Zaburi 73 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 73:1-28

KITABU CHA TATU

(Zaburi 73–89)

Zaburi 73

Haki Ya Mungu

Zaburi ya Asafu.

173:1 Za 24:4; 5:8Hakika Mungu ni mwema kwa Israeli,

kwa wale ambao mioyo yao ni safi.

273:2 Kum 32:35; Za 69:2; Efe 4:27Bali kwangu mimi, miguu yangu ilikuwa karibu kuteleza;

nilikuwa karibu mguu wangu kuachia uliposimama.

373:3 Mit 3:31; 23:17; 24:1-2; Ay 9:24; 21:7; Yer 12:1; Mal 3:15Kwa maana niliwaonea wivu wenye kujivuna

nilipoona kufanikiwa kwa waovu.

4Wao hawana taabu,73:4 Tafsiri nyingine zinasema: hawana maumivu katika kufa kwao.

miili yao ina afya na nguvu.

573:5 Za 73:12; Eze 23:42Hawapati shida zinazowataabisha watu wengine,

wala hawapati mapigo kama wanadamu wengine.

673:6 Law 26:19; Mwa 6:11; 41:42; Wim 4:9; Eze 16:11; Mit 4:17; Mhu 8:11Kwa hiyo kiburi ni mkufu wao,

wamejivika jeuri.

773:7 Za 7:10Uovu hutoka katika mioyo yao iliyokufa ganzi,

majivuno maovu kutoka mioyoni mwao hauna kikomo.

873:8 Za 10:7; 12:5; 41:5; Eze 25:15; Kol 3:8; 2Pet 2:18; Yud 16Hudhihaki na kusema kwa ukorofi,

katika majivuno yao wanatishia kutesa.

973:9 Ufu 13:6Vinywa vyao huweka madai hata kwa mbingu,

nazo ndimi zao humiliki duniani.

10Kwa hiyo watu wao huwageukia

na kunywa maji tele.73:10 Au: na kupokea yote wasemayo.

1173:11 Ay 22:13; Za 94:7Wanasema, “Mungu awezaje kujua?

Je, Yeye Aliye Juu Sana anayo maarifa?”

1273:12 Za 73:5; 49:6Hivi ndivyo walivyo waovu:

siku zote hawajali,

wanaongezeka katika utajiri.

1373:13 Ay 9:29-31; 21:15; Za 24:4; Mal 3:14; Mwa 44:16; Ebr 10:19-22Hakika nimeuweka moyo wangu safi bure,

ni bure nimenawa mikono yangu nisiwe na hatia.

1473:14 Za 73:5Mchana kutwa nimetaabika,

nimeadhibiwa kila asubuhi.

15Kama ningesema, “Nitasema hivi,”

ningelikuwa nimewasaliti watoto wako.

1673:16 Mhu 8:17Nilipojaribu kuelewa haya yote,

yalikuwa magumu kwangu kuelewa.

1773:17 Kut 15:17; Ay 8:13; Flp 3:19; Za 15:1; 77:13Mpaka nilipoingia patakatifu pa Mungu,

ndipo nilipotambua mwisho wao.

1873:18 Kum 32:35; Za 35:6; 17:13Hakika unawaweka mahali pa utelezi,

unawaangusha chini kwa uharibifu.

1973:19 Kum 28:20; Mit 24:22; Isa 47:11; Mwa 19:15Tazama jinsi wanavyoangamizwa ghafula,

wanatoweshwa kabisa na vitisho!

2073:20 Za 78:65; Isa 29:8; Ay 20:8; Mit 12:11; 28:19Kama ndoto mtu aamkapo,

hivyo wakati uinukapo, Ee Bwana,

utawatowesha kama ndoto.

21Wakati moyo wangu ulipohuzunishwa,

na roho yangu ilipotiwa uchungu,

2273:22 Za 49:10; 92:6; 49:12, 20; Mhu 3:18; 9:12nilikuwa mpumbavu na mjinga,

nilikuwa mnyama mkatili mbele yako.

2373:23 Mwa 48:13Hata hivyo niko pamoja nawe siku zote,

umenishika mkono wangu wa kuume.

2473:24 Za 48:14; 1Fal 22:5; Isa 58:8; Yn 14:3; 2Kor 5:1Unaniongoza kwa shauri lako,

hatimaye utaniingiza katika utukufu.

2573:25 Za 16:2; Flp 3:8Nani niliye naye mbinguni ila wewe?

Dunia haina chochote ninachokitamani ila wewe.

2673:26 Kum 32:9; Za 18:1; 84:2; 31:10; 40:12Mwili na moyo wangu vyaweza kushindwa,

bali Mungu ni nguvu ya moyo wangu

na fungu langu milele.

2773:27 Za 34:21; Law 6:2; Yer 5:11; Hos 4:12; 9:1Wale walio mbali nawe wataangamia,

unawaangamiza wote wasio waaminifu kwako.

2873:28 Sef 3:2; Yak 4:8; Za 40:5; 26:7; 9:9; Ebr 10:22Lakini kwangu mimi,

ni vyema kuwa karibu na Mungu.

Nimemfanya Bwana Mwenyezi kimbilio langu;

nami nitayasimulia matendo yako yote.