:2Mkaseme, ‘Hivi ndivyo asemavyo mfalme: Mwekeni mtu huyu gerezani na asipewe chochote ila mkate na maji mpaka nitakaporudi salama.’ ”

27Mikaya akasema, “Kama utarudi salama, basi Bwana hajanena kupitia kwangu.” Kisha akaongeza kusema, “Zingatieni maneno yangu, enyi watu wote!”

Ahabu Anauawa Huko Ramoth-Gileadi

(1 Wafalme 22:29-35)

28Basi mfalme wa Israeli na Yehoshafati mfalme wa Yuda wakaenda Ramoth-Gileadi. 2918:29 1Sam 28:8; Mit 10:24Mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati, “Nitaingia vitani nikiwa nimejibadilisha, lakini wewe uvae majoho yako ya kifalme.” Kwa hiyo mfalme wa Israeli akajibadilisha na kwenda vitani.

30Wakati huu, mfalme wa Aramu alikuwa amewaagiza majemadari thelathini na wawili wa magari ya vita, “Msipigane na yeyote, mdogo au mkubwa, isipokuwa mfalme wa Israeli.” 3118:31 2Nya 13:14; Mit 13:20; Za 46:1Wakati wale majemadari wa magari ya vita walipomwona Yehoshafati, wakafikiri, “Hakika huyu ndiye mfalme wa Israeli.” Kwa hiyo wakageuka ili wamshambulie, lakini Yehoshafati akapiga kelele, naye Bwana akamsaidia. Mungu akawaondoa kwake, 32wale majemadari wakaona kwamba hakuwa mfalme wa Israeli nao wakaacha kumfuatilia.

33Lakini mtu fulani akavuta upinde pasipo lengo na kumpiga mfalme wa Israeli katikati ya kiungio cha mavazi yake ya chuma, mfalme akamwambia mwendesha gari lake, “Geuza gari na uniondoe mimi katika mapigano, nimejeruhiwa.” 3418:34 2Nya 22:5Vita vikaendelea mchana kutwa, naye mfalme wa Israeli akajitegemeza ndani ya gari lake kuwaelekea Waaramu hadi jioni. Basi jioni yake akafa.