Zaburi 64 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 64:1-10

Zaburi 64

Kuomba Ulinzi Dhidi Ya Maadui

Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.

164:1 Za 142:2; 140:1Ee Mungu, unisikie ninapoeleza lalamiko langu,

uyahifadhi maisha yangu kutokana na vitisho vya adui.

264:2 Za 56:6; 59:2; 143:9; Kut 1:10Unifiche kutokana na shauri la siri la waovu,

kutokana na zile kelele za kundi la watenda mabaya.

364:3 Za 7:13; 58:7; 57:4; 55:21; Isa 49:2Wananoa ndimi zao kama panga

na kuelekeza maneno yao kama mishale ya kufisha.

464:4 Za 10:8; 11:2; 55:19; Ay 9:23Hurusha mishale kutoka kwenye mavizio kwa mtu asiye na hatia,

humrushia ghafula bila woga.

564:5 Za 91:3; 140:5; 119:110; 141:9; Ay 22:13Kila mmoja humtia moyo mwenzake

katika mipango mibaya;

huzungumza juu ya kuficha mitego yao,

nao husema, “Ni nani ataiona?”

6Hufanya shauri baya la dhuluma na kusema,

“Tumebuni mpango mkamilifu!”

Hakika nia na moyo wa mwanadamu vina hila.

7Bali Mungu atawapiga kwa mishale,

nao ghafula wataangushwa.

864:8 Mit 12:13; 18:7; 2Fal 10:21; Za 109:25; 59:12; Kum 28:37Atageuza ndimi zao wenyewe dhidi yao

na kuwaleta kwenye maangamizi;

wote wawaonao watatikisa vichwa vyao

kwa dharau.

964:9 Za 40:3; Yer 51:10Wanadamu wote wataogopa,

watatangaza kazi za Mungu

na kutafakari yale aliyoyatenda.

1064:10 Ay 22:19Wenye haki na wafurahi katika Bwana,

na wakimbilie kwake;

wanyofu wote wa moyo na wamsifu yeye!