Zaburi 85 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 85:1-13

Zaburi 85

Maombi Kwa Ajili Ya Ustawi Wa Taifa

Kwa mwimbishaji. Zaburi ya wana wa Kora.

185:1 Kum 30:3; Za 14:7; Yer 30:18; Eze 39:25Ee Bwana, ulionyesha wema kwa nchi yako.

Ulimrejeshea Yakobo baraka zake.85:1 Au: Uliwarudisha mateka wa Yakobo.

285:2 Hes 14:19; Kut 32:30; Za 78:38Ulisamehe uovu wa watu wako,

na kufunika dhambi zao zote.

385:3 Za 78:38; 106:23; Dan 9:16; Kut 32:12; Yn 3:9; Kum 13:17Uliweka kando ghadhabu yako yote

na umegeuka na kuiacha hasira yako kali.

485:4 Za 71:20; 65:5Ee Mungu Mwokozi wetu, uturejeshe tena,

nawe uiondoe chuki yako juu yetu.

585:5 Za 50:21Je, utatukasirikia milele?

Utaendeleza hasira yako kwa vizazi vyote?

685:6 Za 80:18; Flp 3:1; Hab 3:2Je, hutatuhuisha tena,

ili watu wako wakufurahie?

785:7 Za 6:4; 27:1Utuonyeshe upendo wako usiokoma, Ee Bwana,

utupe wokovu wako.

885:8 Law 26:6; Isa 60:17; Yn 14:27; 2The 3:16; Mit 26:11; 27:22; Hab 2:1; Zek 9:10; 2Pet 2:20Nitasikiliza lile atakalosema Mungu aliye Bwana;

anaahidi amani kwa watu wake, watakatifu wake:

lakini nao wasirudie upumbavu.

985:9 Za 27:1; Kut 29:43; Isa 43:3; 45:8; 46:13; 62:11; 51:5; 56:1; 60:19; Hag 2:9; Zek 2:5Hakika wokovu wake uko karibu na wale wamchao,

ili utukufu wake udumu katika nchi yetu.

1085:10 Isa 32:17; Mit 3:3; Lk 2:14; Yn 1:17; 14:27; Za 89:14; 115:1; 72:2, 3; Mik 7:20Upendo na uaminifu hukutana pamoja,

haki na amani hubusiana.

1185:11 Isa 45:8Uaminifu huchipua kutoka nchi,

haki hutazama chini kutoka mbinguni.

1285:12 Za 67:6; 84:11; Yak 1:17; Law 26:4; Zek 8:12Naam, hakika Bwana atatoa kilicho chema,

nayo nchi yetu itazaa mavuno yake.

13Haki itatangulia mbele yake

na kutengeneza njia kwa ajili ya hatua zake.