Zaburi 99 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 99:1-9

Zaburi 99

Mungu Mfalme Mkuu

199:1 1Nya 16:30, 31; Za 97:1; 2Sam 6:2; Kut 15:14; 25:22Bwana anatawala,

mataifa na yatetemeke;

anakalia kiti cha enzi katikati ya makerubi,

dunia na itikisike.

299:2 Za 48:1; 148:13; 2:6; 46:10; 97:9; 113:4; Kut 15:1Bwana ni mkuu katika Sayuni;

ametukuzwa juu ya mataifa yote.

399:3 Za 103:1; 33:21; 97:12; 76:1; 30:4; 106:47; 111:9; 145:21; 148:5; Kut 15:11Wanalisifu jina lako ambalo ni kuu na la kuogopwa:

yeye ni mtakatifu!

499:4 1Fal 10:9; Za 98:9; Mwa 18:19, 25; Ufu 15:3; Ay 36:5; Kum 32:3, 4; Isa 11:3-5; Yer 23:5; Za 2:6Mfalme ni mwenye nguvu na hupenda haki,

wewe umethibitisha adili;

katika Yakobo umefanya

yaliyo haki na sawa.

599:5 Isa 66:1; Kut 15:2; 1Nya 28:2; Za 132:7Mtukuzeni Bwana Mungu wetu,

na mkaabudu katika mahali pa kuwekea miguu yake;

yeye ni mtakatifu.

699:6 Kut 24:6; 28:1; 1Sam 7:5; Za 4:3; 91:15Mose na Aroni walikuwa miongoni mwa makuhani wake,

Samweli alikuwa miongoni mwa walioliitia jina lake;

walimwita Bwana,

naye aliwajibu.

799:7 Kut 13:21; 19:9; Hes 11:25; 12:5Alizungumza nao kutoka nguzo ya wingu;

walizishika sheria zake na amri alizowapa.

899:8 Hes 14:20; Sef 3:7; Kum 9:20; Kut 22:27; Law 26:18Ee Bwana, wetu,

ndiwe uliyewajibu,

kwa Israeli ulikuwa Mungu mwenye kusamehe,

ingawa uliadhibu matendo yao mabaya.

9Mtukuzeni Bwana Mungu wetu,

mwabuduni kwenye mlima wake mtakatifu,

kwa maana Bwana Mungu wetu ni mtakatifu.