New International Version

Revelation 22

Eden Restored

1Then the angel showed me the river of the water of life, as clear as crystal, flowing from the throne of God and of the Lamb down the middle of the great street of the city. On each side of the river stood the tree of life, bearing twelve crops of fruit, yielding its fruit every month. And the leaves of the tree are for the healing of the nations. No longer will there be any curse. The throne of God and of the Lamb will be in the city, and his servants will serve him. They will see his face, and his name will be on their foreheads. There will be no more night. They will not need the light of a lamp or the light of the sun, for the Lord God will give them light. And they will reign for ever and ever.

John and the Angel

The angel said to me, “These words are trustworthy and true. The Lord, the God who inspires the prophets, sent his angel to show his servants the things that must soon take place.”

“Look, I am coming soon! Blessed is the one who keeps the words of the prophecy written in this scroll.”

I, John, am the one who heard and saw these things. And when I had heard and seen them, I fell down to worship at the feet of the angel who had been showing them to me. But he said to me, “Don’t do that! I am a fellow servant with you and with your fellow prophets and with all who keep the words of this scroll. Worship God!”

10 Then he told me, “Do not seal up the words of the prophecy of this scroll, because the time is near. 11 Let the one who does wrong continue to do wrong; let the vile person continue to be vile; let the one who does right continue to do right; and let the holy person continue to be holy.”

Epilogue: Invitation and Warning

12 “Look, I am coming soon! My reward is with me, and I will give to each person according to what they have done. 13 I am the Alpha and the Omega, the First and the Last, the Beginning and the End.

14 “Blessed are those who wash their robes, that they may have the right to the tree of life and may go through the gates into the city. 15 Outside are the dogs, those who practice magic arts, the sexually immoral, the murderers, the idolaters and everyone who loves and practices falsehood.

16 “I, Jesus, have sent my angel to give you[a] this testimony for the churches. I am the Root and the Offspring of David, and the bright Morning Star.”

17 The Spirit and the bride say, “Come!” And let the one who hears say, “Come!” Let the one who is thirsty come; and let the one who wishes take the free gift of the water of life.

18 I warn everyone who hears the words of the prophecy of this scroll: If anyone adds anything to them, God will add to that person the plagues described in this scroll. 19 And if anyone takes words away from this scroll of prophecy, God will take away from that person any share in the tree of life and in the Holy City, which are described in this scroll.

20 He who testifies to these things says, “Yes, I am coming soon.”

Amen. Come, Lord Jesus.

21 The grace of the Lord Jesus be with God’s people. Amen.

Footnotes

  1. Revelation 22:16 The Greek is plural.

Neno: Bibilia Takatifu

Ufunua wa Yohana 22

Mto Wa Maji Ya Uzima

1Kisha yule malaika akanionyesha mto wa maji ya uzima ung’aao kama kioo na kutiririka kutoka kwenye kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana-Kondoo, kupitia katikati ya barabara kuu ya mji huo. Katika pande zote za mto huo kulikuwa na mti wa uzima utoao matunda ya aina kumi na mbili, na kuzaa matunda yake kila mwezi. Majani yake ni ya kuwaponya watu wa mataifa. Katika mji huo hakutakuwa na kitu cho chote kilicholaaniwa, bali kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana-Kondoo kitakuwamo humo na watumishi wake watamwabudu. Watamwona uso wake na jina lake litakuwa kwe nye vipaji vya nyuso zao. Usiku hautakuwapo tena; wala hawata hitaji mwanga wa taa au wa jua, maana Bwana Mungu atakuwa nuru yao, watatawala milele na milele.

Bwana Yesu Anakuja

Kisha yule malaika akaniambia, “Maneno haya ni ya kuami nika na ya kweli. Bwana, Mungu wa roho za manabii, amemtuma mal aika wake kuwaonyesha watumishi wake yale ambayo hayana budi kutokea karibuni. Tazama, ninakuja upesi! Amebarikiwa anayesh ika maneno ya unabii yaliyomo katika kitabu hiki.”

Mimi Yohana, ndiye niliyesikia na kuona mambo haya. Na nil ipokwisha kuyasikia na kuyaona, nilianguka kifudifudi penye miguu ya yule malaika aliyenionyesha mambo hayo, nimwabudu. Lakini yeye akaniambia, “Usifanye hivyo! Mimi pia ni mtumishi pamoja na wewe na ndugu zako manabii na wote wanaoshika maneno ya kitabu hiki. Mwabudu Mungu!”

10 Kisha akaniambia, “Usiyawekee muhuri maneno ya unabii yaliyomo katika kitabu hiki maana wakati umekaribia. 11 Mwache atendaye uovu aendelee kutenda uovu, na aliye mchafu aendelee kuwa mchafu; na atendaye mema aendelee kutenda mema na aliye mta katifu aendelee kuwa mtakatifu.”

12 “Tazama, Ninakuja upesi! Nakuja na tuzo yangu, nimpe tuzo kila mtu kulingana na matendo yake. 13 Mimi ni Alfa na Omega, wa kwanza na wa wisho, Mwanzo na Mwisho.” 14 Wamebari kiwa wanaoosha mavazi yao ili wapate haki ya kushiriki mti wa uzima na wapate kuingia katika ule mji kupitia kwenye milango yake. 15 Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye udanganyifu na kuutenda. 16 Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia mambo haya kwa ajili ya makanisa. Mimi ni Shina na Mzao wa ukoo wa Daudi. Mimi ni Nyota ya asubuhi ing’aayo.”

17 Roho na bibi harusi wanasema, “Njoo!” Na kila mtu asi kiaye na aseme, “Njoo!” Na mtu ye yote mwenye kiu na aje, na kila anayetaka na apokee zawadi ya maji ya uzima bure. .

18 Namwonya kila mtu asikiaye maneno ya unabii yaliyomo katika kitabu hiki: mtu ye yote akiyaongezea cho chote, Mungu atamwongezea maafa yaliyoandikwa katika kitabu hiki. 19 Na kama mtu ye yote akipunguza cho chote katika maneno ya unabii yaliyomo katika kitabu hiki, Mungu atamnyang’anya sehemu yake katika mti wa uzima na katika mji mtakatifu, ambayo yameelezwa katika kitabu hiki.

20 Yeye anayeshuhudia mambo haya anasema, “Hakika ninakuja upesi!” Amina. Njoo, Bwana Yesu!