Zaburi 72 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 72:1-20

Zaburi 72

Maombi Kwa Ajili Ya Mfalme

Zaburi ya Solomoni.

172:1 Kum 1:16; Za 9:8Ee Mungu, mjalie mfalme aamue kwa haki yako,

mwana wa mfalme kwa haki yako.

272:2 Isa 11:2, 4, 5; 16:5; 9:7; Yer 23:5; 33:15Atawaamua watu wako kwa haki,

watu wako walioonewa kwa haki.

3Milima italeta mafanikio kwa watu,

vilima tunda la haki.

472:4 Za 27:11; 76:9; 9:12; Isa 49:13; 11:4; 29:19; 32:7Atawatetea walioonewa miongoni mwa watu

na atawaokoa watoto wa wahitaji,

ataponda mdhalimu.

572:5 1Sam 13:13; Za 33:11Atadumu kama jua lidumuvyo, kama mwezi, vizazi vyote.

672:6 Kum 32:2Atakuwa kama mvua inyeshayo juu ya shamba lililofyekwa,

kama manyunyu yanyeshayo ardhi.

772:7 Za 92:12; Mit 14:11Katika siku zake wenye haki watastawi;

mafanikio yatakuwepo mpaka mwezi utakapokoma.

872:8 Kut 23:31; 1Fal 4:21; Zek 9:10Atatawala kutoka bahari hadi bahari

na kutoka Mto72:8 Yaani Mto Frati. mpaka miisho ya dunia.

9Makabila ya jangwani watamsujudia,

na adui zake wataramba mavumbi.

1072:10 Mwa 10:4, 7; Es 10:1; 1Fal 9:16; 2Nya 9:24Wafalme wa Tarshishi na wa pwani za mbali

watamletea kodi;

wafalme wa Sheba na Seba

watampa zawadi.

1172:11 Mwa 27:29; Ezr 1:2Wafalme wote watamsujudia

na mataifa yote yatamtumikia.

12Kwa maana atamwokoa mhitaji anayemlilia,

aliyeonewa asiye na wa kumsaidia.

1372:13 Isa 60:10; Yoe 2:18; Lk 10:33Atawahurumia wanyonge na wahitaji

na kuwaokoa wahitaji kutoka mauti.

1472:14 Za 69:18; Eze 13:23; 34:10; 1Sam 26:21Atawaokoa kutoka uonevu na ukatili,

kwani damu yao ni ya thamani machoni pake.

1572:15 Mwa 10:7; Za 35:28Aishi maisha marefu!

Na apewe dhahabu ya Sheba.

Watu wamwombee daima

na kumbariki mchana kutwa.

1672:16 Eze 34:27; Isa 4:2; 27:6; 44:4; 58:11; 66:14; Mwa 27:18; Hes 22:4; Za 4:7; 92:12; 104:16Nafaka ijae tele katika nchi yote,

juu ya vilele vya vilima na istawi.

Tunda lake na listawi kama Lebanoni,

listawi kama majani ya kondeni.

1772:17 Kut 3:15; Lk 1:48; Za 89:36; Mwa 12:3Jina lake na lidumu milele,

na lidumu kama jua.

Mataifa yote yatabarikiwa kupitia kwake,

nao watamwita aliyebarikiwa.

1872:18 1Nya 29:10; Za 41:13; 106:48; Lk 1:68; Ay 5:9Bwana Mungu, Mungu wa Israeli, apewe sifa,

yeye ambaye peke yake hutenda mambo ya ajabu.

1972:19 2Sam 7:26; Hes 14:21; Za 41:13Jina lake tukufu lisifiwe milele,

ulimwengu wote ujae utukufu wake.

Amen na Amen.

2072:20 Rut 4:17Huu ndio mwisho wa maombi ya Daudi mwana wa Yese.