Zaburi 89
Wimbo Wakati Wa Taabu Ya Kitaifa
Utenzi wa Ethani Mwezrahi.
189:1 Za 59:16; 36:5; 40:10Nitaimba juu ya upendo mkuu wa Bwana milele;
kwa kinywa changu nitajulisha uaminifu wako
ujulikane kwa vizazi vyote.
289:2 Za 36:5Nitatangaza kuwa upendo wako unasimama imara milele
na uaminifu wako umeuthibitisha mbinguni.
389:3 Eze 34:23; Hes 3:5; Ebr 7:21; Mdo 2:30Ulisema, “Nimefanya agano na mteule wangu,
nimemwapia mtumishi wangu Daudi,
489:4 2Sam 7:12-16; Lk 1:32, 33; Mt 1:1; Isa 9:6, 7; Rum 1:3; 1Fal 9:5; 8:16; Eze 37:24, 25; Za 132:11, 12‘Nitaimarisha uzao wako milele
na kudumisha ufalme wako kwa vizazi vyote.’ ”
589:5 Za 19:1; 1:5Ee Bwana, mbingu zinayasifu maajabu yako,
uaminifu wako pia katika kusanyiko la watakatifu.
689:6 Mwa 1:26; Kut 9:14; Za 18:31; 113:5Kwa kuwa ni nani katika mbingu
anayeweza kulinganishwa na Bwana?
Ni nani miongoni mwa viumbe vya mbinguni
aliye kama Bwana?
789:7 Ay 5:1; Za 11:1; 47:2Katika kusanyiko la watakatifu, Mungu huogopwa sana,
anahofiwa kuliko wote wanaomzunguka.
889:8 Isa 6:3; Za 71:19Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote,
ni nani aliye kama wewe?
Ee Bwana, wewe ni mwenye nguvu,
na uaminifu wako unakuzunguka.
989:9 Za 65:7; Ay 38:11; Nah 1:4; Mt 8:26Wewe unatawala bahari yenye msukosuko;
wakati mawimbi yake yanapoinuka, wewe unayatuliza.
1089:10 Ay 9:13; Za 59:11; 68:1; 92:9; Isa 30:9Wewe ulimponda Rahabu89:10 Rahabu hapa ina maana jina la Misri kwa fumbo, yaani mwenye majivuno (lakini sio Rahabu wa Yos 2).
kama mmojawapo wa waliochinjwa;
kwa mkono wako wenye nguvu,
uliwatawanya adui zako.
1189:11 Kum 10:14; Za 24:1; 115:6; 1Nya 29:11; Mwa 1:1Mbingu ni zako, nayo nchi pia ni yako,
uliuwekea ulimwengu msingi
pamoja na vyote vilivyomo.
1289:12 Yos 19:22; Kum 3:8; 4:48; Za 98:8; Yos 12:1; Amu 4:6Uliumba kaskazini na kusini;
Tabori na Hermoni wanaliimbia jina lako kwa furaha.
1389:13 Yos 4:24Mkono wako umejaa uwezo;
mkono wako una nguvu,
mkono wako wa kuume umetukuzwa.
1489:14 Za 97:2; 85:10, 11Haki na hukumu ndio msingi wa kiti chako cha enzi;
upendo na uaminifu vinakutangulia.
1589:15 Za 1:1; 44:3; Hes 10:10Heri ni wale ambao wamejifunza kukusifu kwa shangwe,
wanaotembea katika mwanga
wa uwepo wako, Ee Bwana.
1689:16 Za 30:4; 105:3Wanashangilia katika jina lako mchana kutwa,
wanafurahi katika haki yako.
1789:17 Za 18:1, 24; 75:10; 92:10; 112:9; 148:14Kwa kuwa wewe ni utukufu na nguvu yao,
kwa wema wako unatukuza pembe89:17 Pembe inawakilisha nguvu. yetu.
1889:18 Hos 13:10; Za 18:2; 47:9; Isa 16:5; 33:17, 22Naam, ngao yetu ni mali ya Bwana,
na mfalme wetu mali ya Aliye Mtakatifu wa Israeli.
19Ulizungumza wakati fulani katika maono,
kwa watu wako waaminifu, ukasema:
“Nimeweka nguvu kwa shujaa,
nimemwinua kijana miongoni mwa watu.
2089:20 Mdo 13:22; Za 78:70; Kut 29:7; 1Fal 1:39; 1Sam 2:35; 2Sam 22:51Nimemwona Daudi, mtumishi wangu,
na nimemtia mafuta yangu matakatifu.
2189:21 Za 89:13; 18:35Kitanga changu kitamtegemeza,
hakika mkono wangu utamtia nguvu.
2289:22 Amu 3:15; 2Sam 7:10Hakuna adui atakayemtoza ushuru,
hakuna mtu mwovu atakayemwonea.
2389:23 Za 18:40; 2Sam 7:9Nitawaponda adui zake mbele zake
na kuwaangamiza watesi wake.
2489:24 2Sam 7:15; Za 61:7Upendo wangu mkamilifu utakuwa pamoja naye,
kwa Jina langu pembe yake itatukuzwa.
2589:25 Za 72:8Nitauweka mkono wake juu ya bahari,
mkono wake wa kuume juu ya mito.
2689:26 Za 62:2; Yer 3:4; 2Sam 7:14; 22:47; 1Nya 22:10; Yn 5:17; Ebr 1:5Naye ataniita kwa sauti, ‘Wewe ni Baba yangu,
Mungu wangu, Mwamba na Mwokozi wangu.’
2789:27 Kol 1:18; Hes 24:7; Za 2:6, 7; Ufu 1:5; 19:16Nitamteua pia awe mzaliwa wangu wa kwanza,
aliyetukuka kuliko wafalme wote wa dunia.
2889:28 Za 89:33-34; Isa 55:3Nitadumisha upendo wangu kwake milele,
na agano langu naye litakuwa imara.
2989:29 Isa 9:7; Yer 33:17; Dan 7:14; Kum 11:21; Za 89:4, 36Nitaudumisha uzao wake milele,
kiti chake cha enzi kama mbingu zinavyodumu.
3089:30 2Sam 7:14; Yer 9:13“Kama wanae wataacha amri yangu
na wasifuate sheria zangu,
31kama wakihalifu maagizo yangu
na kutoshika amri zangu,
3289:32 2Sam 7:14nitaadhibu dhambi yao kwa fimbo,
uovu wao kwa kuwapiga,
3389:33 2Sam 7:15lakini sitauondoa upendo wangu kwake,
wala sitausaliti uaminifu wangu kamwe.
3489:34 Hes 23:19Mimi sitavunja agano langu
wala sitabadili lile ambalo midomo yangu imelitamka.
3589:35 Za 110:4; Ebr 6:13, 17; Amo 4:2; 8:7Mara moja na kwa milele, nimeapa kwa utakatifu wangu,
nami sitamdanganya Daudi:
3689:36 Za 89:4; 2Sam 7:18; Lk 1:33; Yn 12:34kwamba uzao wake utaendelea milele,
na kiti chake cha enzi kitadumu mbele zangu kama jua;
3789:37 Yer 31:35; 33:20, 21kitaimarishwa milele kama mwezi,
shahidi mwaminifu angani.”
3889:38 1Nya 28:9; Isa 22:5; Mao 2:2Lakini wewe umemkataa, umemdharau,
umemkasirikia sana mpakwa mafuta wako.
3989:39 Mao 5:16Umelikana agano lako na mtumishi wako,
na umeinajisi taji yake mavumbini.
4089:40 Za 80:12; Isa 22:5; Mao 2:2Umebomoa kuta zake zote,
na ngome zake zote umezifanya kuwa magofu.
4189:41 Amu 2:14; Za 44:13Wote wapitao karibu wamemnyangʼanya mali zake;
amekuwa dharau kwa jirani zake.
4289:42 Za 13:2; 80:6Umeutukuza mkono wa kuume wa adui zake,
umewafanya watesi wake wote washangilie.
4389:43 Za 44:10Umegeuza makali ya upanga wake,
na hukumpa msaada katika vita.
44Umeikomesha fahari yake,
na kukiangusha kiti chake cha enzi.
4589:45 Za 39:5; 44:15; 109:29Umezifupisha siku za ujana wake,
umemfunika kwa vazi la aibu.
4689:46 Za 79:5Hata lini, Ee Bwana? Utajificha milele?
Ghadhabu yako itawaka kama moto hata lini?
4789:47 Mwa 47:9; Ay 7:7; Za 39:5; 1Pet 1:24Kumbuka jinsi maisha yangu yanavyopita haraka.
Ni kwa ubatili kiasi gani umemuumba mwanadamu!
4889:48 Mwa 5:24; Za 22:29; Ebr 11:5Ni mtu gani awezaye kuishi na asione kifo,
au kujiokoa mwenyewe kutoka nguvu za kaburi?89:48 Kaburi hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol.
4989:49 2Sam 7:12; Isa 55:13Ee Bwana, uko wapi upendo wako mkuu wa mwanzoni,
ambao katika uaminifu wako ulimwapia Daudi?
5089:50 Za 69:19Bwana kumbuka jinsi mtumishi wako amesimangwa,
jinsi ninavyovumilia moyoni mwangu dhihaka za mataifa yote,
5189:51 Za 74:10dhihaka ambazo kwazo adui zako
wamenisimanga, Ee Bwana,
ambazo kwazo wamesimanga
kila hatua ya mpakwa mafuta wako.
5289:52 Za 41:13; 72:19Msifuni Bwana milele!
Amen na Amen.