Zaburi 81 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 81:1-16

Zaburi 81

Wimbo Wa Sikukuu

Kwa mwimbishaji. Mtindo wa gitithi. Zaburi ya Asafu.

181:1 Za 66:1; 81:4Mwimbieni kwa furaha, Mungu aliye nguvu yetu;

mpigieni kelele za shangwe Mungu wa Yakobo!

281:2 Kut 15:20; Za 92:3; Ay 21:12Anzeni wimbo, pigeni matari,

pigeni kinubi na zeze kwa sauti nzuri.

381:3 Kut 19:13; Neh 10:33Pigeni baragumu za pembe za kondoo dume

wakati wa Mwandamo wa Mwezi,

na wakati wa mwezi mpevu,

katika siku ya Sikukuu yetu;

481:4 Za 81:1; Law 23:24; Hes 10:10hii ni amri kwa Israeli,

agizo la Mungu wa Yakobo.

581:5 Kut 11:4; Za 114:1Aliiweka iwe kama sheria kwa Yosefu

alipotoka dhidi ya Misri,

huko tulikosikia lugha ambayo hatukuielewa.

681:6 Kut 1:14; Isa 9:4; 52:2Asema, “Nimeondoa mzigo mabegani mwao;

mikono yao iliwekwa huru kutoka kwenye kikapu.

781:7 Kut 2:23; 19:19; 17:7; Kum 33:8Katika shida yako uliniita nami nikakuokoa,

nilikujibu katika mawingu yenye ngurumo;

nilikujaribu katika maji ya Meriba.

881:8 Za 50:7; 78:1“Enyi watu wangu, sikieni, nami nitawaonya:

laiti kama mngenisikiliza, ee Israeli!

981:9 Kut 20:3Hamtakuwa na mungu mgeni miongoni mwenu;

msimsujudie mungu wa kigeni.

1081:10 Kut 6:6; 13:3; 29:46; Eze 2:8; Za 107:9; 37:3; Yn 13:7Mimi ni Bwana Mungu wako,

niliyekutoa nchi ya Misri.

Panua sana kinywa chako

nami nitakijaza.

1181:11 Kut 32:1-6“Lakini watu wangu hawakutaka kunisikiliza;

Israeli hakutaka kunitii.

1281:12 Eze 20:25; Mdo 7:42; Rum 1:24Basi niliwaacha katika ukaidi wa mioyo yao

wafuate mashauri yao wenyewe.

1381:13 Kum 5:29; Isa 48:18; Yer 44:4, 5; Mt 23:37“Laiti kama watu wangu wangalinisikiliza,

kama Israeli wangalifuata njia zangu,

1481:14 Za 47:3; Amo 1:8ningaliwatiisha adui zao kwa haraka,

na kuugeuza mkono wangu dhidi ya watesi wao!

1581:15 2Sam 22:45Wale wanaomchukia Bwana wangalinyenyekea mbele zake,

na adhabu yao ingedumu milele.

1681:16 Kum 32:14Bali ninyi mngalilishwa ngano iliyo bora,

na kuwatosheleza kwa asali itokayo kwenye mwamba.”