Zekaria 11 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version

Zekaria 11:1-17

111:1 Eze 31:3; 2Nya 36:19; Zek 12:6Fungua milango yako, ee Lebanoni,

ili moto uteketeze mierezi yako!

211:2 Isa 2:13; 32:19; 10:34Piga yowe, ee mti wa msunobari,

kwa kuwa mwerezi umeanguka;

miti ya fahari imeharibiwa!

Piga yowe, enyi mialoni ya Bashani,

msitu mnene umefyekwa!

311:3 Isa 5:29; Yer 2:15; 50:44; Eze 19:9Sikiliza yowe la wachungaji;

malisho yao manono yameangamizwa!

Sikia ngurumo za simba;

kichaka kilichostawi sana

cha Yordani kimeharibiwa!

Wachungaji Wawili Wa Kondoo

411:4 Yer 25:34Hili ndilo asemalo Bwana Mungu wangu: “Lilishe kundi lililokusudiwa kuchinjwa. 511:5 Yer 50:7; Eze 34:2-3; Kum 29:19; Yer 2:3; Hos 12:8; Yn 16:2; 1Tim 6:9; 2Pet 2:3Wanunuzi wake huwachinja na kuondoka pasipo kuadhibiwa. Wale wanaowauza husema, ‘Bwana asifiwe, mimi ni tajiri!’ Wachungaji wao wenyewe hawawahurumii. 611:6 Zek 14:13; Isa 9:19-21; Yer 13:14; Mao 2:21; 5:8; Mik 5:8; 7:2-6Kwa kuwa sitawahurumia tena watu wa nchi,” asema Bwana. “Nitawakabidhi kila mtu mkononi mwa jirani yake na mfalme wake. Wataitenda jeuri nchi, nami sitawaokoa kutoka mikononi mwao.”

711:7 Yer 25:34; Sef 3:12; Mt 11:5Kwa hiyo nikalilisha kundi lililotiwa alama kwa kuchinjwa, hasa kundi lililoonewa sana. Kisha nikachukua fimbo mbili, moja nikaiita Fadhili na nyingine Umoja, nami nikalilisha kundi. 811:8 Eze 14:5; Hos 5:7Katika mwezi mmoja nikawaondoa wachungaji watatu.

Kundi la kondoo likanichukia, nami nikachoshwa nao, 911:9 Yer 43:11; 15:2; Isa 9:20nikasema, “Sitakuwa mchungaji wenu. Waache wanaokufa wafe na wanaoangamia waangamie. Wale waliobakia kila mmoja na ale nyama ya mwenzake.”

1011:10 Za 89:39; Yer 14:21Kisha nikachukua fimbo yangu inayoitwa Fadhili nikaivunja, kutangua Agano nililofanya na mataifa yote. 11Likatanguka siku hiyo, kwa hiyo wale waliodhurika katika kundi, waliokuwa wakiniangalia wakajua kuwa hilo lilikuwa neno la Bwana.

1211:12 Mwa 23:16; Mt 26:15; Kut 21:32Nikawaambia, “Mkiona kuwa ni vyema, nipeni ujira wangu, la sivyo, basi msinipe.” Kwa hiyo wakanilipa vipande thelathini vya fedha.

1311:13 Kut 21:32; Mt 27:9-10; Mdo 1:18-19Naye Bwana akaniambia, “Mtupie mfinyanzi,” hiyo bei nzuri waliyonithaminia! Kwa hiyo nikachukua hivyo vipande thelathini vya fedha na kumtupia huyo mfinyanzi katika nyumba ya Bwana.

14Kisha nikaivunja fimbo yangu ya pili iitwayo Umoja, kuvunja undugu kati ya Yuda na Israeli!

15Kisha Bwana akaniambia, “Vitwae tena vifaa vya mchungaji mpumbavu. 16Kwa maana ninakwenda kumwinua mchungaji juu ya nchi ambaye hatamjali aliyepotea, wala kuwatafuta wale wachanga au kuwaponya waliojeruhiwa, wala kuwalisha wenye afya, lakini atakula nyama ya kondoo wanono na kuzirarua kwato zao.

1711:17 Yer 23:1; Eze 30:21-22; Isa 13:1; Yn 10:12; Mik 3:6“Ole wa mchungaji asiyefaa,

anayeliacha kundi!

Upanga na uupige mkono wake na jicho lake la kuume!

Mkono wake na unyauke kabisa,

jicho lake la kuume lipofuke kabisa!”

Chinese Contemporary Bible 2023 (Traditional)

撒迦利亞書 11:1-17

羊群必遭殺戮

1黎巴嫩啊,打開你的門吧,

好讓火焰吞噬你的香柏樹。

2松樹啊,哀號吧,

因為香柏樹已經倒下,

挺拔的樹木已被毀壞。

巴珊的橡樹啊,哀號吧,

因為茂密的樹林已被砍倒。

3聽啊,牧人在哀號,

因為他們肥美的草場已被毀壞。

聽啊,獅子在吼叫,

因為約旦河畔的叢林已被毀壞。

4我的上帝耶和華說:「你去牧養這群待宰的羊。 5買羊的宰羊卻不受懲罰,賣羊的說,『耶和華當受稱頌!我發財了。』牠們的牧人毫不憐憫牠們。 6我不再憐憫這地方的居民,我要使他們落在鄰人及其君王手中,任這地方被摧毀,必不從敵人手中拯救他們。這是耶和華說的。」

7於是,我牧養這群最困苦的待宰之羊。我拿了兩根杖,一根叫「恩惠」,一根叫「聯合」,開始牧養這群羊。 8我在一個月之內除掉了三個牧人。

我厭煩羊群,他們也厭惡我。 9於是我說:「我不再牧養你們了。要死的就死吧,要亡的就亡吧,讓剩下的互相吞吃吧。」 10然後,我拿起那根叫「恩惠」的杖,把它折斷,以廢除我與萬民所立的約。 11約就在當天廢除了,那些注視著我的困苦羊便知道這是上帝的話。

12我對他們說:「你們若認為好,就給我工錢,不然就算了。」於是,他們給了我三十塊銀子作工錢。 13耶和華對我說:「把這一大筆錢丟給窯戶吧,這就是我在他們眼中的價值!」我便把三十塊銀子丟給聖殿中的窯戶。 14我又把那根叫「聯合」的杖折斷,以斷開猶大以色列之間的手足之情。

15耶和華又對我說:「你再拿起愚昧牧人的器具, 16因為我要使一位牧人在地上興起,他不照顧喪亡的,不尋找失散的,不醫治受傷的,不牧養健壯的,反而吃肥羊的肉,撕掉牠們的蹄子。

17「丟棄羊群的無用牧人有禍了!

願刀砍在他的臂膀和右眼上!

願他的臂膀徹底枯槁,

他的右眼完全失明!」