New International Version

Hebrews 7:1-28

Melchizedek the Priest

1This Melchizedek was king of Salem and priest of God Most High. He met Abraham returning from the defeat of the kings and blessed him, 2and Abraham gave him a tenth of everything. First, the name Melchizedek means “king of righteousness”; then also, “king of Salem” means “king of peace.” 3Without father or mother, without genealogy, without beginning of days or end of life, resembling the Son of God, he remains a priest forever.

4Just think how great he was: Even the patriarch Abraham gave him a tenth of the plunder! 5Now the law requires the descendants of Levi who become priests to collect a tenth from the people—that is, from their fellow Israelites—even though they also are descended from Abraham. 6This man, however, did not trace his descent from Levi, yet he collected a tenth from Abraham and blessed him who had the promises. 7And without doubt the lesser is blessed by the greater. 8In the one case, the tenth is collected by people who die; but in the other case, by him who is declared to be living. 9One might even say that Levi, who collects the tenth, paid the tenth through Abraham, 10because when Melchizedek met Abraham, Levi was still in the body of his ancestor.

Jesus Like Melchizedek

11If perfection could have been attained through the Levitical priesthood—and indeed the law given to the people established that priesthood—why was there still need for another priest to come, one in the order of Melchizedek, not in the order of Aaron? 12For when the priesthood is changed, the law must be changed also. 13He of whom these things are said belonged to a different tribe, and no one from that tribe has ever served at the altar. 14For it is clear that our Lord descended from Judah, and in regard to that tribe Moses said nothing about priests. 15And what we have said is even more clear if another priest like Melchizedek appears, 16one who has become a priest not on the basis of a regulation as to his ancestry but on the basis of the power of an indestructible life. 17For it is declared:

“You are a priest forever,

in the order of Melchizedek.”7:17 Psalm 110:4

18The former regulation is set aside because it was weak and useless 19(for the law made nothing perfect), and a better hope is introduced, by which we draw near to God.

20And it was not without an oath! Others became priests without any oath, 21but he became a priest with an oath when God said to him:

“The Lord has sworn

and will not change his mind:

‘You are a priest forever.’ ”7:21 Psalm 110:4

22Because of this oath, Jesus has become the guarantor of a better covenant.

23Now there have been many of those priests, since death prevented them from continuing in office; 24but because Jesus lives forever, he has a permanent priesthood. 25Therefore he is able to save completely7:25 Or forever those who come to God through him, because he always lives to intercede for them.

26Such a high priest truly meets our need—one who is holy, blameless, pure, set apart from sinners, exalted above the heavens. 27Unlike the other high priests, he does not need to offer sacrifices day after day, first for his own sins, and then for the sins of the people. He sacrificed for their sins once for all when he offered himself. 28For the law appoints as high priests men in all their weakness; but the oath, which came after the law, appointed the Son, who has been made perfect forever.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Waebrania 7:1-28

Kuhani Melkizedeki

17:1 Za 76:2; Mk 5:7; Ebr 7:6; Mwa 14:18-20Kwa kuwa huyu Melkizedeki alikuwa mfalme wa Salemu na kuhani wa Mungu Aliye Juu Sana. Alipokutana na Abrahamu akirudi kutoka kuwashinda hao wafalme, Melkizedeki alimbariki, 2naye Abrahamu alimpa sehemu ya kumi7:2 Sehemu ya kumi mahali pengine huitwa fungu la kumi au zaka; sehemu ya kumi ya pato hutolewa kwa Mungu. ya kila kitu. Kwanza, jina hilo Melkizedeki maana yake ni “mfalme wa haki.” Na pia “mfalme wa Salemu” maana yake ni “mfalme wa amani.” 37:3 Ebr 7:6; Mt 4:3; Za 110:4Hana Baba wala mama, hana ukoo, hana mwanzo wala mwisho wa siku zake. Kama Mwana wa Mungu, yeye adumu akiwa kuhani milele.

47:4 Mwa 14:20; Mdo 2:29Tazama jinsi alivyokuwa mkuu: Hata Abrahamu, baba yetu mkuu, alimpa sehemu ya kumi ya nyara zake. 57:5 Hes 18:21, 26Basi sheria inawaagiza wana wa Lawi ambao hufanyika makuhani kupokea sehemu ya kumi kutoka kwa watu ambao ni ndugu zao, ingawa ndugu zao ni wazao wa Abrahamu. 67:6 Mwa 14:19, 20; Rum 4:13Huyu Melkizedeki, ingawa hakufuatia ukoo wake kutoka kwa Lawi, lakini alipokea sehemu ya kumi kutoka kwa Abrahamu na kumbariki yeye aliyekuwa na zile ahadi. 7Wala hakuna shaka kwamba mdogo hubarikiwa na aliye mkuu kumliko yeye. 87:8 Ebr 5:6; 6:20Kwa upande mmoja, sehemu ya kumi hupokelewa na wale ambao hupatikana na kufa; lakini kwa upande mwingine hupokelewa na yeye ambaye hushuhudiwa kuwa yu hai. 9Mtu anaweza hata kusema kwamba Lawi, ambaye hupokea sehemu ya kumi, alitoa hiyo sehemu ya kumi kupitia kwa Abrahamu, 10kwa sababu Melkizedeki alipokutana na Abrahamu, Lawi alikuwa bado katika viuno vya baba yake wa zamani.7:10 Yaani, alikuwa hajazaliwa.

Yesu Mfano Wa Melkizedeki

117:11 Ebr 7:18-19; 8:7; 10:1; 7:17; 5:6; Gal 2:21Kama ukamilifu ungeweza kupatikana kwa njia ya ukuhani wa Walawi (kwa kuwa katika msingi huo, sheria ilitolewa kwa watu), kwa nini basi imekuwepo haja ya kuja kuhani mwingine: kuhani kwa mfano wa Melkizedeki, wala si kwa mfano wa Aroni? 12Kwa kuwa yanapotokea mabadiliko ya ukuhani, pia lazima yawepo mabadiliko ya sheria. 137:13 Ebr 7:11, 14Yeye ambaye mambo haya yanasemwa alikuwa wa kabila lingine, na hakuna mtu wa kabila hilo aliyewahi kuhudumu katika madhabahu. 147:14 Isa 11:1; Mt 1:3; 2:6; Lk 3:33; Ufu 5:5Kwa maana ni dhahiri kwamba Bwana wetu alitoka katika uzao wa Yuda, tena kuhusu kabila hilo Mose hakusema lolote kwa habari za makuhani. 15Tena hayo tuliyosema yako wazi zaidi kama akitokea kuhani mwingine kama Melkizedeki, 16yeye ambaye amefanyika kuhani si kwa misingi ya sheria kama ilivyokuwa kwa baba zake, bali kwa misingi ya uwezo wa uzima usioharibika. 177:17 Za 110:4; Ebr 7:21; 5:6, 10; 6:20Kwa maana imeshuhudiwa kwamba:

“Wewe ni kuhani milele,

kwa mfano wa Melkizedeki.”

187:18 Rum 8:3; Gal 4:9Kwa upande mmoja, ile amri ya mwanzo isiyofaa na dhaifu imebatilishwa 197:19 Ebr 7:11; 9:9; 10:1; Rum 3:20; 7:7, 8; Gal 3:21; Yak 4:8(kwa maana sheria haikufanya kitu chochote kuwa kikamilifu). Kwa upande mwingine, tumeletewa tumaini lililo bora zaidi ambalo linatuleta karibu na Mungu.

20Nalo tumaini hilo halikutolewa pasipo kiapo! Wengine walikuwa makuhani pasipo kiapo chochote, 217:21 Za 110:4; Hes 23:19; 1Sam 15:29; Mal 3:6; Rum 1:29; Ebr 5:6lakini Yesu alifanywa kuhani kwa kiapo wakati Mungu alimwambia:

Bwana ameapa

naye hatabadilisha mawazo yake:

‘Wewe ni kuhani milele.’ ”

227:22 Ebr 8:6; 9:15; 12:24; Lk 22:20Kwa ajili ya kiapo hiki, Yesu amekuwa mdhamini wa agano lililo bora zaidi.

23Basi pamekuwepo na makuhani wengi wa aina hiyo, kwa kuwa kifo kiliwazuia kuendelea na huduma yao ya ukuhani. 247:24 Ebr 7:28Lakini kwa sababu Yesu anaishi milele, anao ukuhani wa kudumu. 257:25 Rum 11:14; 8:34; Ebr 7:19; 1Tim 2:5; 1Yn 2:1Kwa hiyo anaweza kuwaokoa kabisa wale wanaomjia Mungu kupitia kwake, kwa sababu yeye adumu daima kuomba kwa ajili yao.

267:26 Ebr 4:15; 8:1; Efe 1:20; 4:10; 2Kor 5:21Kwa kuwa ilitupasa tuwe na Kuhani Mkuu wa namna hii, yaani, aliye mtakatifu, asiye na lawama, asiye na dosari, aliyetengwa na wenye dhambi na kuinuliwa juu ya mbingu. 277:27 Ebr 5:1, 3; Rum 6:10; Ebr 9:12, 26, 28; 10:10; 1Pet 3:18; Efe 5:2Yeye hahitaji kutoa dhabihu siku kwa siku kwa ajili ya dhambi, kwanza kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe, kisha kwa ajili ya dhambi za watu kama wale makuhani wakuu wengine. Yeye alitoa dhabihu kwa ajili ya dhambi zao mara moja tu, alipojitoa mwenyewe. 287:28 Ebr 5:2; 1:2; 2:10Kwa kuwa sheria huwaweka makuhani wakuu watu ambao ni dhaifu; lakini lile neno la kiapo, lililokuja baada ya sheria, lilimweka Mwana, ambaye amefanywa kuwa mkamilifu milele.