Zekaria 7 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version

Zekaria 7:1-14

Haki Na Rehema, Sio Kufunga

17:1 Ezr 5:1; Neh 1:1Katika mwaka wa nne wa utawala wa Mfalme Dario, neno la Bwana lilimjia Zekaria siku ya nne ya mwezi wa tisa, mwezi wa Kisleu. 27:2 Yer 26:19; Zek 8:21; Hag 2:10-14Watu wa Betheli walikuwa wamemtuma Shareza na Regem-Meleki pamoja na watu wao, kumsihi Bwana 37:3 Zek 12:12-14; 2Fal 25:9; Yer 52:12-14; Kum 17:9; Mal 2:7kwa kuwauliza makuhani wa nyumba ya Bwana Mwenye Nguvu Zote na manabii, “Je, imempasa kuomboleza na kufunga katika mwezi wa tano, kama ambavyo nimekuwa nikifanya kwa miaka mingi?”

4Kisha neno la Bwana Mwenye Nguvu Zote likanijia kusema: 57:5 Isa 58:5; 2Fal 25:25; Dan 9:2; Zek 1:12; Mt 6:16; Rum 14:6“Waulize watu wote wa nchi na makuhani, ‘Je, mlipofunga na kuomboleza katika mwezi wa tano na wa saba kwa miaka sabini iliyopita, mlifunga kweli kwa ajili yangu? 67:6 Isa 43:23Na mlipokuwa mkila na kunywa, je, hamkuwa mnasherehekea kwa ajili ya nafsi zenu? 77:7 Isa 1:11-20; Yer 22:21; 17:26; 44:4-5Je, haya sio maneno ya Bwana aliyosema kupitia manabii waliotangulia, wakati Yerusalemu pamoja na miji inayoizunguka ilipokuwa katika hali ya utulivu na ya mafanikio, wakati Negebu na Shefala zikiwa zimekaliwa na watu?’ ”

8Neno la Bwana likamjia tena Zekaria: 97:9 Yer 22:3; 42:5; Zek 8:16; Kum 22:1“Hivi ndivyo asemavyo Bwana Mwenye Nguvu Zote: ‘Fanyeni hukumu za haki, onyesheni rehema na huruma ninyi kwa ninyi. 107:10 Yer 49:11; Kut 22:21-22; Law 25:17; Isa 1:23; Ay 35:8; Eze 45:9; Mik 6:8Msimwonee mjane wala yatima, mgeni wala maskini. Msiwaziane mabaya mioyoni mwenu ninyi kwa ninyi.’

117:11 Isa 9:9; Yer 32:33; 11:10; 17:23; 8:5; Eze 5:6“Lakini wakakataa kusikiliza, wakanipa kisogo kwa ukaidi na kuziba masikio yao. 127:12 Yer 5:3; 17:1; 42:21; Eze 11:19; Neh 9:29; Dan 9:12Wakaifanya mioyo yao migumu kama jiwe gumu na hawakuisikiliza sheria au maneno ambayo Bwana Mwenye Nguvu Zote aliyatuma kwa njia ya Roho wake kupitia manabii waliotangulia. Kwa hiyo Bwana Mwenye Nguvu Zote alikasirika sana.

137:13 Yer 7:27; 11:11; 14:12; Mit 1:28; Isa 1:15; Mao 3:44; Eze 20:31“ ‘Wakati nilipoita, hawakusikiliza, kwa hiyo walipoita, sikusikiliza,’ asema Bwana Mwenye Nguvu Zote. 147:14 Kum 4:27; 28:64-67; Law 26:33; Yer 7:34; 23:19; 44:6; Za 44:11; Isa 33:8; Eze 12:19‘Niliwatawanya kwa upepo wa kisulisuli miongoni mwa mataifa yote, mahali ambapo walikuwa wageni. Nchi ikaachwa ukiwa nyuma yao kiasi kwamba hakuna aliyeweza kuingia au kutoka. Hivi ndivyo walivyoifanya ile nchi iliyokuwa imependeza kuwa ukiwa.’ ”

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

撒迦利亚书 7:1-14

呼吁公义和怜悯

1大流士王执政第四年九月,即基斯流月四日,耶和华的话传给了撒迦利亚2那时,伯特利人差遣沙利色利坚米勒及其随从去向耶和华求恩。 3他们问万军之耶和华殿里的祭司和先知:“我们还要照多年的惯例在五月哀伤、禁食吗?”

4万军之耶和华对我说: 5“你要对境内的民众和祭司说,‘这七十年来,你们在五月和七月禁食、哀伤,难道真的是为了我吗? 6你们吃喝,难道不是为自己吃、为自己喝吗? 7这些岂不是耶和华借从前的先知所宣告的吗?当时耶路撒冷和周围的城邑人口兴盛、繁荣,南地和丘陵都有人居住。’”

8耶和华又对撒迦利亚说: 9“万军之耶和华曾对你们的祖先说,‘要秉公行义,彼此以慈爱和怜悯相待。 10不可欺压寡妇、孤儿、寄居者和穷人,不可设阴谋彼此相害。’ 11他们却不理会,顽梗地背过身去,充耳不闻, 12心如铁石,不遵从律法,也不遵从万军之耶和华借着祂的灵指示从前的先知所说的话。因此,万军之耶和华非常愤怒。 13祂说,‘我曾呼唤他们,他们不听;将来他们呼求我,我也不听。 14我要用旋风把他们吹散到陌生的万国中,使他们的土地荒凉、杳无人迹,因为他们使美好的土地一片荒凉。’”