Zechariah 3 – NIV & NEN

New International Version

Zechariah 3:1-10

Clean Garments for the High Priest

1Then he showed me Joshua the high priest standing before the angel of the Lord, and Satan3:1 Hebrew satan means adversary. standing at his right side to accuse him. 2The Lord said to Satan, “The Lord rebuke you, Satan! The Lord, who has chosen Jerusalem, rebuke you! Is not this man a burning stick snatched from the fire?”

3Now Joshua was dressed in filthy clothes as he stood before the angel. 4The angel said to those who were standing before him, “Take off his filthy clothes.”

Then he said to Joshua, “See, I have taken away your sin, and I will put fine garments on you.”

5Then I said, “Put a clean turban on his head.” So they put a clean turban on his head and clothed him, while the angel of the Lord stood by.

6The angel of the Lord gave this charge to Joshua: 7“This is what the Lord Almighty says: ‘If you will walk in obedience to me and keep my requirements, then you will govern my house and have charge of my courts, and I will give you a place among these standing here.

8“ ‘Listen, High Priest Joshua, you and your associates seated before you, who are men symbolic of things to come: I am going to bring my servant, the Branch. 9See, the stone I have set in front of Joshua! There are seven eyes3:9 Or facets on that one stone, and I will engrave an inscription on it,’ says the Lord Almighty, ‘and I will remove the sin of this land in a single day.

10“ ‘In that day each of you will invite your neighbor to sit under your vine and fig tree,’ declares the Lord Almighty.”

Kiswahili Contemporary Version

Zekaria 3:1-10

Maono Ya Nne: Mavazi Safi Kwa Ajili Ya Kuhani Mkuu

13:1 Ezr 2:2; Zek 6:11; 2Sam 24:1; 2Nya 18:21; Za 109:6; Mt 4:10; Ay 1:6; Ufu 12:10Kisha akanionyesha Yoshua,3:1 Yoshua kwa Kiebrania ni Yeshua, maana yake ni Yehova ni wokovu. kuhani mkuu, akiwa amesimama mbele ya malaika wa Bwana, naye Shetani amesimama upande wake wa kuume ili amshtaki. 23:2 Yud 9, 23; Isa 14:1; 7:4; Za 109:31; Mt 4:10; Lk 22:31; Rum 16:20; 8:33; 11:5Bwana akamwambia Shetani, “Bwana akukemee Shetani! Bwana, ambaye ameichagua Yerusalemu, akukemee! Je, mtu huyu siyo kijinga kinachowaka kilichonyakuliwa kwenye moto?”

33:3 Isa 64:6Wakati huu, Yoshua alikuwa amevaa nguo chafu alipokuwa amesimama mbele ya malaika. 43:4 2Sam 12:13; Eze 36:25; Mik 7:18; Mwa 41:42; Za 132:9; Ufu 19:8; Isa 52:1Malaika akawaambia wale waliokuwa wamesimama mbele yake, “Mvueni hizo nguo zake chafu.”

Kisha akamwambia Yoshua, “Tazama, nimeiondoa dhambi yako, nami nitakuvika mavazi ya kitajiri.”

53:5 Kut 29:6Kisha nikasema, “Mvike kilemba kilicho safi kichwani mwake.” Kwa hiyo wakamvika kilemba safi kichwani na kumvika yale mavazi mengine, wakati malaika wa Bwana akiwa amesimama karibu.

6Malaika wa Bwana akamwamuru Yoshua: 73:7 Law 8:35; Kum 17:8-113:7 Eze 44:15-16; 2Nya 23:6; Yer 15:19; Zek 6:15“Hivi ndivyo asemavyo Bwana Mwenye Nguvu Zote: ‘Ikiwa utakwenda katika njia zangu na kushika masharti yangu, basi utaitawala nyumba yangu na kuwa na amri juu ya nyua zangu, nami nitakupa nafasi miongoni mwa hawa wasimamao hapa.

83:8 Kum 28:46; Eze 12:11; Isa 4:2; 49:3“ ‘Sikiliza, ee Yoshua kuhani mkuu, pamoja na wenzako walioketi mbele yako, ambao ni watu walio ishara ya mambo yatakayokuja: Ninakwenda kumleta mtumishi wangu, Tawi. 9Tazama, jiwe nililoliweka mbele ya Yoshua! Kuna macho saba juu ya jiwe lile moja, nami nitachora maandishi juu yake,’ asema Bwana Mwenye Nguvu Zote, ‘nami nitaiondoa dhambi ya nchi hii kwa siku moja.

103:10 Ay 11:18; Hes 16:14; 1Fal 4:25; Mik 4:4“ ‘Katika siku hiyo kila mmoja wenu atamwalika jirani yake akae chini ya mzabibu wake na mtini wake,’ asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.”