Zekaria 13 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zekaria 13:1-9

Kutakaswa Dhambi

113:1 Yer 17:13; Law 16:30; Za 51:2; Ebr 9:14; Isa 1:16-17; Yn 1:29; 1Kor 6:11; 1Pet 1:19; 1Yn 1:7“Katika siku hiyo, chemchemi itafunguliwa kwa nyumba ya Daudi na wakazi wa Yerusalemu, kuwatakasa dhambi na unajisi.

213:2 Yer 43:12; 23:14-15; Eze 6:6; 36:25; Hos 2:17; Mik 5:13; 1Fal 22:22; Kut 23:13; 2Pet 2:1“Katika siku hiyo, nitayakatilia mbali majina ya sanamu kutoka nchi, nayo hayatakumbukwa tena,” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote. “Nitaondoa manabii wao pamoja na roho ya uchafu katika nchi. 313:3 Yer 28:16; 23:34; Kum 13:6-11; 18:20; Neh 6:14; Eze 14:9Ikiwa yupo yeyote atakayeendelea kutabiri, baba yake na mama yake waliomzaa watamwambia, ‘Ni lazima ufe, kwa sababu umesema uongo kwa jina la Bwana.’ Atakapotabiri, wazazi wake mwenyewe watampasua tumbo.

413:4 Yer 6:15; Mt 3:5; 1Fal 18:7; Isa 20:2; Eze 12:24; Mik 3:6-7“Katika siku hiyo, kila nabii ataaibika kwa maono ya unabii wake. Hatavaa vazi la kinabii la nywele ili apate kudanganya watu. 513:5 Amo 7:14Atasema, ‘Mimi sio nabii. Mimi ni mkulima; ardhi imekuwa kazi yangu tangu ujana wangu.’ 6Ikiwa mtu atamuuliza, ‘Majeraha haya yaliyo mwilini mwako ni ya nini?’ Atajibu, ‘Ni majeraha niliyoyapata katika nyumba ya rafiki zangu.’

Mchungaji Apigwa, Nao Kondoo Watawanyika

713:7 Isa 34:5; 40:11; 53:4; Yer 47:6; Eze 37:24; 2Sam 17:2; Mk 4:27; Ebr 13:20; Yn 10:20; 1:29; Mk 14:27“Amka, ee upanga, dhidi ya mchungaji wangu,

dhidi ya mtu aliye karibu nami!”

asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.

“Mpige mchungaji,

nao kondoo watatawanyika,

nami nitageuza mkono wangu

dhidi ya walio wadogo,

813:8 Eze 5:2-4, 12; Zek 14:2; Rum 11:5katika nchi yote,” asema Bwana,

“theluthi mbili watapigwa na kuangamia;

hata hivyo theluthi moja watabaki ndani yake.

913:9 Isa 4:4; 33:14; 30:16; 44:5; Mal 3:2; Za 12:6; 50:15; 86:7; Dan 11:35; 1Pet 1:6-7; Ay 6:29; Yer 6:27; 29:12; 30:22; Law 26:16; Eze 20:38; Isa 48:10; Za 66:10Hii theluthi moja nitaileta katika moto;

nitawasafisha kama fedha isafishwavyo

na kuwajaribu kama dhahabu.

Wataliitia Jina langu

nami nitawajibu;

nitasema, ‘Hawa ni watu wangu,’

nao watasema, ‘Bwana ni Mungu wetu.’ ”