Zaburi 92 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 92:1-15

Zaburi 92

Wimbo Wa Kumsifu Mungu

Zaburi. Wimbo wa siku ya Sabato.

192:1 Za 27:6; 147:1; 135:3Ni vyema kumshukuru Bwana

na kuliimbia jina lako, Ee Uliye Juu Sana,

292:2 Za 55:17kuutangaza upendo wako asubuhi,

na uaminifu wako wakati wa usiku,

392:3 Za 71:22; 1Sam 10:5; Neh 12:27; Za 33:2; 81:2kwa zeze yenye nyuzi kumi

na kwa sauti ya kinubi.

492:4 Za 5:11; 27:6; 8:6; 111:7; 143:5Ee Bwana, kwa kuwa matendo yako yamenifurahisha,

nitaziimba kwa shangwe kazi za mikono yako.

592:5 Ay 36:24; Ufu 15:3; Za 40:5; 139:17; Isa 28:29; 31:2; Rum 11:33Ee Bwana, tazama jinsi yalivyo makuu matendo yako,

tazama jinsi yalivyo ya kina mawazo yako!

692:6 Za 73:22Mjinga hafahamu,

mpumbavu haelewi,

792:7 Ay 21:7; Yer 12:1; Mal 3:15; Za 37:1ingawa waovu huchipua kama majani

na wote watendao mabaya wanastawi,

wataangamizwa milele.

8Bali wewe, Ee Bwana,

utatukuzwa milele.

992:9 Za 45:5; 68:1; 89:10Ee Bwana, hakika adui zako,

hakika adui zako wataangamia.

Wote watendao mabaya watatawanyika.

1092:10 Za 89:17; 29:6; 89:10Umeitukuza pembe92:10 Pembe inawakilisha nguvu. yangu kama ile ya nyati dume,

mafuta mazuri yamemiminwa juu yangu.

1192:11 Za 54:7; 91:8Macho yangu yamewaona adui zangu wakishindwa,

masikio yangu yamesikia maangamizi ya adui zangu waovu.

1292:12 Za 72:7; 1:3; 52:8; Yer 17:8; Hos 14:6; Wim 7:7Wenye haki watastawi kama mtende,

watakuwa kama mwerezi wa Lebanoni,

1392:13 Isa 60:21; Mt 15:13; Yn 15:2, 5; Za 135:2waliopandwa katika nyumba ya Bwana,

watastawi katika nyua za Mungu wetu.

1492:14 Za 1:3; Yn 15:2Wakati wa uzee watakuwa bado wanazaa matunda,

watakuwa wabichi tena wamejaa nguvu,

1592:15 Ay 34:10wakitangaza, “Bwana ni mkamilifu;

yeye ni Mwamba wangu,

na ndani yake hamna uovu.”