Zaburi 74
Maombi Kwa Ajili Ya Taifa Kuokolewa
Utenzi wa Asafu.
174:1 Yer 23:1; Za 43:2; 44:23; 95:7; 79:13; 100:3; Eze 34:8, 31; Lk 12:32Ee Mungu, mbona umetukataa milele?
Mbona hasira yako inatoka moshi
juu ya kondoo wa malisho yako?
274:2 1Kor 6:20; Kum 32:7; Kut 34:9; 15:13, 16; Isa 48:20; Za 2:6; 43:3; 68:16; Isa 46:13; Oba 1:17; Yoe 3:17, 21Kumbuka watu uliowanunua zamani,
kabila la urithi wako, ambao uliwakomboa:
Mlima Sayuni, ambamo uliishi.
374:3 Isa 44:26; 52:9Geuza hatua zako kuelekea magofu haya ya kudumu,
uharibifu wote huu ambao adui ameuleta pale patakatifu.
474:4 Mao 2:7; Hes 2:2; Yer 4:6; Dan 6:27Adui zako wamenguruma pale ulipokutana nasi,
wanaweka bendera zao kama alama.
574:5 Yer 46:23Walifanya kama watu wanaotumia mashoka
kukata kichaka cha miti.
674:6 1Fal 6:18Walivunjavunja milango yote iliyonakshiwa
kwa mashoka na vishoka vyao.
774:7 Law 15:31; 20:3; Mdo 21:28; Za 75:1Waliteketeza kabisa mahali pako patakatifu,
wakayanajisi makao ya Jina lako.
874:8 2Fal 25:9; Za 83:4; 94:5; Yer 34:22; 52:13; 21:10; 2Nya 36:19Walisema mioyoni mwao,
“Tutawaponda kabisa!”
Walichoma kila mahali ambapo Mungu
aliabudiwa katika nchi.
974:9 Kut 4:17; 10:1; 1Sam 3:1; Mik 3:6; Mt 16:4Hatukupewa ishara za miujiza;
hakuna manabii waliobaki,
hakuna yeyote kati yetu ajuaye
hali hii itachukua muda gani.
1074:10 Za 6:3; 79:5; 80:4; 74:22; 44:16Ee Mungu, mtesi atakudhihaki mpaka lini?
Je, adui watalitukana jina lako milele?
1174:11 Kut 15:6; Neh 5:13; Eze 5:3Kwa nini unazuia mkono wako,
mkono wako wa kuume?
Uutoe kutoka makunjo ya vazi lako
na uwaangamize!
1274:12 Za 2:6; 24:7; 68:24; 44:4Lakini wewe, Ee Mungu, ni mfalme wangu tangu zamani,
unaleta wokovu duniani.
1374:13 Isa 51:9; 27:1; Eze 29:3; 32:2; Kut 14:21Ni wewe uliyeigawanya bahari kwa uweza wako;
ulivunja vichwa vya wanyama wakubwa wa kutisha katika maji.
1474:14 Hes 14:9; Za 72:9; Ay 3:8; Isa 13:21; 23:13; 34:14; Yer 50:39Ni wewe uliyeponda vichwa vya Lewiathani74:14 Lewiathani ni mnyama mkubwa wa baharini mwenye magamba anayefanana na joka kubwa, mwenye umbo la kutisha, asiyeweza kuvuliwa.
nawe ukamtoa kama chakula
kwa viumbe vya jangwani.
1574:15 Kut 14:29; 17:6; Hes 20:11; Isa 11:16; Hab 3:9; Ufu 16:12; Yos 2:10Ni wewe uliyefungua chemchemi na vijito,
ulikausha mito ambayo ilikuwa ikitiririka daima.
1674:16 Mwa 1:16; Za 136:7-9Mchana ni wako, nao usiku ni wako pia,
uliziweka jua na mwezi.
1774:17 Mdo 17:26; Kum 32:8; Mwa 8:22Ni wewe uliyeiweka mipaka yote ya dunia,
ulifanya kiangazi na masika.
1874:18 Ufu 16:19; Kum 32:9Ee Bwana, kumbuka jinsi mtesi alivyokudhihaki,
jinsi watu wapumbavu walivyolitukana jina lako.
1974:19 Mwa 8:8; Isa 59:11; Za 9:18Usiukabidhi uhai wa njiwa wako kwa wanyama wakali wa mwitu;
usisahau kabisa uhai wa watu wako wanaoteseka milele.
2074:20 Mwa 6:18; 17:7; Law 26:44; Yer 33:21; Ay 34:22Likumbuke agano lako,
maana mara kwa mara mambo ya jeuri
yamejaa katika sehemu za giza nchini.
2174:21 Isa 58:10; Za 9:9, 18; 10:18; 103:6; 35:10Usiruhusu walioonewa warudi nyuma kwa aibu;
maskini na wahitaji hebu walisifu jina lako.
2274:22 Za 17:13; 53:1Inuka, Ee Mungu, ujitetee;
kumbuka jinsi wapumbavu
wanavyokudhihaki mchana kutwa.
2374:23 Isa 31:4; Za 65:7; 46:6; Hes 25:17Usipuuze makelele ya watesi wako,
ghasia za adui zako, zinazoinuka mfululizo.
第74篇
祈求上帝眷顾祂的子民
亚萨的训诲诗。
1上帝啊,
你为何永远丢弃了我们?
你为何对自己草场上的羊大发雷霆?
2求你眷顾你古时买赎的子民,
你救赎为产业的族类,
求你眷顾你所居住的锡安山。
3求你前往那久已荒废之地,
看看敌人对圣所的破坏。
4你的仇敌在你的圣所咆哮,
他们竖立起自己的旗帜。
5他们大肆毁坏,
好像人抡起斧头砍伐树林。
6他们用斧头、锤子把雕刻的墙板都捣毁了。
7他们纵火焚烧你的圣所,
把它夷为平地,
亵渎了你的居所。
8他们心里说:“我们要全部摧毁。”
于是他们烧毁了境内所有敬拜上帝的地方。
9我们再也看不到你的征兆,
先知也没有了。
无人知道这一切何时才会结束。
10上帝啊,
仇敌嘲笑你的名要到何时呢?
他们要永无休止地辱骂你吗?
11你为何不伸出大能的右手?
求你出手给他们致命的一击。
12上帝自古以来就是我的王,
祂给世上带来拯救。
13你曾用大能分开海水,
打碎水中巨兽的头。
14你曾打碎海怪的头,
把它丢给旷野的禽兽吃。
15你曾开辟泉源和溪流,
也曾使滔滔河水枯干。
16白昼和黑夜都属于你,
你设立了日月。
17你划定地上的疆界,
又创造盛夏和寒冬。
18耶和华啊,
求你记住敌人对你的嘲笑和愚妄人对你的亵渎。
19求你不要把你的子民交给仇敌74:18‑19 “子民”希伯来文是“鸽子”;“仇敌”希伯来文是“野兽”。,
不要永远忘记你受苦的子民。
20求你顾念你立的约,
因地上黑暗之处充满了暴力。
21求你不要让受压迫的人羞愧而去。
愿贫穷困苦的人赞美你的名。
22上帝啊,求你起来维护自己,
别忘记愚妄人怎样整天嘲笑你。
23不要忽视你仇敌的喧嚷,
或者你对头的连连叫嚣。