Zaburi 65 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 65:1-13

Zaburi 65

Kusifu Na Kushukuru

Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Wimbo.

165:1 Kum 23:21; Za 2:6; 116:18Ee Mungu, sifa zakungojea katika Sayuni;

kwako wewe nadhiri zetu zitatimizwa.

265:2 Za 86:9; Isa 66:23; Lk 11:9, 10Ewe usikiaye maombi,

kwako wewe watu wote watakuja.

365:3 Za 40:12; 79:9; Rum 3:25; Ebr 9:14Tulipokuwa tumefunikwa kabisa na dhambi,

wewe ulisamehe makosa yetu.

465:4 Hes 16:5; Za 33:12; 36:8Heri wale uliowachagua

na kuwaleta karibu ili waishi katika nyua zako!

Tunashibishwa kwa mema ya nyumba yako,

mema ya Hekalu lako takatifu.

565:5 Kum 4:34; Isa 64:3; Za 107:23; 18:46; 68:19; 85:4; 45:4; 48:10; 106:22Unatujibu kwa matendo ya kushangaza ya haki,

Ee Mungu Mwokozi wetu,

tumaini la miisho yote ya duniani

na la bahari zilizo mbali sana,

665:6 Amo 4:13; Isa 51:9; Za 18:1; 93:1uliyeumba milima kwa uwezo wako,

ukiwa umejivika nguvu,

765:7 Za 139:20; 89:9; 74:23; 2:1; 93:3, 4; 107:29; Mt 8:26; Kum 32:41; Isa 17:12-13uliyenyamazisha dhoruba za bahari,

ngurumo za mawimbi yake,

na ghasia za mataifa.

865:8 Ay 37:5; Za 100:2; 107:22; 126:2; Isa 24:16; 52:9Wale wanaoishi mbali sana

wanaogopa maajabu yako,

kule asubuhi ipambazukiapo

na kule jioni inakofifilia

umeziita nyimbo za furaha.

965:9 Za 104:14, 24; 68:9, 10; Law 26:4; Mwa 27:28; Kum 32:14Waitunza nchi na kuinyeshea,

waitajirisha kwa wingi.

Vijito vya Mungu vimejaa maji

ili kuwapa watu nafaka,

kwa maana wewe umeviamuru.

1065:10 Kum 32:2; 2Sam 1:21; Ay 36:28; Mdo 14:17Umeilowesha mifereji yake

na kusawazisha kingo zake;

umeilainisha kwa manyunyu

na kuibariki mimea yake.

1165:11 Kum 28:12; Za 104:3, 28; 147:14; Yn 10:10; Lk 6:38Umeuvika mwaka taji ya baraka,

magari yako yanafurika kwa wingi.

1265:12 Ay 28:26; Yoe 2:22; Za 98:8Mbuga za majani za jangwani umezineemesha;

vilima vimevikwa furaha.

1365:13 Za 72:16; 98:8; 144:13; Zek 8:12; Isa 55:12; 44:23; 49:13; 30:33; 14:8Penye nyanda za malisho pamejaa makundi ya wanyama,

na mabonde yamepambwa kwa mavuno;

vyote vinashangilia kwa furaha na kuimba.