New International Version

Hebrews 3:1-19

Jesus Greater Than Moses

1Therefore, holy brothers and sisters, who share in the heavenly calling, fix your thoughts on Jesus, whom we acknowledge as our apostle and high priest. 2He was faithful to the one who appointed him, just as Moses was faithful in all God’s house. 3Jesus has been found worthy of greater honor than Moses, just as the builder of a house has greater honor than the house itself. 4For every house is built by someone, but God is the builder of everything. 5“Moses was faithful as a servant in all God’s house,”3:5 Num. 12:7 bearing witness to what would be spoken by God in the future. 6But Christ is faithful as the Son over God’s house. And we are his house, if indeed we hold firmly to our confidence and the hope in which we glory.

Warning Against Unbelief

7So, as the Holy Spirit says:

“Today, if you hear his voice,

8do not harden your hearts

as you did in the rebellion,

during the time of testing in the wilderness,

9where your ancestors tested and tried me,

though for forty years they saw what I did.

10That is why I was angry with that generation;

I said, ‘Their hearts are always going astray,

and they have not known my ways.’

11So I declared on oath in my anger,

‘They shall never enter my rest.’ ”3:11 Psalm 95:7-11

12See to it, brothers and sisters, that none of you has a sinful, unbelieving heart that turns away from the living God. 13But encourage one another daily, as long as it is called “Today,” so that none of you may be hardened by sin’s deceitfulness. 14We have come to share in Christ, if indeed we hold our original conviction firmly to the very end. 15As has just been said:

“Today, if you hear his voice,

do not harden your hearts

as you did in the rebellion.”3:15 Psalm 95:7,8

16Who were they who heard and rebelled? Were they not all those Moses led out of Egypt? 17And with whom was he angry for forty years? Was it not with those who sinned, whose bodies perished in the wilderness? 18And to whom did God swear that they would never enter his rest if not to those who disobeyed? 19So we see that they were not able to enter, because of their unbelief.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Waebrania 3:1-19

Yesu Ni Mkuu Kuliko Mose

13:1 Ebr 2:11; Rum 8:28; 2:17; 1Tim 6:12; Ebr 4:14; 10:23Kwa hiyo ndugu watakatifu, mnaoshiriki mwito wa mbinguni, mtafakarini Yesu, mtume na Kuhani Mkuu wa ukiri wetu. 23:2 Hes 12:7; Ebr 3:5Alikuwa mwaminifu kwa yeye aliyemweka, kama vile Mose alivyokuwa mwaminifu katika nyumba yote ya Mungu. 33:3 Kum 34:12; Zek 6:12; Mt 16:18Yesu ameonekana anastahili heshima kubwa kuliko Mose, kama vile mjenzi wa nyumba alivyo wa heshima kubwa kuliko nyumba yenyewe. 43:4 Efe 2:10; 3:9; Ebr 1:2; Mwa 1:1Kwa kuwa kila nyumba hujengwa na mtu fulani, lakini Mungu ni mjenzi wa kila kitu. 53:5 Kut 14:31; Ebr 3:2; Hes 12:7; Kum 3:24; 8:15; 18:9; Yos 1:2; 8:31Basi Mose kama mtumishi alikuwa mwaminifu katika nyumba yote ya Mungu, akishuhudia kwa yale ambayo yangetamkwa baadaye. 63:6 Ebr 1:2; 6:11, 18, 19; 7:19; 11:1; 1Kor 3:16; 1Tim 3:15; Rum 11:22; 5:2; Hes 4:14Lakini Kristo ni mwaminifu kama Mwana katika nyumba ya Mungu. Sisi ndio nyumba yake, kama tutashikilia sana ujasiri wetu na tumaini tunalojivunia.

Onyo Dhidi Ya Kutokuamini

73:7 Mdo 28:25; Ebr 9:8; 10:15Kwa hiyo, kama Roho Mtakatifu asemavyo:

“Leo, kama mkiisikia sauti yake,

83:8 Ebr 3:15; 4:7msiifanye mioyo yenu migumu,

kama mlivyofanya katika uasi,

wakati ule wa kujaribiwa jangwani,

93:9 Hes 14:33; Kum 1:3; Mdo 7:36ambapo baba zenu walinijaribu na kunipima

ingawa kwa miaka arobaini

walikuwa wameyaona matendo yangu.

10Hiyo ndiyo sababu nilikasirikia kizazi kile,

nami nikasema, ‘Siku zote mioyo yao imepotoka,

nao hawajazijua njia zangu.’

113:11 Kum 1:34, 35; Ebr 4:3, 5; Za 95:7-11Hivyo nikatangaza kwa kiapo katika hasira yangu,

‘Kamwe hawataingia rahani mwangu.’ ”

123:12 Mt 16:16Ndugu zangu, angalieni, asiwepo miongoni mwenu mtu mwenye moyo mwovu usioamini, unaojitenga na Mungu aliye hai. 133:13 Ebr 10:24, 25; Yer 17:9; Efe 4:22Lakini mtiane moyo mtu na mwenzake kila siku, maadamu iitwapo Leo, ili asiwepo hata mmoja wenu mwenye kufanywa mgumu kwa udanganyifu wa dhambi. 143:14 Efe 3:12; Ebr 3:6Kwa kuwa tumekuwa washiriki wa Kristo, kama tukishikamana tu kwa uthabiti na tumaini letu la kwanza hadi mwisho. 153:15 Za 95:7, 8; Ebr 4:7; 3:7, 8Kama ilivyonenwa:

“Leo, kama mkiisikia sauti yake,

msiifanye mioyo yenu migumu

kama mlivyofanya wakati wa kuasi.”

16Basi ni nani waliosikia lakini bado wakaasi? Je, si wale wote waliotoka Misri wakiongozwa na Mose? 17Lakini ni nani aliowakasirikia miaka arobaini? Je, si wale waliofanya dhambi ambao miili yao ilianguka jangwani? 18Ni nani hao ambao Mungu aliapa kuwa kamwe hawataingia rahani mwake isipokuwa ni wale waliokataa kutii? 19Hivyo tunaona kwamba hawakuweza kuingia kwa sababu ya kutokuamini kwao.