Zaburi 82 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 82:1-8

Zaburi 82

Maombi Kwa Ajili Ya Kutaka Haki

Zaburi ya Asafu.

182:1 Mhu 5:8; Kut 21:6; Za 7:8; 58:11; Isa 3; 13; 66:16; Yoe 3:12; Ay 21:22Mungu anaongoza kusanyiko kuu,

anatoa hukumu miongoni mwa “miungu”:

282:2 Kum 1:17; Za 58:1-2; Mit 18:5“Hata lini utaendelea kuwatetea wasio haki

na kuonyesha upendeleo kwa waovu?

382:3 Kum 24:17; Za 140:12; Yer 5:28; 22:16Teteeni wanyonge na yatima,

tunzeni haki za maskini na walioonewa.

4Mwokoeni mnyonge na mhitaji,

wakomboeni kutoka mkononi mwa mwovu.

582:5 Za 11:3; 14:4; 53:2; Ay 30:26; Isa 5:30; 8:21-22; 9:2; 59:9; 60:2; Yer 13:16; 23:12, 16; Mao 3:2; Amu 5:4“Hawajui lolote, hawaelewi lolote.

Wanatembea gizani;

misingi yote ya dunia imetikisika.

682:6 Kut 22:9; Yn 10:34“Nilisema, ‘Ninyi ni “miungu”;

ninyi nyote ni wana wa Aliye Juu Sana.’

782:7 Za 49:12; Eze 31:14Lakini mtakufa kama wanadamu wa kawaida;

mtaanguka kama mtawala mwingine yeyote.”

882:8 Za 12:5; 76:9; 2:8Ee Mungu, inuka uihukumu nchi,

kwa kuwa mataifa yote ni urithi wako.