Zaburi 94 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 94:1-23

Zaburi 94

Mungu Mlipiza Kisasi Kwa Ajili Ya Wenye Haki

194:1 Mwa 4:24; Za 80:1; Rum 12:19; Kum 33:2Ee Bwana, ulipizaye kisasi,

Ee Mungu ulipizaye kisasi, uangaze sasa.

294:2 Mwa 18:25; Yak 5:9; Hes 10:35; Za 31:23Ee Mhukumu wa dunia, inuka,

uwalipize wenye kiburi kama wanavyostahili.

394:3 Za 13:2; Mwa 20:3Hata lini, waovu, Ee Bwana,

hata lini waovu watashangilia?

494:4 Yer 43:2; Za 52:1; Yud 15Wanamimina maneno ya kiburi,

watenda mabaya wote wamejaa majivuno.

594:5 Za 28:9; 44:2; 74:8; Isa 3:15; Yer 8:21Ee Bwana, wanawaponda watu wako,

wanawaonea urithi wako.

694:6 Kum 10:18; 20:19; Isa 1:17Wanamchinja mjane na mgeni,

na kuwaua yatima.

794:7 Ay 22:14; Mwa 24:12Nao husema, “Bwana haoni,

Mungu wa Yakobo hafahamu.”

894:8 Kum 32:6; Za 73:22Sikizeni, enyi wajinga miongoni mwa watu;

enyi wapumbavu, lini mtakuwa na hekima?

994:9 Kut 4:11; Mit 20:12Je, aliyeweka sikio asisikie?

Aliyeumba jicho asione?

1094:10 Za 39:11; Ay 35:11; Yn 6:45; Isa 2:3; 28:26; Kut 35:34Je, anayeadhibisha mataifa asiadhibu?

Je, awafundishaye wanadamu asiwe na maarifa?

1194:11 Za 139:2; Mt 15:26; 9:4; 1Kor 3:20; 1:21Bwana anajua mawazo ya mwanadamu;

anajua kwamba ni ubatili.

1294:12 Ay 5:17; Kum 8:3; 1Kor 11:32; Mit 3:11; Ebr 12:5; 1Sam 12:23Ee Bwana, heri mtu anayeadhibishwa na wewe,

mtu unayemfundisha kwa sheria yako,

1394:13 Za 86:7; 7:15; 55:23unampa utulivu siku za shida,

mpaka shimo litakapokuwa limechimbwa

kwa ajili ya mwovu.

1494:14 Kum 31:6; Za 37:28; Rum 11:2; 1Sam 12:22; 1Fal 6:13; Yer 31:37Kwa kuwa Bwana hatawakataa watu wake,

hatauacha urithi wake.

1594:15 Za 97:2; 7:10; 11:2; 36:10Hukumu itasimamishwa tena kwenye haki,

wote walio na mioyo minyofu wataifuata.

1694:16 Hes 10:35; Isa 14:22; Za 17:13; 59:2Ni nani atakayeinuka dhidi ya mwovu kwa ajili yangu?

Ni nani atakayenikinga dhidi ya watenda maovu?

1794:17 Za 124:2; 31:17Kama Bwana asingelinisaidia upesi,

ningelikuwa ninaishi katika ukimya wa kifo.

1894:18 Kum 32:35; Ay 12:5Niliposema, “Mguu wangu unateleza,”

Ee Bwana, upendo wako ulinishikilia.

1994:19 Mhu 11:10; Ay 6:10Wakati wasiwasi ulipokuwa mwingi ndani yangu,

faraja yako ilinipa furaha nafsini mwangu.

2094:20 Za 58:2; Isa 10:1; 2Kor 6:14; Amo 6:3; Yer 22:30; 36:30Je, kiti cha utawala wa udhalimu kitajiunga nawe,

ule utawala uletao taabu kutokana na sheria zake?

2194:21 Za 56:6; 106:38; Mit 17:15, 26; 28:21; Isa 5:20, 23; Mt 27:1, 4; Mwa 18:23; Mit 17:15; Kut 23:7Huungana kuwashambulia wenye haki,

kuwahukumu kufa wasio na hatia.

2294:22 Za 18:2; 61:2; 2Sam 22:3Lakini Bwana amekuwa ngome yangu,

na Mungu wangu amekuwa mwamba ninaoukimbilia.

2394:23 Za 37:38; 145:20; 54:5; 9:5; Mit 2:22; Kut 32:34Yeye atawalipa kwa ajili ya dhambi zao

na atawaangamiza kwa ajili ya maovu yao;

Bwana Mungu wetu atawaangamiza.