Zaburi 71 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 71:1-24

Zaburi 71

Kuomba Ulinzi Na Msaada Siku Zote Za Maisha

171:1 Kum 23:15; Rut 2:12; Za 22:5Ee Bwana, nimekukimbilia wewe,

usiache nikaaibika kamwe.

271:2 2Fal 19:1671:2 Kut 34:6Kwa haki yako uniponye na kuniokoa,

unitegee sikio lako uniokoe.

371:3 Za 18:2Uwe kwangu mwamba wa kimbilio,

mahali nitakapokimbilia kila wakati;

toa amri ya kuniokoa, kwa kuwa wewe

ni mwamba wangu na ngome yangu.

471:4 2Fal 19:19; Za 140:4; Mwa 48:16Ee Mungu wangu uniokoe kutoka kwenye mkono wa mwovu,

kutoka kwenye makucha ya watu wabaya na wakatili.

571:5 Za 9:18; 25:5; Ay 4:6; Yer 17:7Kwa kuwa umekuwa tumaini langu, Ee Bwana Mwenyezi,

tegemeo langu tangu ujana wangu.

671:6 Ay 3:16; Za 9:1; 22:9; 34:1; 52:9; 119:164; 145:2Tangu kuzaliwa nimekutegemea wewe,

ulinitoa tumboni mwa mama yangu.

Nitakusifu wewe daima.

771:7 Kum 28:46; 1Kor 4:9; Za 61:3; 2Sam 22:3Nimekuwa kama kioja kwa wengi,

lakini wewe ni kimbilio langu imara.

871:8 Za 71:15; 51:15; 63:5; 96:6; 104:1Kinywa changu kimejazwa sifa zako,

nikitangaza utukufu wako mchana kutwa.

971:9 Za 51:11; 92:14; Kum 4:31; 31:6Usinitupe wakati wa uzee,

wala usiniache nguvu zangu zinapopungua.

1071:10 Za 3:7; 10:8; 59:3; 31:13; Mt 1:10; 12:14Kwa maana adui zangu wananisengenya,

wale wanaonivizia kuniua wafanya hila.

1171:11 Isa 40:27; 54:7; Mt 27:46; Za 7:2; 9:10; Mao 5:20Wanasema, “Mungu amemwacha,

mkimbilieni mkamkamate,

kwani hakuna wa kumwokoa.”

1271:12 Za 38:21, 22; 22:19Ee Mungu, usiwe mbali nami,

njoo haraka kunisaidia, Ee Mungu wangu.

1371:13 Ay 8:22; Za 15:3; 70:2; Yer 18:19Washtaki wangu na waangamie kwa aibu,

wale wanaotaka kunidhuru

na wafunikwe kwa dharau na fedheha.

1471:14 Za 25:3; 42:5; 130:7; 131:3Lakini mimi, nitatumaini siku zote,

nitakusifu zaidi na zaidi.

1571:15 Za 71:8; 66:6; 51:14Kinywa changu kitasimulia haki yako,

wokovu wako mchana kutwa,

ingawa sifahamu kipimo chake.

1671:16 Za 77:12; 106:2; 118:15; 9:1; 145:4Ee Bwana Mwenyezi, nitakuja

na kutangaza matendo yako makuu,

nitatangaza haki yako, yako peke yako.

1771:17 Yer 7:13; Ay 5:9; Za 26:7; 86:10; 96:3; Kum 4:5Ee Mungu, umenifundisha tangu ujana wangu,

hadi leo ninatangaza matendo yako ya ajabu.

1871:18 Isa 46:4; Kut 9:16; Ay 8:8; Yoe 1:3; Za 78:4; 145:4; 22:30, 31Ee Mungu, usiniache,

hata niwapo mzee wa mvi,

mpaka nitangaze uwezo wako kwa kizazi kijacho,

nguvu zako kwa wote watakaokuja baadaye.

1971:19 Lk 1:49; Za 36:5; 35:10; 77:13; 89:8; 126:2Ee Mungu, haki yako imefika juu katika mbingu,

wewe ambaye umefanya mambo makuu.

Ee Mungu, ni nani aliye kama wewe?

2071:20 Za 80:3, 19; 25:17; 85:4; 63:9; Hos 6:2Ingawa umenifanya nipate taabu, nyingi na chungu,

utanihuisha tena,

kutoka vilindi vya dunia

utaniinua tena.

2171:21 Za 18:35; 86:17; Isa 12:1; 40:1, 2; 49:13; 54:10Utaongeza heshima yangu

na kunifariji tena.

2271:22 Za 33:2; 92:3; 144:9; Ay 21:12; 2Fal 19:22Ee Mungu wangu, nitakusifu kwa kinubi

kwa ajili ya uaminifu wako;

Ee Uliye Mtakatifu wa Israeli,

nitakuimbia sifa kwa zeze.

2371:23 Za 20:5; Kut 15:13Midomo yangu itapaza sauti kwa furaha

ninapokuimbia sifa,

mimi, ambaye umenikomboa.

2471:24 Za 35:28; Es 9:2Ulimi wangu utasimulia matendo yako ya haki

mchana kutwa,

kwa maana wale waliotaka kunidhuru,

wameaibishwa na kufadhaishwa.