Zaburi 9 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 9:1-20

Zaburi 99 Zaburi hii ikiunganishwa na ya 10 zimetungwa kila beti likianzia na herufi ya alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T); zote ni 22.

Shukrani Kwa Mungu Kwa Ajili Ya Haki Yake

Kwa mwimbishaji. Mtindo wa muth-labeni.9:0 Muth-labeni ni mtajo mmojawapo katika lugha za muziki. Zaburi ya Daudi.

19:1 Za 86:12; 11:1; 119:2, 10; 145:5; 138:1; Kum 4:34Ee Bwana, nitakutukuza kwa moyo wangu wote,

nitayasimulia matendo yako yote ya ajabu.

29:2 Ay 22:19; Isa 25:9; Za 14:7; 31:7; 70:4; 92:1; 97:8; 126:3; Mit 23:15; Yoe 2:21; Ufu 19:7; Yer 30:19; Sef 3:14; Mt 5:12; 2Nya 31:2Nitafurahi na kushangilia ndani yako.

Nitaliimbia sifa jina lako, Ewe Uliye Juu Sana.

3Adui zangu wamerudi nyuma,

wamejikwaa na kuangamia mbele zako.

49:4 1Fal 8:45; Isa 6:1; Ay 16:21; Za 7:11; 11:4; 47:8; 67:4; 98:9; 1Pet 2:23Kwa maana umetetea haki yangu na msimamo wangu;

umeketi kwenye kiti chako cha enzi,

ukihukumu kwa haki.

59:5 Mwa 20:7; 37:10; 1Nya 16:21; Za 59:5; 105:14; Isa 26:14; 66:15; Ay 18:17; Kum 9:14Umekemea mataifa na kuwaangamiza waovu;

umeyafuta majina yao milele na milele.

69:6 Kum 29:28; Yer 2:3; Mhu 9:5; Isa 14:22; 26:14; Sef 2:8-10; Za 34:16; 109:15Uharibifu usiokoma umempata adui,

umeingʼoa miji yao;

hata kumbukumbu lao limetoweka.

79:7 Mik 5:2; Ufu 19:6; Ebr 1:11; Hab 1:12; Za 90:2; 1Nya 16:31Bwana anatawala milele,

ameweka kiti chake cha enzi apate kuhukumu.

89:8 Za 7:11; 11:7; 45:6; 72:29:8 Kum 33:27; 2Sam 22:3; Za 10:18; 32:7; 74:21; 121:7Mungu atahukumu ulimwengu kwa haki,

atatawala mataifa kwa haki.

9Bwana ni kimbilio la watu wanaoonewa,

ni ngome imara wakati wa shida.

109:10 Mwa 28:15; Kum 4:31; Za 22:1; 37:25; 71:11; 70:4; 91:14; Isa 49:14; Yer 15:18; Ebr 13:5; Yn 17:3; 2Kor 4:6; 1Yn 2:3, 4; 2Tim 1:12Wote wanaolijua jina lako watakutumaini wewe,

kwa maana wewe Bwana,

hujawaacha kamwe wakutafutao.

119:11 Za 7:17; 2:6; 57:9; 18:49; 44:11; 105:1; 106:27; Isa 24:13; Eze 20:23; 1Tim 3:16Mwimbieni Bwana sifa, amefanywa mtawala Sayuni,

tangazeni miongoni mwa mataifa, yale aliyoyatenda.

129:12 2Sam 4:11; Za 10:17; 22:24; Isa 49:13Kwa maana yeye alipizaye kisasi cha damu hukumbuka,

hapuuzi kilio cha wanaoonewa.

139:13 Hes 10:9; Za 3:7; 18:3; 6:2; 41:4; 51:1; 86:3, 16; 119:132; Ay 17:16; Mt 16:18Ee Bwana, tazama jinsi walivyo wengi adui zangu wanaonitesa!

Nihurumie, uniinue kutoka malango ya mauti,

149:14 2Fal 19:21; Isa 1:8; 10:32; 37:22; 62:11; Yer 4:31; 6:2; Mao 1:6; Mt 21:5; Mik 1:13; Sef 3:14; Zek 2:10; Yn 12:15ili niweze kutangaza sifa zako

katika malango ya Binti Sayuni

na huko niushangilie wokovu wako.

159:15 Ay 4:8; Za 35:7, 8; 57:6Mataifa wameanguka kwenye shimo walilolichimba,

miguu yao imenaswa kwenye wavu waliouficha.

169:16 Kut 7:5; Mt 5:22Bwana anajulikana kwa haki yake,

waovu wamenaswa katika kazi za mikono yao.

179:17 Hes 16:30; Mt 5:5; Za 50:22; Ay 8:13; Hos 2:13; Yer 2:32Waovu wataishia kuzimu,

naam, mataifa yote wanaomsahau Mungu.

189:18 Za 25:3; 39:7; 71:5; Mt 23:18; Yer 14:8, 12; Za 74:19; 12:5; Flp 1:20Lakini mhitaji hatasahaulika siku zote,

wala matumaini ya walioonewa hayatapotea.

199:19 2Nya 14:11; Za 3:7; 110:6; Isa 2:4; Yoe 3:12Ee Bwana, inuka, usimwache binadamu ashinde.

Mataifa na yahukumiwe mbele zako.

209:20 Mwa 35:5; Isa 13:8; Lk 21:26; Za 31:13; 62:9; Isa 31:3; Eze 28:2Ee Bwana, wapige kwa hofu,

mataifa na yajue kuwa wao ni watu tu.