Zekaria 2 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zekaria 2:1-13

Maono Ya Tatu: Mtu Mwenye Kamba Ya Kupimia

1Kisha nikatazama juu: pale mbele yangu alikuwepo mtu mwenye kamba ya kupimia mkononi mwake! 22:2 Eze 40:3; Zek 1:16; Ufu 21:15Nikamuuliza, “Unakwenda wapi?”

Akanijibu, “Kupima Yerusalemu, kupata urefu na upana wake.”

3Kisha malaika aliyekuwa akizungumza nami akaondoka, malaika mwingine akaja kukutana naye 42:4 Eze 38:11; Isa 49:20; Yer 30:19; 33:22; Zek 14:11; Eze 36:10na kumwambia: “Kimbia, umwambie yule kijana, ‘Yerusalemu utakuwa mji usio na kuta kwa sababu ya wingi wa watu na mifugo iliyomo. 52:5 Isa 10:17; 11:10; 24:23; 26:1; Eze 38:14; 42:20; Za 46:5; 85:9; 125:2; Ufu 21:23; Isa 4:5Mimi mwenyewe nitakuwa ukuta wa moto kuuzunguka,’ asema Bwana, ‘nami nitakuwa utukufu wake ndani yake.’

62:6 Za 44:11; Eze 17:21; 37:9; Mt 24:31; Mk 13:27; Kum 28:64“Njooni! Njooni! Kimbieni mtoke katika nchi ya kaskazini,” asema Bwana, “Kwa kuwa nimewatawanya kwenye pande nne za mbingu,” asema Bwana.

72:7 Isa 42:7; 48:20; Yer 3:18“Njoo, ee Sayuni! Kimbia, wewe ukaaye ndani ya Binti Babeli!” 82:8 Kum 32:10; 2The 1:6Kwa kuwa hivi ndivyo asemavyo Bwana Mwenye Nguvu Zote: “Baada ya yeye kuniheshimu na kunituma mimi dhidi ya mataifa yaliyokuteka nyara, kwa kuwa yeyote awagusaye ninyi, anaigusa mboni ya jicho lake, 92:9 Isa 14:2; 48:16; Yer 12:14; Hab 2:8; Zek 4:9; 6:15hakika nitauinua mkono wangu dhidi yao ili watumwa wao wawateke nyara. Ndipo mtakapojua ya kwamba Bwana Mwenye Nguvu Zote amenituma.

102:10 Sef 3:14; Isa 23:12; Kut 25:8; Hes 23:21; Law 26:12; Zek 8:3; 9:9; Ufu 21:3; 2Kor 6:16“Piga kelele na ufurahie, ee Binti Sayuni, kwa maana ninakuja, nami nitaishi miongoni mwenu,” asema Bwana. 112:11 Yer 23:7; Mik 4:2; Zek 8:8, 20-22; Isa 2:2-3; Kut 12:49; Eze 33:33“Mataifa mengi yataunganishwa na Bwana siku hiyo, nao watakuwa watu wangu. Nitaishi miongoni mwenu nanyi mtajua kwamba Bwana Mwenye Nguvu Zote amenituma kwenu. 122:12 Kut 34:9; Za 33:12; Yer 10:16; 40:5; Kum 12:5; Isa 14:1; Kum 32:9Bwana atairithi Yuda kama fungu lake katika nchi takatifu na atachagua tena Yerusalemu. 132:13 Kut 14:14; Isa 41:1; Kum 26:15; Za 46:10; Hab 2:20; Rum 3:19Tulieni mbele za Bwana, enyi watu wote, kwa sababu ameinuka kutoka makao yake matakatifu.”