Zekaria 10 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zekaria 10:1-12

Bwana Ataitunza Yuda

110:1 Law 26:4; 1Fal 8:36; Za 104:13; 135:7; Ay 14:9; Yer 14:22; Yoe 2:32Mwombeni Bwana mvua wakati wa vuli;

ndiye Bwana atengenezaye mawingu ya tufani.

Huwapa watu manyunyu ya mvua,

pia mimea ya shambani kwa ajili ya kila mtu.

210:2 Eze 21:21; Isa 44:25; 40:19; Yer 23:16; Hes 27:17; Hos 3:4; Mt 9:36Sanamu huzungumza udanganyifu,

waaguzi huona maono ya uongo;

husimulia ndoto ambazo si za kweli,

wanatoa faraja batili.

Kwa hiyo watu wanatangatanga kama kondoo

walioonewa kwa kukosa mchungaji.

310:3 Isa 14:9; Yer 25:34; Eze 34:8-10; Kut 4:31; Rut 1:6; Sef 2:7; Lk 1:68; 1Pet 2:12“Hasira yangu inawaka dhidi ya wachungaji,

nami nitawaadhibu viongozi;

kwa kuwa Bwana Mwenye Nguvu Zote

atalichunga kundi lake,

nyumba ya Yuda,

naye atawafanya kuwa kama farasi

mwenye kiburi akiwa vitani.

410:4 Za 118:22; Mdo 4:11; Isa 22:23; Zek 9:10Kutoka Yuda litatokea Jiwe la pembeni,

kutoka kwake vitatoka vigingi vya hema,

kutoka kwake utatoka upinde wa vita,

kutoka kwake atatoka kila mtawala.

510:5 2Sam 22:43; Mik 7:10; 5:8; Amo 2:15; Hag 2:22; Zek 12:4Kwa pamoja watakuwa kama mashujaa

wanaokanyaga barabara za matope

wakati wa vita.

Kwa sababu Bwana yu pamoja nao,

watapigana na kuwashinda wapanda farasi.

610:6 Eze 30:24; 36:37; Za 102:13; 34:17; Isa 37:19; 14:1; 58:9; 65:24; Zek 8:7-8; 13:9“Nitaiimarisha nyumba ya Yuda

na kuiokoa nyumba ya Yosefu.

Nitawarejesha kwa sababu

nina huruma juu yao.

Watakuwa kama watu ambao

sijawahi kuwakataa

kwa sababu mimi ndimi Bwana Mungu wao,

nami nitawajibu.

710:7 Zek 9:15; 1Sam 2:1; Isa 60:5; Yoe 2:23Waefraimu watakuwa kama mashujaa,

mioyo yao itafurahi kana kwamba ni kwa divai.

Watoto wao wataona na kufurahi,

mioyo yao itashangilia katika Bwana.

810:8 Isa 5:26; Yer 33:22; Eze 36:11Nitawaashiria na kuwakusanya ndani.

Hakika nitawakomboa,

nao watakuwa wengi

kama walivyokuwa mwanzoni.

910:9 Isa 44:21; Eze 6:9Ijapokuwa niliwatawanya miongoni mwa mataifa,

hata hivyo wakiwa katika nchi za mbali

watanikumbuka mimi.

Wao na watoto wao watanusurika katika hatari

nao watarudi.

1010:10 Isa 11:11; 49:19; Zek 8:8; Yer 50:19; Rum 11:25; Kut 14:26-27Nitawarudisha kutoka Misri

na kuwakusanya toka Ashuru.

Nitawaleta katika nchi ya Gileadi na Lebanoni,

na hapo hapatakuwa na nafasi ya kuwatosha.

1110:11 Isa 19:5-7; 51:10; Sef 2:13; Eze 29:15; 30:13Watapita katika bahari ya mateso;

bahari iliyochafuka itatulizwa

na vilindi vyote vya Mto Naili vitakauka.

Kiburi cha Ashuru kitashushwa,

nayo fimbo ya utawala ya Misri itatoweka.

1210:12 Eze 30:24; Mik 4:5Nitawaimarisha katika Bwana,

na katika jina lake watatembea,”

asema Bwana.