Zaburi 95 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 95:1-11

Zaburi 95

Wimbo Wa Kumsifu Mungu

195:1 Za 34:11; 80:2; 5:11; 81:1; Isa 44:23; Sef 3:14; 2Sam 22:47Njooni, tumwimbie Bwana kwa furaha;

tumfanyie kelele za shangwe

Mwamba wa wokovu wetu.

295:2 Za 42:4; 81:2; 100:2; Mik 6:6; Efe 5:19Tuje mbele zake kwa shukrani,

tumtukuze kwa vinanda na nyimbo.

395:3 Za 48:1; 86:10; 145:3; 147:5; 47:2; 96:4; 97:9Kwa kuwa Bwana ni Mungu mkuu,

mfalme mkuu juu ya miungu yote.

495:4 Za 63:9Mkononi mwake mna vilindi vya dunia,

na vilele vya milima ni mali yake.

595:5 Mwa 1:9; Za 146:6Bahari ni yake, kwani ndiye aliifanya,

na mikono yake iliumba nchi kavu.

695:6 Flp 2:10; Efe 3:14; 2Nya 6:13; 1Kor 6:20; 2Sam 12:16; Za 22:29; 100:3; 149:2; Lk 22:41; Isa 17:7; 54:5; Dan 6:10, 11; Ezr 9:5; 1Fal 8:54; Hos 8:14; Yn 1:3; Ay 35:10Njooni, tusujudu, tumwabudu,

tupige magoti mbele za Bwana Muumba wetu,

795:7 Za 74:1; Ebr 3:7kwa maana yeye ndiye Mungu wetu,

na sisi ni watu wa malisho yake,

kondoo chini ya utunzaji wake.

Kama mkiisikia sauti yake leo,

895:8 Hes 14:22; Mk 10:5; Kut 17:7; Kum 33:8; Ebr 4:7; 3:8, 15; Za 78:40msiifanye mioyo yenu migumu

kama mlivyofanya kule Meriba,95:8 Meriba maana yake ni Kugombana.

kama mlivyofanya siku ile

kule Masa95:8 Masa maana yake ni Kujaribiwa. jangwani,

995:9 Hes 14:22; 1Kor 10:9ambapo baba zenu walinijaribu na kunipima,

ingawa walikuwa wameyaona matendo yangu.

1095:10 Hes 14:34; Mdo 7:36; Isa 53:6; Ebr 3:10, 17; Za 119:67, 176; 58:3; Kut 16:35; Mit 12:26; 16:29; Yer 31:19; 50:6; Eze 34:6; Kum 8:6Kwa miaka arobaini nilikasirikia kizazi kile,

nikasema, “Hawa ni taifa ambalo mioyo yao imepotoka,

nao hawajazijua njia zangu.”

1195:11 Hes 14:23; Kum 1:35; Ebr 4:3; 3:7-11Hivyo nikatangaza kwa kiapo katika hasira yangu,

“Kamwe hawataingia rahani mwangu.”