Zaburi 76 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 76:1-12

Zaburi 76

Mungu Wa Israeli Ni Mhukumu Wa Dunia Yote

Kwa mwimbishaji. Kwa ala za nyuzi za muziki. Zaburi ya Asafu. Wimbo.

176:1 Za 99:3Katika Yuda, Mungu anajulikana,

jina lake ni kuu katika Israeli.

276:2 Mwa 14:18; Ebr 7:1; Za 2:6; 2Sam 5:7Hema lake liko Salemu,

makao yake katika Sayuni.

376:3 Za 46:9; Eze 39:9Huko alivunja mishale imetametayo,

ngao na panga, silaha za vita.

476:4 Za 36:9; Eze 38:12Wewe unangʼaa kwa mwanga,

mwenye fahari zaidi ya milima yenye utajiri wa wanyama pori.

576:5 Amu 20:44; Za 13:3; Mt 9:24; Isa 46:12; Yer 51:39Mashujaa hulala wametekwa nyara,

hulala usingizi wao wa mwisho;

hakuna hata mmoja wa watu wa vita

anayeweza kuinua mikono yake.

676:6 Kut 15:1; Zek 12:4; Nah 2:13; Za 50:21Kwa kukemea kwako, Ee Mungu wa Yakobo,

farasi na gari la vita vilikaa kimya.

776:7 Ay 41:10; Nah 1:6; 1Nya 16:25; Ezr 9:15; Ufu 6:17; Za 2:5Wewe peke yako ndiye wa kuogopwa.

Ni nani awezaye kusimama mbele yako unapokasirika?

876:8 1Nya 16:30; Eze 38:20Kutoka mbinguni ulitamka hukumu,

nayo nchi ikaogopa, ikawa kimya:

976:9 Za 9:8; 58:11; 74:22; 82:8; 96:13; 72:4wakati wewe, Ee Mungu, ulipoinuka kuhukumu,

kuwaokoa wote walioonewa katika nchi.

1076:10 Kut 9:16; Rum 9:17Hakika ghadhabu yako dhidi ya wanadamu inakuletea sifa,

na masalia ya ghadhabu yako unajifunga mshipi.

1176:11 Mhu 5:4-5; Za 68:35; Law 22:18; Za 50:14; 2Nya 32:23Wekeni nadhiri kwa Bwana Mungu wenu na kuzitimiza;

nchi zote za jirani na walete zawadi

kwa Yule astahiliye kuogopwa.

12Huvunja roho za watawala;

anaogopwa na wafalme wa dunia.

Chinese Contemporary Bible 2023 (Traditional)

詩篇 76:1-12

第76篇

上帝是勝利者

亞薩的詩歌,交給樂長,用弦樂器。

1上帝在猶大人人皆知,

以色列威名遠揚。

2祂的住處在撒冷

祂的居所在錫安

3祂在那裡摧毀敵人的火箭、

盾牌和刀劍等兵器。(細拉)

4上帝啊,你榮耀無比,

你的威嚴超過盛產獵物的群山。

5強敵被擄掠,他們倒地而亡,

勇士都無還手之力。

6雅各的上帝啊,你一斥責,

他們就人仰馬翻。

7唯有你當受敬畏。

你發怒的時候,

誰能在你面前站立呢?

8-9上帝啊,

你從天上宣告審判。

你施行審判,

拯救世上一切受苦之人時,

大地一片恐懼靜默。(細拉)

10你向人類發怒帶給你榮耀,

你要發盡你的烈怒。

11你們要向你們的上帝耶和華許願、還願,

願四周的鄰邦都帶禮物來獻給當受敬畏的主。

12祂挫敗首領的傲氣,

世上的君王都敬畏祂。