Zaburi 83 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 83:1-18

Zaburi 83

Maombi Kwa Ajili Ya Kushindwa Kwa Adui Wa Israeli

Wimbo. Zaburi ya Asafu.

183:1 Za 28:1; 35:22; Isa 42:14; 57:11; 62:1; 64:12Ee Mungu, usinyamaze kimya,

usinyamaze, Ee Mungu, usitulie.

283:2 Za 2:1; Isa 17:12; Amu 8:28Tazama watesi wako wanafanya fujo,

jinsi adui zako wanavyoinua vichwa vyao.

383:3 Kut 1:10; Za 31:13; 17:14Kwa hila, wanafanya shauri dhidi ya watu wako,

wanafanya shauri baya dhidi ya wale unaowapenda.

483:4 Es 3:6; Yer 33:24; 11:19; 2Sam 10:6; 2Nya 20:1Wanasema, “Njooni, tuwaangamize kama taifa,

ili jina la Israeli lisikumbukwe tena.”

583:5 Za 2:2Kwa nia moja wanapanga mashauri mabaya pamoja,

wanafanya muungano dhidi yako,

683:6 Za 137:7; Isa 34:5; Yer 49:7; Amo 1:11; 2Nya 20:1; Mwa 25:16mahema ya Edomu na Waishmaeli,

ya Wamoabu na Wahagari,

783:7 Yos 13:5; Mwa 19:38; 14:7; Kut 17:14; 15:14; Isa 23:3; Eze 27:3Gebali,83:7 Yaani Bubilo, mji wa zamani sana wa Ufoinike (kama kilomita 80 kaskazini mwa Beiruti). Amoni na Amaleki,

Ufilisti, pamoja na watu wa Tiro.

883:8 Mwa 10:11; Kum 2:9Hata Ashuru wameungana nao

kuwapa nguvu wazao wa Loti.

983:9 Hes 31:7, 8; Isa 9:4; Yos 11:1; Amu 4:2, 15, 23, 24; 7:1, 2, 3; Mwa 25:2Uwatendee kama vile ulivyowatendea Midiani,

na kama vile ulivyowatendea Sisera na Yabini

hapo kijito cha Kishoni,

1083:10 1Sam 28:7; 2Fal 9:37; Isa 5:25; Yer 8:2; 9:22; 16:4; 25:33; Sef 1:17ambao waliangamia huko Endori

na wakawa kama takataka juu ya nchi.

1183:11 Amu 7:25; 8:5Wafanye wakuu wao kama Orebu na Zeebu,

watawala wao kama Zeba na Salmuna,

1283:12 2Nya 20:11; Eze 35:10ambao walisema, “Na tumiliki nchi

ya malisho ya Mungu.”

1383:13 Ay 13:25Ee Mungu wangu, wapeperushe kama mavumbi ya kisulisuli,

kama makapi yapeperushwayo na upepo.

1483:14 Kum 32:22; Isa 9:13Kama vile moto uteketezavyo msitu

au mwali wa moto unavyounguza milima,

1583:15 Za 50:3; Ay 9:17wafuatilie kwa tufani yako

na kuwafadhaisha kwa dhoruba yako.

1683:16 Za 34:5; 109:29; 132:18Funika nyuso zao kwa aibu

ili watu walitafute jina lako, Ee Bwana.

1783:17 2Fal 19:26; Za 35:4Wao na waaibishwe na kufadhaishwa milele,

na waangamie kwa aibu.

1883:18 Za 68:4; 7:8; 18:13Hebu wajue kwamba wewe, ambaye jina lako ni Bwana,

kwamba wewe peke yako ndiwe Uliye Juu Sana ya dunia yote.