Zaburi 97 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 97:1-12

Zaburi 97

Mungu Mtawala Mkuu

197:1 Kut 15:18; Za 93:1; 96:10; 99:1; 96:11; Isa 24:23; 52:7Bwana anatawala, nchi na ifurahi,

visiwa vyote vishangilie.

297:2 Ay 22:14; Kut 19:9; Za 89:14Mawingu na giza nene vinamzunguka,

haki na hukumu ndio msingi wa kiti chake cha enzi.

397:3 Dan 7:10; Hab 3:5; Isa 9:19; Yoe 1:19; 2:3; Hab 3:5; 2Sam 22:9Moto hutangulia mbele zake

na huteketeza adui zake pande zote.

497:4 Ay 36:30; 2Sam 22:8; Za 18:7; 104:32; Ufu 6:12Umeme wake wa radi humulika dunia,

nchi huona na kutetemeka.

597:5 Za 46:2, 6; 22:14; Yos 3:11Milima huyeyuka kama nta mbele za Bwana,

mbele za Bwana wa dunia yote.

697:6 Za 50:6; 98:2; 19:1Mbingu zinatangaza haki yake,

na mataifa yote huona utukufu wake.

797:7 Kut 12:12; 20:4; Isa 37:18, 19; 42:17; Law 26:1; Kum 5:8; Yer 10:14; Ebr 1:6; Za 16:4Wote waabuduo sanamu waaibishwa,

wale wajisifiao sanamu:

mwabuduni yeye, enyi miungu yote!

897:8 Za 9:2; 48:11Sayuni husikia na kushangilia,

vijiji vya Yuda vinafurahi

kwa sababu ya hukumu zako, Ee Bwana.

997:9 Ay 34:29; Efe 1:21; Za 7:8; 47:9Kwa kuwa wewe, Ee Bwana, ndiwe Uliye Juu Sana kuliko dunia yote;

umetukuka sana juu ya miungu yote.

1097:10 Ay 28:28; Mit 2:8; Za 145:20; 31:23; 101:3; 37:28, 40; 34:7; Yer 15:21; 20:13; Dan 3:28; 6:16; 1Sam 2:9; Rum 12:9; 7:15; Amo 5:15Wale wanaompenda Bwana na wauchukie uovu,

kwa maana yeye hulinda maisha ya waaminifu wake

na kuwaokoa kutoka mkononi mwa mwovu.

1197:11 Ay 22:28; Za 11:5; 7:10Nuru huangaza wenye haki

na furaha kwa watu wanyofu wa moyo.

1297:12 Ay 22:19; Flp 4:4; Kut 3:15; Isa 41:16; Za 99:5; 104:34Furahini katika Bwana, ninyi mlio wenye haki,

lisifuni jina lake takatifu.